Unajua mfuko mdogo uliopo ndani ya mfuko mkubwa kwenye jeans zako? Ule ambao kwa sababu ya udogo wake hauonekani kuwa na matumizi makubwa? Watu wengi wamekuwa wakijiuliza unatumika kwa nini hasa.
Mfuko huo mdogo uliopo ndani ya mfuko wa mbele wa kulia ulikuwa sehemu ya muundo wa awali kabisa.
Takriban miaka 150 iliyopita, tarehe 20 Mei 1873,
Levi Strauss & Co. walipata hati miliki ya “An Improvement in Fastening Pocket Openings,” Suruali hizo za awali, zilizoitwa
waist overalls, zilikuwa na sifa zilezile tunazoziona leo, zipu ya vifungo (button fly), rivets za shaba, kitambaa cha denim ya bluu, mshono wa Arcuate, na mifuko minne.
Mfuko huu uliundwa mahsusi ili wafanyakazi waweze kubeba saa zao za mfukoni kwa usalama.
Wakati huo, saa za mfukoni zilikuwa maarufu sana. Mara nyingi zilikuwa zikifungwa kiunoni kwa kutumia mnyororo, kisha kuwekwa ndani ya mfuko mdogo wa suruali. Hii ilisaidia kuzilinda zisipotee au kuharibika, na pia kuzifanya zipatikane kwa urahisi pale zilipohitajika.
Ingawa siku hizi saa za mfukoni hazitumiki sana, mfuko huu mdogo umeendelea kubaki kama sehemu ya muundo wa jadi wa jeans, ukihifadhi historia na utamaduni wake.