Hivi Gen Z mnajua kweli historia ya huu mnara? Kitu kilichonipa ushawishi wa kutaka kukua zaidi ni hili neno 'Bismini'. Maana yake ni nini? Na chimbuko lake ni nini? Nimejaribu kutafuta lakini hakuna walikoeleza maana ya Bismini
====
Hekaya fupi ya Mnara wa Askari Jijini Dar es Salaam
Mnara wa Askari ulioko katikati ya jiji la Dar es Salaam ni mojawapo ya alama kuu za kihistoria nchini Tanzania.
Ulisimikwa mwaka 1927 na serikali ya kikoloni ya Waingereza kwa heshima ya askari wa Kiafrika waliopigana katika Vita ya Kwanza ya Dunia wakiwa sehemu ya Kikosi cha King’s African Rifles pamoja na waliokuwa wabeba mizigo (Carrier Corps).
Sanamu hiyo ya shaba ilichongwa na msanii wa Kiingereza James Alexander Stevenson, na ilionyeshwa kwanza katika maonyesho ya Royal Academy nchini Uingereza kabla ya kuletwa Tanganyika.
Mnara huu ulichukua nafasi ya sanamu ya utawala wa Kijerumani iliyokuwa ikimwonyesha gavana Hermann von Wissmann akiwa na askari mweusi miguuni mwake, sanamu ambayo iling’olewa na Waingereza walipotwaa mji wa Dar es Salaam mwaka 1916.
Askari aliyeonyeshwa katika sanamu ya sasa anaonekana akiwa katika mkao wa kivita, bunduki mkononi na uso wake ukielekea baharini, ishara ya ujasiri na mchango wa Waafrika katika vita hiyo kubwa.
Maandishi ya kumbukumbu katika Kiswahili, Kiingereza na Kiarabu yameandikwa kwenye msingi wa mnara huu, ukiwemo msemo maarufu wa kusema “Ukipigania nchi yako, hata ukifa, jina lako litakumbukwa na wanao.”