Historia ya Mtaa wa Aggrey uliopo Jijini Dar es Salaam

Historia ya Mtaa wa Aggrey uliopo Jijini Dar es Salaam

Tupe historia ya ununio .. Nasikia huo mtaa zaman walikua wananuiana kinoma yaani ukichukia tuu nenda ununio unakutana na wanunaji wenzako hahah aisee historia ya tabata ntaleta siku nyingine Leo na usingiz
 
Hata ku copy Na ku paste ni akili pia, punguza chuki, dharau, kashfa Na kebehi, havikusaidii chochote wala havikunufaishi Na chochote. Jifunze upendo hata kama hujawahi kupendwa
Sasa toka lini historia ya mtu iwe sio ya kucopy na kupaste,hivi unaweza kuandika historia ya Chief Mkwawa au Kinjekitile yako pekee ya kutunga kichwani tofauti na wengine.Mimi namshukuru BujuBuji sidhani hata kama wengi wetu tulijua asili ya jina la mtaa wa Aggrey.Ila Watanzania tumekuwa watu wa kuponda kila kitu,na kujifanya maarifa yako au utashi wako ndio unajua kila kitu.Hata Biblia au Quran nayo ni copy and paste na tunaenzi.
 
_Mtaa wa Aggrey, mtaa wa Aggrey haya sasa soma historia yake...._

*UBAGUZI WA RANGI ULIVYOMKUMBA DR. AGGREY UKIWEMO WA NEW AFRICA HOTEL ENZI ZA UKOLONI*


DR. JAMES EMMANUEL KWEGYIL AGGREY ni jina ambalo takriban 98% ya Watanzania hawalijui wala hawajawahi kulisikia.

DR. AGGREY, mghana aliyetokea Achimota Ghana, ingawa kwa sasa ni marehemu, ni mwafrika ambaye bado anayeheshimika sana ulimwenguni licha ya kufariki miaka karibu 100 iliyopita.

DR. AGGREY ameacha historia kubwa barani Afrika ikiwemo Tanzania. Katika maisha yake alikumbana na kila aina ya ubaguzi toka kwa wazungu.

Hapa Tanzania pia, ubaguzi wa rangi haukumuacha salama kwani alikumbana nao katika hoteli maarufu ya NEW AFRICA HOTEL.

Hoteli hiyo ya NEW AFRICA HOTEL iliyopo maeneo ya posta jijini Dar Es Salaam, ilijengwa na Wajerumani baada ya kukabidhiwa Tanganyika kufuatia Berlin Conference 1884-85.

Enzi za ukoloni wa Mjerumani na Mwingereza, ilikuwa ni marufuku kwa Mwafrika kukanyaga hotelini hapo labda tu kwa kibali maalum au kama ni mfanyakazi wa hoteli hiyo.

DR. AGGREY alikuja Tanganyika mwaka 1924 kama Mjumbe wa *Phelps-Stokes Fund Commission* kuja kuangalia jinsi ya kuwaendeleza Waafrika kielimu. Dr. AGGREY alikuwa Mwafrika pekee kwenye Commission hiyo. Commission iliundwa kutokana na *Ms. Carolyne Phelps Stokes*, ambaye alifariki mwaka 1909 na kuacha kitita cha fedha,($ 1,000,000) na usia uliosema- *"I bequeath the same to My trustees to be used for the education of Negros, both in Africa and the United States, North American Indian and needy and deserving white students"*.

Ni kutokana na wosia huu ndipo ilipoundwa Commission hiyo ambayo ilizuru mataifa kumi ya Afrika. Commission hiyo ilizuru Tanganyika na Zanzibar toka Machi 1924 hadi April 1924.


Baada ya Commission hiyo kuwasili jijini Dar Es Salaam, wajumbe waliamua kufikia NEW AFRICA HOTEL, moja ya hotel chache kubwa na ya kuheshimika nchini wakati huo.

Katika hali ya kusikitisha, DR. AGGREY, akiwa Mwafrika pekee katika Commission hiyo, alikataliwa kupewa chumba katika hotel hiyo ya kutokana na Uafrika wake!.

