Historia ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda: Kilio Cha Mifereji ya Damu iendayo Ethiopia

Mkuu nafkiri hoja yangu hujaielewa mpaka sasa

Ni hivi china na ujerumani hawana shida ya ukabila hivyo hata akitawala mtu mmoja hamna shida ila Rwanda kenya uganda burundi na DRC kuna shida kubwa ya ukabila hivyo basi kabila moja kutawala nchi kwa miaka zaidi ya 20 haliwezi kukubalika na makabila mengine lazima vita izuke

Kagame hata akileta maendeleo vipi kama wahutu hawatopata haki sawa hayo maendeleo yatapukutika siku moja maana mauaji yatarudi tu unlike china na ujerumani hakuna ukabila maana makabila makubwa Ndio yanatawala
 
Haki sawa wanayokosa ni ipi kwa mfano? Au haki sawa ni kukalia kiti cha uraisi?
 
Haki sawa wanayokosa ni ipi kwa mfano? Au haki sawa ni kukalia kiti cha uraisi?
Usawa kwenye uchumi,jeshi na siasa hakuna kabisa. Watutsi ni wachache ila ndio wamekalia ofisi zote nyeti za serikali hata uchumi unashikiliwa na watutsi huku wahutu walio wengi wakiwa wanataabika hii lazima ilete mgawanyiko

Kagame aweke usawa hasa katika siasa na uchumi atamaliza kabisa ukabila ila akiendelea kutawala kwa mabavu huku wahutu wanapigika lazima genocide itarudi tuu

Jiulize wahutu wako 85% ila mgombea urais wa kitutsi Bwana kagame huwa anashinda kwa 90% ilihali watutsi wapo 14% pekee.....
 
Hapo kwenye uchumi wafanya biashara wakubwa ni Kabila lipi? Kwenye siasa pm ni Kabila gani? Mawaziri wangapi ni wahutu? Kwenye kura hoja yako hapo nini? Kwamba kura zinapigwa kikabila hivyo hastahili kupata 90%? Sasa hapo kati ya wewe na PK nani mkabila? Nadhani unastahili kuondoa bias kwenye michango yako kuwa huru mzee
 
Kwanza sipo biased ila naongea ukweli ndio maana nikasema akiweka usawa nchi itaenda sijasema akipinduliwa...

Kwanza Namba ya mawaziri haiwezi kuwa ndio usawa Naongelea serikali nzima hakuna 50:50 ya fursa za uongozi

Uchumi same case wanaomiliki sekta kubwa za uchumi ni watutsi yaani viwanda, malls,mabenki n.k huku wahutu wakiwa vibarua tu na akishaonekana tajiri anadhoofishwa (mifano ipo)

Kuhusu kura nachomaanisha haziakisi maoni ya wahutu ambao wengi wao wamechoshwa na kagame ila cha kushangaza unakuta anapata 90% za kura za wahutu ndio unabaki unashangaa

Kagame aweke usawa hapo atawale milele hakuna atakayelialia ila yeye anasema maendeleo kwanza ilihali wahutu wanapigika.... huko mbeleni ikitokea Tutsi genocide msijeanza kulialia
 
Toa copy za kutosha hasa ungeandika kitabu cha makomandoo uganda,mfereji wa damu hii simulizi ningetaka kila nakala niipate.Tunaomba ulindwe na Mungu uwe mzima.
 

sasa ulitaka ashinde kwa asilimia ndogo kwa sababu he is from monority, kama anashinda kwa asilimia kubwa it means anakubalika na watu wa jamii zote
 
sasa ulitaka ashinde kwa asilimia ndogo kwa sababu he is from monority, kama anashinda kwa asilimia kubwa it means anakubalika na watu wa jamii zote
Anakubalika?? Unajua sababu za General wake tegemezi katumba nyamwasa kukimbia uhamishoni ?? Unajua kwanini kamfunga victoire ingabire??

Kagame uchaguzi ukiwa huru na haki akipambanishwa na mhutu mwenye msimamo mkali kama victoire lazima aanguke maana aliposema tu waadhimishe pia genocide ya wahutu laki 7 waliouawa na RPF aliishia kuwekwa ndani huku wahutu wakimuona kma mkombozi wao hivyo akipatikana mgombea wa hivyo tena wahutu watapiga kura kwa hasira na kagame ataisahau ikulu

Wahutu hawamkubali kagame sababu serikali yake bado inawabagua ni vile tu hakuna upinzani wa kihutu sababu wote wanauawa wakionekana na nguvu na hayo aliyasema Nyamwasa mwenyewe kwamba chaguzi zote namba zinachezewa sasa nikuamini wewe au Mkuu wa majeshi ???
 
