Historia ya mababu wa kale wa Misri na elimu yao kuhusu uumbaji.. ""Mwanzo""

Historia ya mababu wa kale wa Misri na elimu yao kuhusu uumbaji.. ""Mwanzo""

Kabla ya kwenda mbele zaidi..napenda jua hizi habari/simulizi zilitangulia kuwepo kabla ya kuandikwa biblia na quaran ama zimekuja baada ya biblia/quaran.
Maake nachoona ni upande mmoja umecopy na kuedit then paste....hebu nijuze kipi kilianza wakuu.
zilikuwepo kabla ya hivyo vitabu vya dini
 
Mkuu kama siyo wazazi wa Atum kwanini Nu aliitwa ' "the Father of the Gods'?

kwenye bandiko pale kuna mahala alilituma jicho lake kutafuta wanae, huko google hilo jicho ndiyo wanaliita 'eye of RA' (as a messenger) kwa hiyo haya ndiyo yalikua matumizi ya RA?...

Ngoja niendelee kuwafatilia kwa umakini
Is
RA
El
 
Itoshe tu kusema imani za sasa ni maboresho ya imani za zamani sana kabla hata abraham bado ni kijana mdogo
 
Hizi ni ngano/hadithi za kale sawa sawa kabisa na zile za biblia....ila so far nshajua biblia na quaran hamna kitu pale i
Hivi sukari kwa sasa kilo moja inauzwa bei gani..!!?? Naona Neuroglycopenic features of hypoglycemia zinasumbua humu ndani
 
Mababu weusi wa kale huko misri walikuwa wanaamini kuwa Maisha na watu walikuwa na mwanzo, kivipi!!?

Elimu ya mababu hao inasema hapo mwanzo kulikuwa na maji yaliyokuwa yamejaa Dunia Nzima pamoja na Giza Zito,

Siku moja kikazuka kama kisiwa kidogo katika yale maji, na juu ya kisiwa hicho alisimama Atum/ Adam/ Temu/ Atom / Mungu/Mtu wa kwanza View attachment 354359

Atum alikohoa na kwenye hayo makohozi alitoka mwanaume aliyeitwa "SHU"
View attachment 354361

Atum alitema mate likiwa ni tendo lake la pili akamtema mwanamke "TEFNUT" View attachment 354362

Atum akapita kila kona ya Ulimwengu na kuumalizia katika uumbaji, maana yalikuwa ni maji tu yaliyokuwa yamezunguka kila kona ya Dunia. Wanyama na kila kitu juu ya uso wa nchi vikafwanya kwa miujiza yake.

Siku Moja Atum aliwapoteza Shu na Tefnut, kitu kilichofanya awatafute kila mahali bila mafanikio!,
Atum alituma Jicho lake la kulia lizunguke kila kona na kila mahali ulimwenguni kuwatafuta wanawe,

ccbe47eee73388e990e83e0d1c1b3363.jpg


Mwisho Jicho lake hilo liliweza kuona watoto zake, hivyo Atum alipata furaha kuu, alilia machozi ya furaha huku akielea huku na huko katika Ulimwengu.


36530083e5b0aa825322e271769a1644.jpg


Machozi yale yalipokuwa yakianguka chini na kugusa ulimwengu yalikuwa yakiumba watu katika rangi na hali tofauti.

Shu na Tefnut (hawa tunaweza kuwaita kama ndo uzao wa kwanza wa watawala wa kibinadamu) walizaa watoto wawili yaani GEB na NUT hao walipendana sana wao wakazaa watoto wanne, Seth, (Mungu wa maovu) Nephtys, Osiris (Mungu wa chini ya Dunia) na Isis (Malkia).

Baada ya watoto wale kuzaliwa shu alimrusha juu ya anga NUT ili aende juu angani akasimamie kila kitu juu ya anga la Dunia na GEB akalazwa chini katika Ardhi ili asimamie uso wote wa Dunia.

