Historia ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda: Kilio Cha Mifereji ya Damu iendayo Ethiopia

Historia ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda: Kilio Cha Mifereji ya Damu iendayo Ethiopia

Hata miaka 100 kama akiwa hai akae tu, viongoz aina ya Kagame wanatokeaga mara moja moja

Kwamba Gadafi alisahau maendelea ya kijamii? Libya ya wapi unazungumzia? Rwanda hakuna amani?

Mfano mzuri ni China, sababu ya kumfanya Xi Jinping atawale maisha yake yote unaijua? watu wa vile wanatokea mara moja moja, angalia yule mwanamama pale ujeruman
Mkuu nafkiri hoja yangu hujaielewa mpaka sasa

Ni hivi china na ujerumani hawana shida ya ukabila hivyo hata akitawala mtu mmoja hamna shida ila Rwanda kenya uganda burundi na DRC kuna shida kubwa ya ukabila hivyo basi kabila moja kutawala nchi kwa miaka zaidi ya 20 haliwezi kukubalika na makabila mengine lazima vita izuke

Kagame hata akileta maendeleo vipi kama wahutu hawatopata haki sawa hayo maendeleo yatapukutika siku moja maana mauaji yatarudi tu unlike china na ujerumani hakuna ukabila maana makabila makubwa Ndio yanatawala
 
Haki sawa wanayokosa ni ipi kwa mfano? Au haki sawa ni kukalia kiti cha uraisi?
 
Haki sawa wanayokosa ni ipi kwa mfano? Au haki sawa ni kukalia kiti cha uraisi?
Usawa kwenye uchumi,jeshi na siasa hakuna kabisa. Watutsi ni wachache ila ndio wamekalia ofisi zote nyeti za serikali hata uchumi unashikiliwa na watutsi huku wahutu walio wengi wakiwa wanataabika hii lazima ilete mgawanyiko

Kagame aweke usawa hasa katika siasa na uchumi atamaliza kabisa ukabila ila akiendelea kutawala kwa mabavu huku wahutu wanapigika lazima genocide itarudi tuu

Jiulize wahutu wako 85% ila mgombea urais wa kitutsi Bwana kagame huwa anashinda kwa 90% ilihali watutsi wapo 14% pekee.....
 
Hapo kwenye uchumi wafanya biashara wakubwa ni Kabila lipi? Kwenye siasa pm ni Kabila gani? Mawaziri wangapi ni wahutu? Kwenye kura hoja yako hapo nini? Kwamba kura zinapigwa kikabila hivyo hastahili kupata 90%? Sasa hapo kati ya wewe na PK nani mkabila? Nadhani unastahili kuondoa bias kwenye michango yako kuwa huru mzee
 
Kwanza sipo biased ila naongea ukweli ndio maana nikasema akiweka usawa nchi itaenda sijasema akipinduliwa...

Kwanza Namba ya mawaziri haiwezi kuwa ndio usawa Naongelea serikali nzima hakuna 50:50 ya fursa za uongozi

Uchumi same case wanaomiliki sekta kubwa za uchumi ni watutsi yaani viwanda, malls,mabenki n.k huku wahutu wakiwa vibarua tu na akishaonekana tajiri anadhoofishwa (mifano ipo)

Kuhusu kura nachomaanisha haziakisi maoni ya wahutu ambao wengi wao wamechoshwa na kagame ila cha kushangaza unakuta anapata 90% za kura za wahutu ndio unabaki unashangaa

Kagame aweke usawa hapo atawale milele hakuna atakayelialia ila yeye anasema maendeleo kwanza ilihali wahutu wanapigika.... huko mbeleni ikitokea Tutsi genocide msijeanza kulialia
 
KILIO CHA MIFEREJI YA DAMU IENDAYO ETHIOPIA

View attachment 718281

FINALE

Chiefs kutokana na ushauri wa watu wengi kuhusu nilichotaka niandike juu ya kudunguliwa kwa ndege ya Rais Habyarimana na hatimaye kifo chake mimeona nifuate ushuri huo na nisiandike maoni hayo kwa sasa.
Naomba nifanye hitimisho la makala hii na kama tutapata wasaa huko mbeleni basi tuta revisit makala hii na kujadili zaidi.