Hahahaha unachekesha ndugu, so hoja ya Victoria ngabire ni ipi ukiondoa huo uchochezi wa mauaji ya kimbali? Hoja za kitaifa alizonazo ni zipi? Za kujenga nchi? Unajua waasisi wa genocide walianza kama huyo wakaachwa ndo yakatokea ya 94 so ungekuwa wewe ndo raisi kisha mtu akahubiri sera za kugawa watu ungemchekea? Hoja ya kuchezewa namba ni nchi ipi ambayo wapinzani hawasemi hayo? Us wanasema namba zilichezewa trump akashinda na hata ushindi wa putin juzi watu wanamashaka nao. Vaa viatu vya PK kisha tuone nchi ikikushinda ikarudi ilikokuwa miaka 20 iliyopita kama historia haitakucheka. Hivi siasa za kugawa watu na kupanda chuki ziliwahi kufanikiwa kuleta mabadiliko chanya wapi katika hii dunia? Kugawa watu na kufufua chuki za kale zinazoanza kusahalika kuna faida gani ktk future ya Rwanda? Stop living in the past, wahutu wengi bado mnaishi miaka ya 1980's-1990's get a life to live, achana na past. Issues ya general iko wazi the man is a traitor. Hata hapa bongo wasaliti wapo, wanasaliti nchi yetu na hawafurahii nchi ikipiga hatua ndefu za maendeleo, wapo tayari kuikwamisha kwa mbinu zozote zile so hata wakati wa yesu wasaliti walikuwepo na wataendelea kuwepo ila Mungu ibariki Africa tutashinda tu
 
Katumba nyamwasa ni msaliti??? Kasaliti nini?? Ina maana wote kina patrick karegeya, kakere n.k wote ni wasaliti?? Okay tufanye ni wasaliti je kuna fact gani ambayo wamedanganya mbona zote kagame hajawahi kukanusha zaidi alisema atawashughulikia wote mmoja baada ya mwingine!!

Sikusema ingabire ndio awe rais nimesema wahutu hawamkubali kagame kwa sababu ya ubaguzi ila wanakosa figure wa kuwaongozea mapambano ndio nikasema akitokea agressive hutu kma ingabire au type ya odinga na besigye basi ndio mwisho wa kagame kutawala kwa sanduku la kura unless aibe kura kwa bunduki

Hakuna mtu ana live in the past kwani mie muhutu au mnyarwanda? Mie natoa maoni yangu kma mpenda haki na pan africanist..... Hakuna kitu kama past sababu matatizo yale yaliyopelekea genocide ya 1994 bado yapo sasa unasemaje watu wamove on ilihali changamoto za ukabila hamzimalizi??? Wekeni usawa hutoona kelele za wakosoaji wa kagame ila mnaposema eti tuache ukabila ilihali kagame kajaza watutsi watupu serikalini tutakuelewaje???

Usawa kwanza maendeleo baadae maana vita ikirudi hayo maendeleo yatapukutika kama biskuti
 


Unapoteza nguvu nyingi kubishana na mfuasi sugu wa mtu fulani. Kiongozi bora na mwenye mapenzi na nchi yake ni yule anaeandaa mfumo wa nchi kutawaliwa hata bila ya yeye kua madarakani. Marekani tunayoiona akina Washington wangeweza kutawala milele lakini hawakua wabinfasi badala yake waliwekeza kwenye mifumo ya nchi kutawaliwa vizuri hata wakiwa nje ya ikulu. Huyu unaebishana nae anaamini kua rwanda nzima hakuna raia yeyote mwenye sifa za kutawala zaidi ya huyu aliyepo madarakani. Kama PK angekua anaitakia mema rwanda angeandaa warithi akiwa bado ana nguvu za kushauri na sio huu upuuzi wa kubadilisha katiba kila kipindi chake kikiisha.
 
Nashkuru pia umerudi, maana ni kitambo sana sikuoni humu...I'm so happy mkuu the Habib 😀😀. Karibu sana na nnashkuru pia umenitag! Nakutakia jioni njema, mpe Hi dada yetu Nifah nimemmis sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…