Hili jambo lilimuhuzunisha sana lakini hakukata tamaa na akaendelea na harakati zake za kuwasaidia waafrika wenzake kwa kadri alivyoweza. Baada ya kukataliwa chumba, ilimbidi DR. AGGREY akajitaftie chumba kwenye hoteli nyingine.

DR. AGGREY, akiwa Dar Es Salaam, ndiye aliyemshauri KLEIST SYKES kuunda chama kwa maana ndiyo inhekuwa rahisi kupigania haki zao kwa pamoja. KLEIST alikuwa kijana msomi mwenye kuzungumza Kijerumani na Kiingereza fasaha. Ilimchukua SYKES miaka mitano kuunda chama kiitwacho AFRICAN ASSOCIATION (AA) hapo mwaka 1929 kwa minajiri ya kuwapigania Waafrika. African Association baadae ilibadilishwa na kuwa TANGANYIKA AFRICAN ASSOCIATION(TAA) mwaka 1948. AA ndiyo iliyokuwa chimbuko la TANU iliyoanzishwa tarehe 7.7.1954.

Kutokana na wazo hilo muhimu kwa historia ya nchini yetu, WAHENGA watakumbuka kuwa iliamuliwa DR. AGGREY apewe mtaa jijini Dar Es Salaam kama kumbukumbu. Ndipo mtaa huo uliopo maeneo ya Kitumbini kuelekea Kariakoo, jijini Dar Es Salaam ukapewa jina la *MTAA WA AGGREY*.

DR. AGGREY alikuwa ni mwalimu mwenye utaalamu wa hali ya juu aliyetambuliwa na kuheshimika duniani kote.

Mwaka 1895 akiwa Mwalimu wa shule ya Wesleyan Memorial School, alifanya mtihani, pamoja na waalimu wengine 119 nchi nzima ya Ghana, uliotungwa Uingereza. DR. AGGREY aliibuka Mwanafunzi Bora na ndiye pekee aliyepata *Second Class* na kutunukiwa cheti maalum.

Cheti hicho alichotunukiwa na Malkia wa Uingereza kiliandikwa-: *"This Certificate of Distinction qualifies you, without further examination, to teach in any similar school in any British colony, the world over"*. Dr. AGGREY alikuwa Mwafrika wa kwanza kutunukiwa Tuzo hiyo.

Commission hiyo, baada ya kutoka Tanganyika ilikwenda Belgian Congo. Huko, baada ya shughuli ya siku nzima za siku ya kwanza, Gavana (mzungu) akaialika Commission kwaajili ya Dinner, Ikulu. Gavana alipomuona DR. AGGREY akiwa na wajumbe wengine ambao walikuwa ni wazungu aliamuru asiingie ndani hivyo akabaki mlangoni akiliwa mbu na kupigwa baridi hadi wenzake walipomaliza dinner!

Figisu hizi hazilumkatisha tamaa Dr. AGGREY na badala yake zilimpa nguvu zaidi kwani alielewa kuwa jukumu lake ni kuwasaidia Waafrika kielimu. Baada ya hapo Commission ilikwenda Angola ambako masaibu ya ubaguzi wa rangi yaliendelea dhidi yake ambapo kuna siku alichelewa kutoa mhadhara baada ya kusukumizwa nje ya treni kwavile tu ni mweusi!

Commission hiyo baada ya hapo ikaenda Afrika ya Kusini ambako DR. AGGREY alitoa moja kati ya hotuba bora kabisa kuwahi kutolewa na Mwafrika ambapo, kwa ufupi, alisema: :
*"By Education, I don't simply mean learning. I mean the training of the mind, in morals and in a hand that helps to make one socially efficient. Not simply the three R's, but the three H's ie the Head, the Hand and the Heart. No race or people can rise half slave, half free. The surest way to keep a people down is to educate the men and neglect the women. If you educate a man you simply educate an individual but if you educate a woman you educate a family."*

*"I am proud of my colour and whoever is not proud of his colour is not fit to live. Keep your temper and smile. That is what Jesus meant when he told men to turn the other cheek."*

*"I have no time for revenge, that is not African. Some white people ought to be transformed to Negros just for a few days, so as to feel what we feel and suffer what we suffer. I prefer to be a Spokesman of my entire country: Africa, My Africa"*.