Sitaingia deep sana kwenye sehemu hii ya mwisho, naomba nifanye hitimisho tu…

Baada ya Jenerali Dallaire kupata uhakika kwamba ndege iliyodunguliwa ilikuwa imembeba Rais Juvenal Habyarimana alituma wanajeshi kumi wenye asili ya Kibelgiji kwenda nyumbani kwa Waziri Mkuu Agathe Uwilingiyimana ili kumpa ulinzi yeye na familia yake na pia kumpeleka mpaka kwenye kituo cha redio cha taifa cha Radio Rwanda ili apate kulihutubia taifa na kuwasihi raia wawe na utulivu.

Lakini kulikuwa na kikosi cha kijeshi cha weledi cha serikali ya Rwanda kinachoitwa 'Gendarmerie' (Presidential Guard) walikuwa tayari wameshaidhibiti Radio Rwanda na walianza kurusha matangazo na kuutangazia umma kwamba Rais Habyarimana ameuwawa na watusi (RPF) na hivyo wakati wa 'kuingia kazini' (kuuwa watusi) ulikuwa umewadia.

Askari wale wa Kibelgiji walidhibitiwa na makomando wa Presidential Guard na kunyang'anywa silaha. Kisha walimchukua Waziri Mkuu Uwilingiyimana mpaka nyumbani kwake ambako walimuua yeye pamoja na mumewe. Watoto wao walisalimika baada ya kujificha nyuma ya fenicha.
Kisha askari wale kumi wa Kibelgiji walipelekwa mpaka kwenye kambi ya jeshi la Rwanda ya Kigali ambako waliteswa na kisha kuuwawa kwa amri wa meja wa jeshi la Rwanda aliyeitwa Bernard Ntuyahanga.

Usiku wa siku hii ya tarehe 6 April mpaka siku ya tarehe 7 April 1994, wanajeshi wa Rwanda na wahutu wenye msimamo mkali walikuwa wanapita nyumba kwa nyumba mjini Kigali wakiwa na orodha mkononi wakiua wanasiasa wenye ushawishi pamoja na waandishi wa habari.

Ndani ya usiku huu wa kwanza mawaziri ambao wana msimamo wa kati waliuwawa na wale ambao walisalimika walienda kujificha.
Walifanya hivi ili kuondoa uwezekano wowote wa kuundwa serikali kwa dharura.

Katika kikao cha kamati ya dharura ambacho pia Dallaire aliitwa kushiriki, Kanali Bagorosa alimpendekeza Augustin Bizimungu kuwa Mnadhimu mpya wa jeshi (mnadhimu rasmi wa jeshi alikufa kwenye ndege pamoja na Rais Habyarimana) lakini Dallaire alifanikiwa kuweka msimamo wa kumkataa Bizimungu kutokana na msimamo wake mkali. Hivyo Marcel Gatsinzi ambaye ni muhutu mwenye msimamo wa kati akachaguliwa kuwa mnadhimu mpya wa jeshi.

Baada tu ya kuteuliwa, Gatsinzi alifanya juhudi kubwa kuzuia jeshi lisijihusishe na mauaji ya watusi. Kitendo hiki kiliwaudhi mno akina Bagorosa pamoja na viongozi wengine wa juu wa jeshi ambao walikuwa na msimamo mkali. Hii ilipelekea siku kumi baadae Gatsinzi kuuwawa na nafasi yake kuchukuliwa na Augustin Bizimungu ambaye alipendekezwa awali na Kanali Bagorosa.

Mauaji yalikuwa yanasambaa kwa kasi kubwa ya ajabu. Kingine ambacho kilisaidia zaidi ni tamaduni ya watu wa Rwanda kutii mamlaka.
Amri zilikuwa zinatolewa kutoka Kigali na kisha kufika kwa Magavana wa majimbo ambao nao walielekeza wananchi wao kutekeleza amri hizo kwamba wanapaswa kumuua kila mtusi wanayemuona mbele yao.

