Kijana, hilo Baraza la Mitihani Tanzania (National Examination Council of Tanzania aka NECTA) ambalo wewe ndilo lilikutahini, lilianzishwa mwaka 1971. Kabla ya hapo kulikuwa na baraza la mitihani nchi zote za Afrika Mashariki (Tanzania, Kenya na Uganda) ie The East Africa Examination Council ambalo lililosimamiwa na Uingereza na mitihani yake ilitungwa na Cambridge University huko London.
The Ordinary Level Certificate ilikuwa ina incorporate a General Certificate of Education (GCE) ambayo ni ya nchi zote za Jumuiya za Madola ya Muingereza zilizokuwa makoloni ya Muingereza.
Hivyo hata hiyo ACSEE ya Chenge ya mwaka 1968 ni Cambridge University na siyo ya NECTA kama ya kwako. Baada ya nchi zote za EA kujitoa kwenye baraza hilo la mitihani la Cambridge University mwaka 1971, ndipo kila nchi nchi hizo ikaanzisha baraza lake la mitihani na kutunga curriculum zake kwa wanafunzi wake wa shule za sekondari. Curriculum hizi hapa kwetu zimekuwa zilibadilishwa kila kukicha kwa matakwa ya wanasiasa hadi kupelekea elimu ya vijana wetu kushuka sana ukilinganisha na viwango vya kimataifa.
Kushuka huku kwa elimu ya vijana wetu ni hadi kwenye vyuo vikuu vyetu. Utakuta sasa mhitimu wa shahada ya udaktari wa binadamu hawezi kufanya operesheni ya kutoa kidole tumbo kwa mgonjwa wa acute appendicitis. Utakuta wahitimu hawa hawawezi kutoa mtoto kwa njia ya operesheni (Ceaserian Section) kwa mama mjamzito mwenye pingamizi la uzazi (obstructed labour) ili hali huko nyuma wahitimu ya diploma in medicine (AMO) waliweza kufanya operesheni hizo kwa ufanisi mkubwa.
Hivyo ndivyo kwa wahitimu wetu wa sasa kwa profession zote hususani wanasheria na wapelelezi wa kesi za jinai, wahandisi, wahasibu na kadhalika. Wanachokijua na walichobobea kwa sasa ni kupiga dili tu.