Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kwa miaka 33, tangu mwaka 1991 taifa la Bangladesh limetawaliwa na wanawake wawili mawaziri wakuu kwa vipindi tofauti kwa kila mmoja wakipokezana miaka mitano mitano. Aliyeanza kutawala alikuwa Khaleda Zia kisha akaja Sheikh Hasina halafu akarudia Zia tena ndipo akarudi Hasina tena kuanzia mwaka 2009 mpaka sasa alipotimuliwa na waandamanaji.
Wote wawili wametokea katika familia za Urais au Marais. Sheikh Hasina ni mtoto wa Rais wa Kwanza wa Bangladesh ambaye aliongoza mapambano ya Bangladesh kujitenga kutoka India na ambaye baadaye alipunduliwa na kuuwawa na wanafamilia wake wengi, Khaleda Zia ni mke mjane wa Rais aliyepindua nchi kijeshi kabla na yeye kupinduliwa tena baadaye.
Wanawake wote wawili waliibuka kama marafiki wapigania demokrasia na wanamegeuzi waliogeuka baadaye kuwa mahasimu, mafisadi na madikteta.
Enzi za uhasama kulikuwa na vurugu nyingi za kisiasa, kutekana na kuuana kati ya kambi zao. Sheikh Hasina aliweza kujisimika mamlakani vizuri zaidi kama waziri mkuu mwenye nguvu na kumfunga hasimu wake na rafiki yake wa zamani Zia kifungo cha gerezani, leo hii Hasina alivyotimuliwa na waandamanaji Rais wa Bangladesh kaamuru Zia na wafungwa wengine wa kisiasa kuachiwa huru!