Vijana wa Interahamwe ambao niliwaeleza huko nyuma ambao walikuwa wameandaliwa siku nyingi kwa silaha za jadi (mapanga) pamoja na mafunzo walikuwa wanaongoza wananchi wengine kufanya mauaji kwa majirani zao na marafiki zao.
Kila mtusi aliuwawa na hata wahutu ambao walikiwa wanawaficha au kuwahirumia watusi nao waliuwawa.

Katika miji mengine mauaji yalikuwa yanafanyika kwa urahisi kabisa kutokana na majirani kujuana vyema makabila yao.
Ila kwenye sehemu kama Kigali ambako kuna mchanganyiko mkubwa wa watu mauaji yalikuwa yanafanyika kwa uangalifu. Ni hapa Kigali ambako kwenye barabara viliwekwa vizuizi lukuki vya wanajeshi na vijana wa Interahamwe.

View attachment 718282

View attachment 718283

View attachment 718286

Vizuizi hivi vilikiwa ni kwa ajili ya kukagua vitambulisho vya taifa. Vitambulisho hivyo vilikuwa vinaonyesha pia kabila la mtu. Wahutu walikuwa wanaachwa na watusi wakiuwawa mara moja.
Kama raia alikuwa hajabeba kitambulisho basi alihukumiwa kutokana na muonekano wake. Kwamba watusi ni wembamba, warefu, sura nyembamba na pua ndefu. Raia wenye muonekano huu walikuwa hawaulizwi mara mbili, shingo zao zilikuwa ni halali ya panga za vijana wa Interahamwe na jeshi la Rwanda.

Mauaji yalisambaa nchi nzima isipokuwa kwenye maeneo ambayo yalikuwa chini ya RPF kama vile majimbo ya Ruhengeri, Byumba, Kibungo na baadhi ya maeneo ya Kigali.

RPF walikiwa wanasonga mbele kwa ufanisi mkubwa wakiteka mji baada ya mji.

Wahutu kwenye miji ambayo RPF walikuwa wanaiweka kwenye himaya, walikuwa wanaikimbia miji hiyo kuhofia wanajeshi wa RPF kulipiza kisasi kwa kuwauwa. Ndipo hapa ambapo ndani ya siku chache sana za mwezi April karibia Wahutu 500,000 walivuka daraja maeneo ya Maporomoko ya Rusumo kuja Tanzania na kupokelewa kwenye kambi za wakimbizi za Umoja wa Mataifa.

Sehemu nyingine zote za nchi mauaji ya watusi yaliendelea na yalifanyika kimkakati kabisa.

Kanali Théoneste Bagorosa ambaye alijipachika uongozi wa kamati ya dharura, kupitia kamati hiyo wao ndio walikiwa kama wanaongoza nchi. Bagorosa ndiye ambaye alikuwa anatoa amri na kuhutubia kwenye radio kusisitiza mauaji ya 'mende' kwenye nyumba yao. Bagorosa pia alifanya vikao na viongozi wa juu wa vikundi cha Interahamwe na Impuzamugambi na kuwapa maelekezo ya namna ya kuongoza wananchi kufanya mauaji hayo.

Vinara wengine wa mauaji haya alikuwa ni waziri wa Ulinzi Augustin Bizimana, kamanda wa Paratroopers Aloys Ntabakuze, na kiongozi wa Presidential Guard Protais Mpiranya.
Lakini pia kulikuwa na mfanyabiashara maarufu mjini Kigali aliyeitwa Felician Kabuga ambaye alikuwa anawasaidia rasilimali fedha Interahamwe ili waendelee na morali ya mauaji.

