Historia ya Komandoo Tarimo

Historia ya Komandoo Tarimo

Mimi baba yangu tu ndo alikuwa komando. Nakumbuka tuko shambani tunalima, mara mbweha wawili wakatokea na kuanza kuvuruta kikapu cha msosi, kilikuwa mbali kidogo chini ya mti, ile anataka kwenda pale kuwatimua, likatokea li nguruwe pori sijui limekimbizwa na mkulima mwingine huko...mimi nikawa katikati sijui kinachoendelea, nimetaharuki tu....aisee yule nguruwe alirushiwa jembe moja hatari likakata uso, ile nageuka nione nani karusha...namuona dingi anamsulubu mbweha kwa jiwe moja hatari...ilikuwa ni shidaa!!
Hahaah mkuu mshua wako ni shujaa ila hamfikii baba yangu ni Legend zaidi
 
Mkuu unataka vita na JIWE wewe? Kuandika history ya watu wa ile kanda hakutompendeza
 
Nenda Rombo Mtaa wa Mamsera utamkuta shangazi yake Ruth L.Tarimo atakueleza
 
Wadau niko njiandaa kuandika historia ya komandoo wa kitanzania aliye kuwa akitwa Tarimo, kijana huyu alipata mafunzo yake kule Cuba, na baadae kurejea nyumbani Tanzania.

Je kuna mtu awaye yeyote mwenye ufahamu wa ili Jambo? naomba michango yenu zaidi.

Unamzungumzia kapteni Mohamed Tamim mzaliwa wa Tanga.

Tarimo alikuwa ni mmoja wa mawakili wa utetezi pamoja na mawakili Jadeja, Hussein Mucadam na Murtaza Lakha.

Mawakili wa serikali walikuwa wakiongozwa na wakili William Sekule na Johnson Mwanyika.

Kesi ilikuwa ikisikilizwa mahakama kuu barabara ya kivukoni (ya enzi hizo) chini ya jaji kiongozi Nasoro Mzavas.

Jaji Mzavas alitoa hukumu mwezi Decemba tarehe 28 mwaka 1985 ambapo washitakiwa wote walopatikana na hatia walifungwa maisha.

Jumla ya washtakiwa wote walikuwa ni 19 na baadhi yao ni Pius Lugangira au "Unlce Tom" au "Uncle checkbob", Khatibu Hassan Ghandi au Hatty Mac-Ghee, Kapteni Mohamed Tamimu ambae aliuawa wakati wa kukamatwa, Kapteni Damas Mbogoro, Kapteni Chris Kadege, Kapteni Badru Rwechungura Kajaja, Na Kapteni Vitalis Mapunda.

Wengine ni Kapteni Christopher Ngaiza, Kapteni Zacharia Hans Pope, Kapteni Rodrick Rosham Robert, Kapteni Suleiman Kamando na wengine wengi tu akiwemo huyo Eugene Maganga.

Bwana George Banyikwa na mkewe Zera Banyikwa ambao baadhi ya vikao vya kupanga uhaini vilikuwa vikifanyika nyumbani kwao Sinza, waliachiwa huru.

Halafu kuna mwasia mmoja maeneo ya Keko nae alijumuishwa kwenye kesi lakini baadae akaachiwa.

Iia Huyu Christopher Ngaiza alikuwa ni msaidizi wa raisi Nyerere akimsaidia kwenye ule mradi wa Bonde la Kagera.

Hivyo kwa kuweka kumbukumbu sawa ni kwamba unamzungumzia Kapteni Mohamed Tamim.
 
