Historia ya Brig. Jen. Ambrose Bayeke, Shujaa wa vita vya Kagera

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
Wana historia wa vita vya Kagera / Uganda wamekuwa wakiwataja makamanda wakuu wa vita hivyo waliokuwa na vyeo vya Brigedia kwenda juu.

Majina kama Abdalah Twalipo, Tumainieli Kiwelu, John Walden, Ahmed Kitete, na wengine yametajwa zaidi ktk historia ya vita vya Kagera.

Lakini chini ya makamanda hao walikuwepo wakuu wa vikosi ambao walipiganisha vita hiyo. Miongoni mwao walikuwepo Lt.Col. Lupembe, Lt.Col. Msuya, Lt.Col. Kisanko, Lt.Col. Bayeke, na wengine.

Hapo chini kuna historia ya Brig.Jen.Ambrose Bayeke ambaye wakati wa vita vya Kagera alikuwa Mkuu wa vikosi mojawapo ktk vita hiyo.

1722740978160.png

I am quite pleased to announce that my book Ujamaa’s Army: The Creation and Evolution of the Tanzania People’s Defence Force 1964-1979 is now officially under contract with Ohio's War and Militarism in African History series. Look for it in print in 2023!

Author Charlie Thomas
 
View attachment 3060926
Major general John Butler Walden of TPDF
Huyu alikuwa mtemi kweli; mwenyezi mungu aipumzishe roho yake pema peponi. Pamoja na uchotara wake, alilitumikia jeshi letu kwa uzalendo wa hali ya juu sana kama mmatumbi mwenzetu tu. Kwake kula ugali kwa maharage na kisanvu ilikuwa kama kawaida tu.
 
Wana historia wa vita vya Kagera / Uganda wamekuwa wakiwataja makamanda wakuu wa vita hivyo waliokuwa na vyeo vya Brigedia kwenda juu.

Majina kama Abdalah Twalipo, Tumainieli Kiwelu, John Walden, Ahmed Kitete, na wengine yametajwa zaidi ktk historia ya vita vya Kagera.

Lakini chini ya makamanda hao walikuwepo wakuu wa vikosi ambao walipiganisha vita hiyo. Miongoni mwao walikuwepo Lt.Col. Lupembe, Lt.Col. Msuya, Lt.Col. Kisanko, Lt.Col. Bayeke, na wengine.

Hapo chini kuna historia ya Brig.Jen.Ambrose Bayeke ambaye wakati wa vita vya Kagera alikuwa Mkuu wa vikosi mojawapo ktk vita hiyo.

Thanks for this
P
 
Ni kweli kuna machotara wengi haswa wa Iringa na baadhi ya wageni walikuwa wazalendo wa kweli wa nchi hii kuliko wenyeji.

Baadhi yao ni Amiri Jamal ndie alimjengea Nyerere ile nyumba pale Magomeni.

Kuna Dr Leader Sterling, kuna Bert Shackland alishiriki na kushinda mbio za magari za East Africa Safari Rally.

Kuna AL Noor Kussum,kuna machotara wengi wa Iringa waliingia polisi na jeshini wakiongozwa na Hans Poppe alikuwa RPC Bukaba akauliwa na bomu Iddi Amini alipoivamia Tanzania mara ya kwanza mwaka 1971.

Kwa hasira za kifo cha baba yao watoto wake wawili wa kiume wakaingia jeshini JWTZ, na wote walishiriki Vita vya Kagera na baada ya vita wote wawili walishiriki ule uhaini wa 1982 kutaka kumpindua Nyerere.

Jeshini kulikuwa na machotara wengi wa Iringa mmoja wao ni Brigadier Cuthless huyu alipenda kutumia pikipiki kama mimi mpaka anakufa uzeeni kabisa bado anavuta mashine!. Pia kuna Tax baba yake Dr Stagomena Tax.

Kufuatia nchi yetu kutawaliwa na mfumo dume wazalendo wa kike wa nchi hii waliojitolea maisha yao yote hawatajwi kabisa miongoni ma mashujaa wa taifa hili, kapo kabinti kamoja ka Kiingereza kalikuja Tanzania enzi za usichana wake, Joan Wickens ,kalikuwa PA wa Mwalimu Nyerere miaka yote 23 ya urais wake na akaendelea nae mpaka Nyerere amekufa ndipo kikarejea kwao Uingereza kikiwa kibibi hakikuwahi kuolewa wala kupata mtoto usichana wake wote kamemalizia kwa Nyerere.

Kiukweli Tanzania tuna mashujaa wengi unsung heroes and heroines worth properly documented vinginevyo historia zao na ushujaa wao utafutika na kupotea, na mimi kwa vile ni mtoto wa miongoni mashujaa hawa wazalendo nitajitahidi kufanya kitu and charty begins at home Tribute to Silent Heroes!. Hongera “Idara” Kuhudumia Wastaafu Wake Till Death!”. Jee Huu Sio Ubaguzi?. Why Only Some are Cared to Death but not All?!

Brigadia Lupembe...Brigadia Kisanko....daah
 
Huyu mama,Joan Wickens, naamini ameandika kitu, kitakuja kubadili mambo mengi sana ya nchi yetu...miaka 30 baada ya kifo chake inazidi kupungua...na wale walioweza kuzima maandishi yake nao pia wamepungua.. either nguvu zimepungua au wapo kwenye makao yenye haki, maana mwenye nguvu na asiye nazo wote lao moja
 
Back
Top Bottom