Siku ya tarehe 8 April, mauaji yakiwa yanaendelea kwa kasi, kanali Bagorosa akaitisha tena kamati ya dharura na kupendekeza serikali ya mpito.
Theodore Sindikubwabo aliteuliwa kiwa Rais wa muda huku Jean Kambanda akiteuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa muda.
Baraza la mawaziri lote liliundwa na wanachama wa 'power wings' wa vyma vya siasa vya MRND na CDR.
Serikali hii ya muda iliapishwa siku ya tarehe 9 April 1994 na mara moja makao makuu ya serikali yalihamishwa kutoka Kigali kwenda Gitamara ili kuepuka mapigano ambayo yalikuwa yanategemewa kati ya RPF na vikosi vya serikali.

Kamati ya dharura ilivunjwa… lakini Bagorosa ndiye alikuwa kwa uhalisia anaiendesha nchi. Yeye ndiye alikuwa na maamuzi ya mwisho ya katika kila jambo. Serikali iliyotangazwa ilikuwa ni kama geresha tu ili kuhalalisha kile ambacho kilikuwa kinaendelea.

Mauaji yaliendelea, amri ilitolewa kwamba asiachwe hata mtusi mmoja akiwa hai. Hata mtoto mchanga.

Kuna matukio mengi sana ya kusikitisha ambayo yalitokea lakini sitaingia ndani sana kwenye sehemu hii kama ambavyo nimesema awali.

Lakini hatuwezi kusahau tukio la mauaji kanisani eneo la Nyarubuye.
Siku ya April 12, watusi wapatao 1,500 walikuwa wamejificha ndani ya kanisa katoliki la eneo hili.
Kasisi wa kanisa hili, Padre Athanase Seromba aliwatonya Interahamwe juu ya uwepo watusi kanisano kwake. Interahamwe walitumia bulldozer kulisambaratisha kanisa lote na waliomo ndani. Wale ambao walikuwa wanajaribu kukimbia walikatwa mapanga mpaka kifo.

Tukio lingine ambalo hatuwezi kulisahau ni maelfu ya watusi ambao walikuwa wamejificha kwenye majengo ya shule ya ufundi ya Kigali (École Technique Officielle) mahala ambako wanajeshi wa Ubelgiji sehemu ya UNAMIR walikuwa wameweka kambi. Baadae Ubelgiji iliondoa wanajeshi wake wote nchini Rwanda baada ya wale kumi waliotumwa kumlinda waziri mkui Uwilingiyimana kuuwawa na Presodential Guard.
Baada ya wanajeshi wa Ubelgiji kuondoka eneo hili, vijana wa Interahamwe walivamia na kuua watusi elfu kadhaa ambao walikuwa wamejificha hapa.

View attachment 718287

View attachment 718288

Japokuwa mauaji haya katika historia inakumbuka zaidi watusi na wahutu wachache kwamba ndio waliuwawa. Lakini mara nyingi tunasahau zaidi ya watu wa kabila la Watwa 30,000 ambao nao pia waliuwawa. Watu wa kabila la Twa walikuwa nao wanahesabika kama wasaliti. Wahutu wenye msimamo mkali waliwashutumu kwamba walikuwa wanawasaidia RPF kuingia kwenye miji.

Sasa basi;

Nilieleza kwamba Kagame alikuwa amefanikiwa kuingiza makomando 1,000 ndani ya Kigali ambao walikuwa wanalinda wanadiplomasia wa RPF katika Bunge.
Mauaji ya kimbari yalipoanza tu, vikosi vya serikali vilishambulia jengo la Bunge kwa lengo la kuua makoamndo wa RPF ambao walikuwa pale. Lakini makomando hawa wa RPF walifanikiwa kwa ufasaha kabisa kudbibiti vikosi vya serikali na kuwarudisha nyuma nje kidogo ya Kigali.

Kagame aliongoza RPF kupambana kutokea Kaskazini mwa nchi wakiwa wamejigawanya kwenye makundi matatu na huku wakitafuta namna ya 'kulink' na makomando ambao walikuwa ndani ya Kigali.

Ndani ya siku chache RPF walipambana kuelekea kusini wakiiweka kwenye himaya mji wa Gabiro na sehemu kubwa inayozunguka kigali upande wa mashariki na Kaskazini.
Hawakutaka kuivamia Kigali mara moja au Byumba, bali walipigana katika mtindo ambao walikuwa wanauzunguka mji wote wa Kigali kwa nje.

