Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
HISTORIA YA KABURI LA ABUSHIRI BIN SALIM
Abushiri bin Salim alikamatwa sehemu za Handeni baada ya kusalitiwa akiwa anafanya mipango ya kutorekea Mombasa akiwakimbia Wajerumani.
Vita vyake vya mwisho dhidi ya Wajerumani ilikuwa Nzole karibu na Bagamoyo.
Jeshi lake lilishindwa kuhimili nguvu ya jeshi la Wajerumani likaparaganyika askari wake wengi waliuawa na wengine kukimbia kuokoa maisha yao.
Abushiri ilimdhihirikia wazi kuwa hatoweza tena kukusanya nguvu ya kupambana na Hermann von Wissmann.
Abushiri akiwa amefungwa minyororo na akiwa hana nguo za kumstiri alitembezwa katika barabara za Pangani kila mtu amuone.
Bwana mkubwa huyu, kijana tajiri na mfanyabishara maarufu alipitishwa katika hali hiyo kumfedhehesha na kufikisha ujumbe kwa wananchi wote kuwa Wajerumani wana nguvu ya kushinda vita na yeyote wataekabiliananae.
Ilikuwa ikisemwa kuwa kaburi la Abushiri halijulikani wapi alizikwa.
Lakini wenyeji wa Pangani wakijua wapi Abushiri amezikwa.
Kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingine baadhi ya watu Pangani wakijua wapi lilipo kaburi la Abushiri.
Abushiri alinyongwa tarehe 15 December 1889.
Leo nimepelekwa kuona mahali alipozikwa Abushiri na nilipotoka hapo nimekwenda kuuona msikiti wa Ibadh aliokuwa akisali.
Msikiti ule wa asili haupo mahali pake pamejengwa msikiti mwingine.
PIA SOMA
- Maajabu kuhusu Kaburi la Abushiri
View: https://youtu.be/Qp4-OQO9LIM