Mimi namkumbuka komando halisi TAMIM!! Wangapi mnamkumbuka huyu na alifanya nini? Hint: Unamkumbuka uncle Tom? Haya vijana somo la historia ya nchi yenu, waulizeni wazee wenu waliohai!!
hawa ndio wanajulikana Tamimu alitaka kupindua nchi
 
...Ndinani, umenikumbusha mbaaali sana, miaka ya 1983 au 1984 nikiwa shule ya msingi. Nilikua nafuatilia story za hawa jamaa waliokuja kujulikana sana baadae katika 'Kesi ya Uhaini'. Moja ya story ya Captain TAMIM ya kusisimua ni ile katika kukimbia asikamatwe na askari kanzu akaona lorry/gari ya wazi nyuma ikiwa imebeba crate kibao za bia akarukia na kudandia gari lile akaanza kuwavurumishia chupa za bia askari waliokuwa wanamfukuza ili wamkamate..., it is so sad kuwa ultimately akapigwa risasi na kuuwawa!

Two weeks ago nilienda Bukoba, pale airport nilikutana na mwenzao katika kesi ile, kama sijakosea anaitwa Captain Roberts. Wameshakuwa aged sasa hawa watu, unfortunately alikuwa kalewa sana. Angekua katika akili ya kawaida nilitamani kuongea nae nijue wakati huo walikusudia kuifanyia nini nchi zaidi ya kile tulichokuwa tunafanyiwa na viongozi wetu wakati ule...
Mzee baba primary tu umeshanza kufuatilia stori za makomandoo?
 
Kuna Challenges Za Mimi Kuzikubali Na Kujifunza Ila Siyo Kama Hizi Za Ki POPOMA Na Zilizotolewa Na POPOMA. Jitahidi Umrekebishe Nduguyo!
Ujuaji mwingi mbele kiza. Acha ujuaji dogo Gentamycine.

Huwezi jua kila kitu hapa duniani.

Ynyokooooo
 
Huna Uwezo Wa Kumfundisha Kagame Wewe Na Acha Kutaka Kupata KIKI Humu Kwa Kujifanya Wewe Ndiyo Mjeda Wa Uhakika TPDF..........au Wewe Ndiyo Yule Mr. Misifa Mwakibolwa? Halafu Ulivyo POPOMA Hata Tu Majina Yao Umekosea Kuyataja Na Huyajui Pia. Angalia Sasa Unavyoumbuka Humu Na Watu TUNAKUSANIFU Tu Na KUKUCHEKA! Kwa Kukusaidia Tu Rwanda Hatuna Mtu Aitwae Fred Rwigema Wala Patrick Karejea Bali Tuna Watu Waitwao Fredrick Rwigyema Na Patrick Karegeya. Siku Nyingine Ukija Humu Jamvini Ujikamilishe Vizuri Vinginevyo Utakuwa UNAJICHORESHA Tu Kwa Akina GENTAMYCINE.
Muulize unataka uyataje kwa uyakinifu kwani wewe unatokea kimironko......watusi wana matatizo saana achana nao
 
Wadau niko njiandaa kuandika historia ya komandoo wa kitanzania aliye kuwa akitwa Tarimo, kijana huyu alipata mafunzo yake kule Cuba, na baadae kurejea nyumbani Tanzania.

Je kuna mtu awaye yeyote mwenye ufahamu wa ili Jambo? naomba michango yenu zaidi.

Nini mchango wake kwa Taifa??
 
Kumbe wanyarwanda mmejaa humu mnaanza kubaguana na kuitana wanyamahanga, mnataka kuleta vita vyenu vya kijinga hapa kwetu wakati nyie ni maboya tu. Eti komando Kagame.. Komando my foot! Halaf mnajifanyaga ni watu wa hadhi ya juu kuliko watu wengine wakati nyie ni mandezi tu. Mbona hamkumwambia mjomba wenu Kagame arushe hata risasi moja mpakani tumfunze adabu? Mmmmmxxxiiuu...
Risasi.........mwanaume kikwete alifika mpakan akampa masaa 12 tena akamwambia hata hangaika barrack moja tuu ya ngara inamtosha......mbona PK alipakatwa na mkewe kule nyamirambo
 
Back
Top Bottom