Mwishoni mwa mwezi April, RPF walikuwa wameweka eneo lote la mpaka wa Rwanda na Tanzania kwenye himaya yao. Kutokea hapa walisonga mbele kuelekea magharibi ya mji wa Kibungo na hatimaye kusini mwa Kigali.

Mpaka kufikia May 16 walikuwa wamekata mawasiliano ya barabara kati ya mji wa Kigali na Gitamara ambao ndipo ilikuwepo serikali ya mpito.
Mpaka kufikia June 13, RPF walikuwa wameuweka mji wa Gitamara kwenye himaya yao na kuilazimu serikali ya mpito kukimbia na kwenda kuweka makazi kwenye mji wa Gisenyi.

Mpaka hatua hii RPF walikiwa wamefanikiwa kuizunguka Kigali kila pande na pia ndani ya mji kulikuwa na makomando wao.

Tusisahau kwamba vikosi vya serikali walikuwa na silaha nzito zaidi askari wengi zaidi.
Kilichokuwa kinawasaidia RPF ni mbinu adhimu za kivita za Kagame.
Ni hapa ambapo Jenerali Dallaiire alimuita Kagame "master of psychological warfare".

Kagame alikuwa anachukua advantage ya kwamba… kwanza vikosi vya serikali walikuwa wameelekeza nguvu zao zaidi na akili zao katika mauji ya kimbari badala ya kuweka kipaumbele cha kupambana na RPF. Lakini mafanikio ya RPF kuchukua mji baada ya mji pia yalikuwa yamefanya vikosi vya serikali kuishiwa morali na Kagame alifanya hivi makusudi ndio maana akaiweka Kigali kuwa ya mwisho kuiteka.

Kwa hiyo sasa alikuwa anafanya mashambulizi ya ufanisi ya kushtukiza kwa masaa kadhaa pale Kigali na kisha ana-retreat. Wanasubiri masaa mengine kadhaa wanashambulia tena kisha wana-retreat. Tena na tena na tena. Alichokuwa anafanya ni kama kuwachekecha vikosi vya serikali na kuwachosha. Hii ilifanikiwa, kwani tarehe 4 July, RPF walifanya shambulio kubwa na kufanikiwa kuwashinda kwa urahisi kabisa vikosi vya serikali na kuiweka Kigali kwenye himaya yao.
Ilipofika tarehe 18 July walichukua mji wa Gisenyi na eneo lote la kaskazini magharibi ya Rwanda na kuifanya ile serikali ya mpito kukimbilia Zaire.

Mpaka hapa maana yake ni kwamba Rwanda yote sasa ilikuwa chini ya himaya ya RPF isipokuwa eneo dogo la kusini magharibi ambalo lilikuwa chini ya jeshi la Ufaransa walioingia Rwanda chini ya Oparesheni maalumu ya Umoja wa Mataifa.

Kwa hiyo, mpaka hapa ni rasmi kwamba RPF walikuwa wamezima mauaji ya Kimbari. Tarehe rasmi ya mauaji ya kimbari kukoma ni tarehe 15 July 1994 japokuwa Rwanda wenyewe wanaadhimisha siku hii kila mwaka tarehe 4 July kama siku ya Ukombozi wa Taifa na ni siku ya mapumziko.

Umoja wa mataifa unatoa takwimu kwamba watu 800,000 waliuwawa kwenye mauji yale huku serikali ya Rwanda yenyewe ikisisitiza kuwa ni watu 1,071,000. Inakisiwa kwamba Wahutu walikuwa ni 10% ya watu hawa waliouwawa.

Mauaji haya ni moja ya mauaji mabaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya dunia yetu hii.
Ni mauaji ambayo yanapaswa kutufunza mambo mengi sana. Kwamba ubaguzi, unyonyaji, ukandamizaji na kujikweza huzaa chuki kwa wale wanaoteswa. Chuki hii inaweza kufurukuta rohoni mwa watu hawa kwa miongo kadhaa lakini siku itakapopata ufa wa kujipenyeza, moto wake unaweza usizimike pasipo kuitafuna dunia.

