Historia ya Kaburi Abushiri bin Salim 1840 - 1889

Historia ya Kaburi Abushiri bin Salim 1840 - 1889

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
HISTORIA YA KABURI LA ABUSHIRI BIN SALIM

Abushiri bin Salim alikamatwa sehemu za Handeni baada ya kusalitiwa akiwa anafanya mipango ya kutorekea Mombasa akiwakimbia Wajerumani.

Vita vyake vya mwisho dhidi ya Wajerumani ilikuwa Nzole karibu na Bagamoyo.

Jeshi lake lilishindwa kuhimili nguvu ya jeshi la Wajerumani likaparaganyika askari wake wengi waliuawa na wengine kukimbia kuokoa maisha yao.

Abushiri ilimdhihirikia wazi kuwa hatoweza tena kukusanya nguvu ya kupambana na Hermann von Wissmann.

Abushiri akiwa amefungwa minyororo na akiwa hana nguo za kumstiri alitembezwa katika barabara za Pangani kila mtu amuone.

Bwana mkubwa huyu, kijana tajiri na mfanyabishara maarufu alipitishwa katika hali hiyo kumfedhehesha na kufikisha ujumbe kwa wananchi wote kuwa Wajerumani wana nguvu ya kushinda vita na yeyote wataekabiliananae.

Ilikuwa ikisemwa kuwa kaburi la Abushiri halijulikani wapi alizikwa.
Lakini wenyeji wa Pangani wakijua wapi Abushiri amezikwa.

Kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingine baadhi ya watu Pangani wakijua wapi lilipo kaburi la Abushiri.

Abushiri alinyongwa tarehe 15 December 1889.

Leo nimepelekwa kuona mahali alipozikwa Abushiri na nilipotoka hapo nimekwenda kuuona msikiti wa Ibadh aliokuwa akisali.

Msikiti ule wa asili haupo mahali pake pamejengwa msikiti mwingine.

PIA SOMA
- Maajabu kuhusu Kaburi la Abushiri

View: https://youtu.be/Qp4-OQO9LIM
 
Mzee Mohamed abushiri nasikia alikuwa rafiki yake Abdul sykes na mara nyingi swala ya jioni walikuwa wakienda wote? Yana ukweli haya mzee wangu?
Alikua rafiki mkubwa wa Chief Mkwawa pia.

Hata ujio wa Ujerumani Abushiri ndiye aliyemtumia barua Mkwawa na kumtahadharisha kuhusu WaJerumani.

Mkwawa ndio akajenga ngome ya Liringa ambayo wajerumani walijaribu kuingia wakashindwa.

Mpaka pale waluguru walipomsaliti Mkwawa.
 
Proved,
Abushiri mama yake ni Mwafrika kutoka Ethiopia.

Abushiri alisalitiwa na mtu mmoja anajulikana kwa jina moja Magaya alikuwa kiongozi katika kijiji kinaitwa Kwa Mkoro, Uzigua.
Kwani Abushiri hakujihusisha na biashara ya Utumwa?

Vipi wenyeji wengine wa Pangani walishiriki kwenye hiyo vita au ulikuwa uasi wa Abushiri pekee?

Kwanini Waarabu wa huko Pwani hawakumuunga mkono kwenye vita dhidi ya Wajerumani?.....
 
Kwa nini unataja Waarabu?

Abushiri aliungwa mkono na makabila mengi akawa na jeshi la askari 3000.

Wala haukuwa uasi.

Walikuwa wanapigana na adui Mjerumani aliyevamia nchi yao.
 
Alikua rafiki mkubwa wa Chief Mkwawa pia.
Hata ujio wa Ujerumani Abushiri ndiye aliyemtumia barua Mkwawa na kumtahadharisha kuhusu WaJerumani.
Mkwawa ndio akajenga ngome ya Liringa ambayo wajerumani walijaribu kuingia wakashindwa.
Mpaka pale waluguru walipomsaliti Mkwawa.
Waluguru?

Niangaze kwa mapana zaidi kwenye hili! Chifu Mkwawa utawala wake ulienea mpaka maeneo ya Morogoro Mkuu?
 
Waluguru?

Niangaze kwa mapana zaidi kwenye hili! Chifu Mkwawa utawala wake ulienea mpaka maeneo ya Morogoro Mkuu?
Hapana utawala wake ulikua Iringa tu kwenye himaya yake.

Ila alikua ana ugomvi na machifu wa uluguru wa Tosamaganga,Matombo,Mvuha.

