Historia ya mkoa wa Tanga

Naomba kujua uhusiano kati ya n'tanga, tanga na mpka ikawa tanganyika. Nasema hivi sababu tanga kuna eneo linaitwa tanganyika...
 
Naomba kujua uhusiano kati ya n'tanga, tanga na mpka ikawa tanganyika. Nasema hivi sababu tanga kuna eneo linaitwa tanganyika...
Hata Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro kuna Kijiji kinaitwa Tanganyika.
 


Mkoa wenye waislamu wengi usitegemee hawa ndugu zetu wauzungumzie vizuri. Hiyo istiqama tu inawatoa jasho
 


Na mkoa wowote walipopita waarabu/waislamu watu wake wanabusara na hekma ya hali ya juu + maendeleo.
 
Nyendo,
ungewaeleza wasomaji kwamba kabla ya mkoa wa Tanga, wakati wa utawala wa Waingereza, kulikuwa na jimbo la Tanga. Na wakati huo eneo ambalo sasa hivi ni wilaya za Same na Mwanga lilikuwa sehemu ya jimbo la Tanga[ tanga province]. pia mkoa wa Tanga ulitoa wasomi wengi wa mwanzo ktk Tanganyika kutokana na uwepo wa shule kongwe za mishen za Kideleko na Magila.
 
Naomba kujua uhusiano kati ya n'tanga, tanga na mpka ikawa tanganyika. Nasema hivi sababu tanga kuna eneo linaitwa tanganyika...
Km ulvoambiwa ntanga kibondei ni shamba, afu nyika kwa kisambaaa na kibondei ni porini, au mbali na nyumbani kwaio tanganyika ni shamba la mbali na nyumbani
 
Happy kwenye vita. Ukienda pale Maere upande wa magharibi kuna muinuko miubwa kidogo utakuta kuna mabaki ya nyumba kubwa sana ,inasemekana ikipigwa na mabomu kutokea kwenye Meli. Ilikuwa NI kambi ya wajerumani ,ilipigwa na waingereza. Lakini sidhani kama utaruhusiwa kufika huko maana kwa Sasa Kuna kambi jeshi karibu na maeneo hayo.
Umenikumbusha sana
 
Nzuri ila umesummarize sana maana haujagusia watawala kama ABUSHIRI BIN SULTAN, KIMWERI NYUMBAE, SIMBA MWENE MBEGA.

Abushiri alikuwa zaidi upande wa Bagamoyo na alipigana na Mjerumani kumzuia asitawale.

Alinyongwa na Wajerumani.
 
Hakuna kabila la wasegeju huko Tanga?
Nilisoma zamani shule ya Msingi kwamba Wasegeju ni moja ya makabila mkoani humo,
Wapo mpakani wa Kenya na Tanzania, wilayani Mkinga (njia ya kuelekea Mombasa).
 
Tofaufisha wilaya na halmashauri. Korogwe kuna halmashauri mbili ktk wilaya moja. Handeni kuna majimbo mawili wilaya moja.
Uko sahihi mkuu. Lushoto pia ina majimbo matatu ya uchaguzi (Mlalo, Lushoto na Bumbuli) na halmashauri mbili (Lushoto na Bumbuli). Haya mambo yanachanganya sana, hasa kutofautisha wilaya na hamlashauri. 😀 😀 😀 🔥
 
Mbona nasikia kwamba huko Tanga kabila kuu ni wazigua ? Na wewe wasema ni wasambaa ! Ebu fafanua zaidi ndugu yangu
Wazigua wapo Handeni na Kilindi. Sio wengi kama Wasambara (waite Wasambaa). Wasambaa wapo Lushoto, Korogwe na Muheza lkn pia ndio walio wengi Tanga mjini, wakichukua nafasi ya wenyeji Wadigo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…