Kuna vitu vingi vingi sana sana najua sijavigusia kwenye hitimisho langu hili. Naomba kwa makala hii tuishie hapa… huko mbeleni tukipata wasaa tunaweza kuirejea na kugusia yale ambayo nimeyaacha katika mfululizo huu.

Dunia yetu itakuwa mahala salama na pazuri pa kuishi endapo wote kwa pamoja tutajifunza kwamba hakuna aliye mbora kuliko mwingine. Tukijifunza kuheshimu utu, kujiheshimu na kuheshimiana. Tukiwa mawakili wa haki na umoja. Na sote tukikumbuka kwamba sisi ni wana wa baba mmoja.

Kwa makala hii naomba niishie hapa ili kupisha makala nyingine kuanza.

View attachment 718290
Paul Kagame akiwana bunti yake

View attachment 718291
Kigali leo hii

Muhimu: Ushauri ambao mmekuwa mkinipa kwa muda mrefu hatimaye nimeufanyia kazi. Ndani ya wiki mbili zijazo nitatoa kitabu changu cha kwanza kabisa cha simulizi ya Vipepeo Weusi. Kama ambavyo mmekuwa mkiniunga mkono kwenye nyuzi hizi kwa miaka mitatu sasa naomba pia sapoti yenu katika hatua hii mpya ambayo naichukua. Kwa pamoja tupambane kurejesha utamaduni wa watu kujisomea na tuinue kizazi kipya chenye maarifa.

Naomba baraka zenu ili project hii iwe na mafanikio na hatimaye nitoe vitabu vingi zaidi na zaidi.

Asanteni sana.

Habibu B. Anga 'The bold' - 0718 096 811
Toa copy za kutosha hasa ungeandika kitabu cha makomandoo uganda,mfereji wa damu hii simulizi ningetaka kila nakala niipate.Tunaomba ulindwe na Mungu uwe mzima.
 
Usawa kwenye uchumi,jeshi na siasa hakuna kabisa. Watutsi ni wachache ila ndio wamekalia ofisi zote nyeti za serikali hata uchumi unashikiliwa na watutsi huku wahutu walio wengi wakiwa wanataabika hii lazima ilete mgawanyiko

Kagame aweke usawa hasa katika siasa na uchumi atamaliza kabisa ukabila ila akiendelea kutawala kwa mabavu huku wahutu wanapigika lazima genocide itarudi tuu

Jiulize wahutu wako 85% ila mgombea urais wa kitutsi Bwana kagame huwa anashinda kwa 90% ilihali watutsi wapo 14% pekee.....

sasa ulitaka ashinde kwa asilimia ndogo kwa sababu he is from monority, kama anashinda kwa asilimia kubwa it means anakubalika na watu wa jamii zote
 
sasa ulitaka ashinde kwa asilimia ndogo kwa sababu he is from monority, kama anashinda kwa asilimia kubwa it means anakubalika na watu wa jamii zote
Anakubalika?? Unajua sababu za General wake tegemezi katumba nyamwasa kukimbia uhamishoni ?? Unajua kwanini kamfunga victoire ingabire??

Kagame uchaguzi ukiwa huru na haki akipambanishwa na mhutu mwenye msimamo mkali kama victoire lazima aanguke maana aliposema tu waadhimishe pia genocide ya wahutu laki 7 waliouawa na RPF aliishia kuwekwa ndani huku wahutu wakimuona kma mkombozi wao hivyo akipatikana mgombea wa hivyo tena wahutu watapiga kura kwa hasira na kagame ataisahau ikulu

Wahutu hawamkubali kagame sababu serikali yake bado inawabagua ni vile tu hakuna upinzani wa kihutu sababu wote wanauawa wakionekana na nguvu na hayo aliyasema Nyamwasa mwenyewe kwamba chaguzi zote namba zinachezewa sasa nikuamini wewe au Mkuu wa majeshi ???
 
