Historia ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Hey pals,,

I hope mko poa

Kwanza tuanze kwa kibwagizo kidogo tu
👇

Baba uliye juu mbinguni,wewe ndo Baba wa taifa,,/
Huyu Baba tuliye pewa hana lolote ni sifa,,,/

Hizo ni line nilizo kuta kwenye clip moja huko you tube ya jamaa mmoja akifanya freestyle kwenye Dakika kumi za maangamizi ambayo huwa segment inayo ruka kwenye kipindi cha planet bongo East Africa radio.
Kusema ukweli sikumwelewa jamaa alicho maanisha ila nilipenda tu jamaa alivyo kuwa akiflow na kumpa sifa Baba yetu aliye mbinguni (MUNGU).

Okay tuacheni hiyo,

Nimekuwa nikifuatilia matamko ya viongozi wa chama hiki bila kusahau Kinaitwa CCM,kama nimekosea jina lake vizuri mtanikosoa wadau,Matamko ya viongozi wa chama hiki kwenye awamu hii ya tano ni tofauti kabisa na awamu zingine zilizo pita,kwa ufupi ni kuwa wanajiamini kupitiliza kiasi kwamba naanza kuwaza baadhi ya vitu,

Moja ya maswali ninayo jiuliza ni haya hapa

👉Walio kianzisha chama hiki walifikiria kuwa ipo siku kuna chama kingine kitakuja kuchukua utawala wa nchi hii?

👉Au kilianzishwa ili kitawale milele?,Na kama Kilianzishwa kitawale milele nini kilifanya Hao watu waanzishe mfumo wa vyama vingi?

👉Je,mfumo wa vyama vingi ni kiini macho tu?

👉Je,haya mambo yanayo fanywa awamu hii ya kuminya demokrasia ndo yalikuwa ni moja ya mikakati ya kuanzishwa chama hiki? viongozi walio pita awamu zingine mbona hatukuyashuhudia haya? Au waliogopa kuyafanya kwa kuwa walikuwa na roho ya utu huku wakienda kinyume na mikakati ya chama chao?

👉Je,Awamu hii ya tano ndo kapatikana kiongozi ambaye anafanya Yale yote ambayo waasisi wa chama hiki waliyaweka kwenye mikakati yao?

👉Au uwezo mdogo wa viongoz wa awamu hii kujibu hoja ndo Ume wafanya CCM kuwabana upinzani?

NB: Kwa yanayo endelea kwa sasa hapa nchini ni kuwa CCM hawataki kutoka madarakani kwa kura labda kuna njia nyingine wanataka upinzani wafanye.

CCM lazima itoke madarakani kwa kura, ila kabla ya kura lazima viongozi wa upinzani wafanye kitu.

Jimmy-De-Lite
 
Hatuna mbadala wa Ccm kwa miaka 50 ijayo

Tusije tukaingizwa vitani na walafi wa madaraka

Zimwi likujualo....
 
Hangaikeni na kuzama kwa chadema CCM iacheni kama ilivyo ni mlima mrefu sana


State agent
 
Ni punguani anaweza kudhani kuna mbadala wa CCM. Tulidhani CHADEMA kingeweza kumbe kilikuwa chama cha Vibaraka wa mabeberu wakaanza kugombana wenyewe kwa wenyewe walivyoona wanaungwa mkono. Watanzania tumekishitukia hicho chama ndo maana kimeangukia pua na hakitainuka milele. Bora CCM itawale milele kuliko vyama vya kikabila kama CHADEMA, vya udini kama CUF na sasa ACT kimekuwa na mlengo wa udini
 
Akili yako fupi kama maisha ya funza.
 
Akili yako fupi kama maisha ya funza.
Magufuli ni moto wa kuotea mbali. Mlidhani mtaleta nyodo mlizokuwa mnamletea mkwere anawachekea? Magufuli kawasoma kuwa hamjui sheria pia CHADEMA woote vilaza. Mmeshindwa kufuata katiba ya chana chenu kumuondoa Mbowe kwenye uwenyekiti wakati muda wake uliisha kitambo ndo muje kukiondoa CCM madarakani? Kujaza form tu za kugombea uwenyekiti wa serikali za mtaa mmeshindwa alafu eti mnazila na kugonea uchaguzi. Kagomeni CCM itaendelea kutawala milele. Magufuli anacheza na akili zenu mbovu
 
Akili yako fupi kama maisha ya funza.
Magufuli ni moto wa kuotea mbali. Mlidhani mtaleta nyodo mlizokuwa mnamletea mkwere anawachekea? Magufuli kawasoma kuwa hamjui sheria pia CHADEMA woote vilaza. Mmeshindwa kufuata katiba ya chana chenu kumuondoa Mbowe kwenye uwenyekiti wakati muda wake uliisha kitambo ndo muje kukiondoa CCM madarakani? Kujaza form tu za kugombea uwenyekiti wa serikali za mtaa mmeshindwa alafu eti mnazila na kugonea uchaguzi. Kagomeni CCM itaendelea kutawala milele. Magufuli anacheza na akili zenu mbovu
 
Kuna muda huwa nafikia hatua ya kumlaumu Mwalimu, yaani kabla ya kuondoka angekivunja hili dude...kuna muda lilitaka eti kumgeuka haya yeye mwenyewe...akatoka Butiama moja kwa moja hadi Dodoma ndani kikaoni...yaliyotokea humo wanayajua.
 
Tulia wewe, Uchaguzi mdogo tu huu unawashinda kuandaa na kuukamilisha....aibu kubwa mnalipaka Taifa.
 
Ukweli mtupu tuutafakari tujue nini cha kufanya.
 
LKN pia CCM ndicho chama pekee kisichofungamana na kabira lolote,ukanda wowote au dini yoyote, CCM ni chama cha watanźania woote,bira kujari makabira yako na dini zao
Ndabaningi...
Utahitaji utafiti wa kisayansi kusadikisha hoja zako.

Tanzania ukabila si tatizo toka ukoloni wala ukanda ni hisia zilizo chini sana.

Tatizo la Tanzani ni udini.
Fanya utafiti.
 
Unapoitamka Tanzania maana ake ni toka 1964,unapoitamka tanganyika maana ake ni baada ya ukoloni miaka ya1961,nyuma ya hapo ni hakuna tanganyika wala Tanzania,ila ila kuna Dutch ost africa, ya wakoloni, hapo unaiona tanganyika,Uganda,na kenya vikiwa chini ya mtawala mmoja mkoloni,swali langu ni kwa nn kenya kuna ukabila na uganda kuna ukabila,?! Na Tanzania pana utulivu kw nn,!? Ccm ipo madarakani toka mwaka 1958 baada ya uchaguz wa balaza la legco na nyerere kuwa wazir mkuu wa kwanza tanganyika.kw nn ccm ipo mpk leo na haiteteleki inazidi kuimalika?.wewe kw akii yako haya yanatokea kw kudra za mwenyez mungu au ni kwa bahati mbaya tu?
 
Ndabaningi...
Utahitaji utafiti wa kisayansi kusadikisha hoja zako.

Tanzania ukabila si tatizo toka ukoloni wala ukanda ni hisia zilizo chini sana.

Tatizo la Tanzani ni udini.
Fanya utafiti.
Mzee mohamedi tanzania kuna udini???. Hebu fafanua mkuu unijuze?.
 
LKN pia CCM ndicho chama pekee kisichofungamana na kabira lolote,ukanda wowote au dini yoyote, CCM ni chama cha watanźania woote,bira kujari makabira yako na dini zao

Hakuna kitu kinaitwa kabira rudi shuleni kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…