Osiris alimuoa Isis na kwa Muda huo Osiris akiwa ni mtawala wa Dunia yote, huku Seth akiwa kamuoa Nephtys miaka mingi ilienda lakini mambo hayakuwa shwari sana, Seth alikuwa na wivu mkuu kuwa kwanini Osiris kaka yake atawale Ulimwengu! Alikuza wivu wake siku hadi siku mpaka siku fulani alimfuata Osiris na kumuua na kumgawanya gawanya vipande, kisha kuvitupa huku na kule ili kufunga asiweze kuamshwa tena kama kipande chochote kitakosekana!

Hatimaye roho ya osiris ilishuka Chini ya Ulimwengu na ikaenda kutawala huko.

Huku Duniani hatimaye Seth akawa mfalme wa ulimwengu, huku mke wa Osiris akihangaika, na kulia kila siku, ila siku moja Isis alipata Mimba ya ajabu bila mwanaume, ikiwa ni roho ya osiris kuiweka mimba hiyo Tumboni mwa Isis,

Hatimaye Isis akaja kujifungua mtoto wa wa kuume aliyeitwa Horus/ Heru.
View attachment 354366

Horus alipokua mtu mzima akaja kusimuliwa jinsi babayake Osiris alivyouawa, na baba mgodo wake Seth, hivyo naye akapanga kisasi cha kuja kulipiza kisasi kwa Seth.

Hatimaje siku ya siku Seth na Horus walikutana na kilichofuata ilikuwa ni vita ya masaa kadhaa, Horus alipoteza jicho lake Moja ila mwisho wa siku alimuua Seth.

Na hatimaye Horus (mtoto) akawa mfalme wa Dunia na Osiris baba ake akiwa ni mfalme wa chini ya ulimwengu.
Oioojiiuoii[/8i]
 
Yap yap madini concious kuhusu black history hawa waleta dini wakaziedit na kulazamisha wote tuamini kama soga zao za kucopy na kupaste ndio ukweli. Mleta uzi nipe source nifuatilie vizuri habari za mababu weusi
 
Hahaaha story zake zipo tofauti, kuna baadhi ambao hudai kuwa alifanya hivyo na wengine hudai vile, Ukienda Misri pale Giza, kwenye kila kitu wanamakumbusho pale hudai nilichokidai, ila ukiingia online huku ndio patashika wazungu wanacreate mawazo yao kutupatia! Lol
Cha msingi kama una hela kabla hujafa tembelea Giza kisha nenda pale makumbusho ya Cairo si mbali toka pale Tahril square utapata historia nzuri sana halafu malizia na Old Orthodox church mahali alipofichwa mtoto Yesu
 
Cha msingi kama una hela kabla hujafa tembelea Giza kisha nenda pale makumbusho ya Cairo si mbali toka pale Tahril square utapata historia nzuri sana halafu malizia na Old Orthodox church mahali alipofichwa mtoto Yesu
[emoji15] Yesu ana mtoto?
 
Katika kabila lenu hakuna visaasili (legends) vinavyohusu uumbaji, chanzo cha binadamu, ulimwengu na vyote vilivyomo? Anza na hivyo kwanza kabla hujakimbilia kwa hawa Wamisri wa kale.
Mkuu vipi? Atum inaonekana alikuwa ndio binadamu toleo la kwanza na sio Adam na Eva.

Hivi chimbuko letu sisi ni tunatoka wapi hasa? Maanake naona wengine sijui ethiopia,gabon wengine sijui Soweto..

Alafu mbona ulinikimbia asee?
 
Mkuu vipi? Atum inaonekana alikuwa ndio binadamu toleo la kwanza na sio Adam na Eva.

Hivi chimbuko letu sisi ni tunatoka wapi hasa? Maanake naona wengine sijui ethiopia,gabon wengine sijui Soweto..

Alafu mbona ulinikimbia asee?
Asili imeanzia Ethiopia.
 
Naomba kuuliza hapo, wakati huyo jamaa anawatema viumbe hao na wengine wanatoka kwenye machozi nani alikuwa anafuatilia hasa kwa watu wa kwanza, habari hizi amehadithia yeye au nani?
mbavu zangu mie.kaka umemaliza hi myth
 
Back
Top Bottom