Hahahaha unachekesha ndugu, so hoja ya Victoria ngabire ni ipi ukiondoa huo uchochezi wa mauaji ya kimbali? Hoja za kitaifa alizonazo ni zipi? Za kujenga nchi? Unajua waasisi wa genocide walianza kama huyo wakaachwa ndo yakatokea ya 94 so ungekuwa wewe ndo raisi kisha mtu akahubiri sera za kugawa watu ungemchekea? Hoja ya kuchezewa namba ni nchi ipi ambayo wapinzani hawasemi hayo? Us wanasema namba zilichezewa trump akashinda na hata ushindi wa putin juzi watu wanamashaka nao. Vaa viatu vya PK kisha tuone nchi ikikushinda ikarudi ilikokuwa miaka 20 iliyopita kama historia haitakucheka. Hivi siasa za kugawa watu na kupanda chuki ziliwahi kufanikiwa kuleta mabadiliko chanya wapi katika hii dunia? Kugawa watu na kufufua chuki za kale zinazoanza kusahalika kuna faida gani ktk future ya Rwanda? Stop living in the past, wahutu wengi bado mnaishi miaka ya 1980's-1990's get a life to live, achana na past. Issues ya general iko wazi the man is a traitor. Hata hapa bongo wasaliti wapo, wanasaliti nchi yetu na hawafurahii nchi ikipiga hatua ndefu za maendeleo, wapo tayari kuikwamisha kwa mbinu zozote zile so hata wakati wa yesu wasaliti walikuwepo na wataendelea kuwepo ila Mungu ibariki Africa tutashinda tu
 
Katumba nyamwasa ni msaliti??? Kasaliti nini?? Ina maana wote kina patrick karegeya, kakere n.k wote ni wasaliti?? Okay tufanye ni wasaliti je kuna fact gani ambayo wamedanganya mbona zote kagame hajawahi kukanusha zaidi alisema atawashughulikia wote mmoja baada ya mwingine!!

Sikusema ingabire ndio awe rais nimesema wahutu hawamkubali kagame kwa sababu ya ubaguzi ila wanakosa figure wa kuwaongozea mapambano ndio nikasema akitokea agressive hutu kma ingabire au type ya odinga na besigye basi ndio mwisho wa kagame kutawala kwa sanduku la kura unless aibe kura kwa bunduki

Hakuna mtu ana live in the past kwani mie muhutu au mnyarwanda? Mie natoa maoni yangu kma mpenda haki na pan africanist..... Hakuna kitu kama past sababu matatizo yale yaliyopelekea genocide ya 1994 bado yapo sasa unasemaje watu wamove on ilihali changamoto za ukabila hamzimalizi??? Wekeni usawa hutoona kelele za wakosoaji wa kagame ila mnaposema eti tuache ukabila ilihali kagame kajaza watutsi watupu serikalini tutakuelewaje???

Usawa kwanza maendeleo baadae maana vita ikirudi hayo maendeleo yatapukutika kama biskuti
 
Unapoteza nguvu nyingi kubishana na mfuasi sugu wa mtu fulani. Kiongozi bora na mwenye mapenzi na nchi yake ni yule anaeandaa mfumo wa nchi kutawaliwa hata bila ya yeye kua madarakani. Marekani tunayoiona akina Washington wangeweza kutawala milele lakini hawakua wabinfasi badala yake waliwekeza kwenye mifumo ya nchi kutawaliwa vizuri hata wakiwa nje ya ikulu. Huyu unaebishana nae anaamini kua rwanda nzima hakuna raia yeyote mwenye sifa za kutawala zaidi ya huyu aliyepo madarakani. Kama PK angekua anaitakia mema rwanda angeandaa warithi akiwa bado ana nguvu za kushauri na sio huu upuuzi wa kubadilisha katiba kila kipindi chake kikiisha.
 
Nashkuru pia umerudi, maana ni kitambo sana sikuoni humu...I'm so happy mkuu the Habib 😀😀. Karibu sana na nnashkuru pia umenitag! Nakutakia jioni njema, mpe Hi dada yetu Nifah nimemmis sana
 
Back
Top Bottom