Na hao ndio waliotoa siri za Chief Mkwawa kwa WaJerumani namna ya kuifikia ngome ya LIRINGA ya Chief Mkwawa,maana walikua wakitumia njia ya front hawakuweza kuikabili ngome ya Mkwawa.

Waluguru ndio wakaonesha maeneo ya miinuko kwa kupitia Matombo kutokea Tosamaganga kama mlango wa nyuma ndipo waJerumani wakafanikiwa kuivunja ngome ya LIRINGA na kumdhibiti Mkwawa.

Kama waluguru wasingeonesha hiyo back door ya Tosamaganga waJerumani wasingefanikiwa kumdhibiti Mkwawa mkuu.

Ukienda makumbusho ya Iringa pale ya Chief Mkwawa kuna barua ya Mkwawa aliiandika kwa herufi za kiarabu ila ni ya kiswahili kumuandikia Abushiri namna waluguru walivyomsaliti kwa kuwasaidia waJerumani.
 
Hapana utawala wake ulikua Iringa tu kwenye himaya yake.
Ila alikua ana ugomvi na machifu wa uluguru wa Tosamaganga,Matombo,Mvuha.
Na hao ndio waliotoa siri za Chief Mkwawa kwa WaJerumani namna ya kuifikia ngome ya LIRINGA ya Chief Mkwawa,maana walikua wakitumia njia ya front hawakuweza kuikabili ngome ya Mkwawa....
Doh! Subhanallah! Basi nimepitwa na mengi sana!

Na hii habari uliyonipatia imenisikitisha sana. Sijajua kwa namna gani nimeshikwa na majonzi kwa namna hii! Sijui huruma ndiyo imenizidi zaidi moyoni?

Ahsante sana Mkuu, nitafanya utaratibu wa kuzuru makumbusho ya Iringa ya Chifu Mkwawa.
 
Sisi waAfrika kutawaliwa na wakoloni tumejitakia wenyewe mkuu.

Kwa sababu ugomvi wa machifu wa makabila uliwawezesha wakoloni kufanya ile mbinu ya alliance & collaboration/divide and rule.

Mkoloni anatafuta kabila kinzani anaingia nalo ushirika halafu analitumia kabila hilohilo kuliteka kabila kinzani.

Katika ngome za makabila yote mJerumani alikiri kuwa ngome ya Chief Mkwawa ya Liringa ilikua ngome ngumu.

Maana waJerumani wamepoteza majenerali kama wawili wakubwa kama sijakosea kwa kuivamia ile ngome.
Kwa sababu licha ya kuwa na ukuta mkubwa imara ila pia Mkwawa alikua na silaha za moto (magobole) ambayo alipata kutoka kwa rafiki yake Abushiri.

Hilo lilileta ukinzani kwa WaJerumani.
Kusalitiana waAfrika/Tanzania tulianza mbali sana mkuu.
 
Hapana utawala wake ulikua Iringa tu kwenye himaya yake.
Ila alikua ana ugomvi na machifu wa uluguru wa Tosamaganga,Matombo,Mvuha.
Na hao ndio waliotoa siri za Chief Mkwawa kwa WaJerumani namna ya kuifikia ngome ya LIRINGA ya Chief Mkwawa,maana walikua wakitumia njia ya front hawakuweza kuikabili ngome ya Mkwawa.
Abushiri alikufa 1889, Ngome ya Mkwawa ilivunjwa mwaka 1894, huoni contradiction hapo? Au Abushiri aligeuka kuwa mzimu?
 
Abushiri alikufa 1889, Ngome ya Mkwawa ilivunjwa mwaka 1894, huoni contradiction hapo? Au Abushiri aligeuka kuwa mzimu?
Ilivunjwa ila haikujengwa mwaka 1894.

Mie nimezungumzia kuwa taarifa za Abushiri ndizo zilimtahadharisha Mkwawa kujenga hiyo ngome.

Haimaanishi kuwa waluguru walipomsaliti mkwawa basi ngome ikavunjwa hapohapo hapana.

Vita nyingi zilipiganwa mpaka kuivunja hiyo ngome mkuu kupitia hiyo njia.
 
Aliwezaje kuwasiliana na Chief Mkwawa? Kijiografia, Pangani na Iringa ni mbali sana. Kipindi kile hakukuwa na usafiri wa uhakika zaidi wa kumuwezesha Abushiri kutuma mtu au yeye mwenyewe kutoka Pangani kwenda Iringa kuonana na Chief ili kumpa taarifa za kiintelijesia juu ya uvamizi wa Wajerumani
 
Back
Top Bottom