*"My fellow Africans, I dont care what you know; show me what you can do. Many of you who get educated dont work, but take to drink. You see white people drink so you think you can drink too. You imitate the weakness of the white people, but not their greatness. You won't imitate a whiteman working hard"*.

*"If you play only the white notes on a piano, you get only sharps; if only the black keys, you get flats. But if you play the two together you get harmony and beautiful music"*.

Baada ya kutoa muhadhara huo White settlers walichanganyikiwa kwa uwezo mkubwa wa DR. AGGREY na na kiongozi wao akatamka-: *Damn his colour, he is a saint*!.

DR. AGGREY alikuwa ni mjuzi wa mambo mengi lakini hobby yake kubwa ilikuwa ni kusoma vitabu vya kila aina na alipenda kusema-: *I want to know everything"*. Alikuwa akijisomea hadi usiku wa manani. Aliposinzia, alikuwaakichukua taulo akalichovya kwenye maji na kujifunga kichwani na kuweka miguu yake kwenye karai la maji ya baridi ili aendelee kusoma vitabu vyake! Kwa hakika, alipenda sana kusoma vitabu.

Dr. AGGREY alikuwa akiongea Queen's English na alipozuru US kwa mara ya kwanza, wamarekani hawakuamini kama mwafrika angekuweza kuongea kwa lafudhi ile na kupelekea Waziri HEC Byrant aseme:
*"He is dark as dark, but very few in America can use English as he can"*.

DR. AGGREY alifariki dunia nchini US tarehe 30 Julai 1927 kutokana na ugonjwa wa Meningatis na kuzikwa North Carolina, US.

Kwa heshima ya DR. AGGREY, mwaka 2017 nchini Ghana, picha yake iliwekwa kwenye fedha ya nchi hiyo(5 Cedi Bill).

Huyo ndie DR. JAMES EMMANUEL KWEGYIL AGGREY mwenye mchango mkubwa katika historia ya Taifa letu.



*You Will Never Walk Alone!*
Addition😀r.Agrgrey ndo' mwafrika wa kwanza kutunikiwa PhD.
 
Bujibuji hongera kwa elimu nzuri,kuna wakati nilitembelea Ghana niliambiwa na wenyeji kuwa Dr.Aggrey alikuwa anaweza kuongea lugha zaidi ya 07 za kimataifa (more than 07 international languages) pia aliwahi kuwa mwalimu Chuo cha ualimu Accra kama sikosei.Hakika alibarikiwa sana na pia alikuwa akimcha MUNGU sana.
 
Dr. JAMES EMMANUEL KWEGYIL AGGREY, aliyezaliwa mwaka 1875 na kufariki takribani miaka 100 iliyopita, ni Mghana ambaye kamwe hatasahaulika katika historia ya nchi yetu, ingawa takriban 90% ya Wabongo hawajawahi hata kumsikia!.

Dr. AGGREY alikuwa ni Mwalimu mahiri aliyeheshimika duniani kote. Tarehe 15.5.1895, akiwa Mwalimu-kijana wa miaka 20 tu, alifanya mtihani pamoja na waalimu wenzake wengine 119 kutoka mikoa yote nchini Ghana uliotungwa Uingereza. Dr. AGGREY aliibuka kinara ambapo alitunukiwa cheti na Malkia kilichoandikwa- "This Certificate of Distinction, qualifies you, without further examination, to teach in any school in any British colony". Dr. AGGREY alikuwa Mwafrika wa kwanza kutunukiwa tuzo hiyo na Malkia!.

DR. AGGREY, kutokana na weledi wake wa kipekee, aliteuliwa kuwa mjumbe wa "Phelps-Stokes Fund Commission" iliyoundwa kuangalia namna kuwaendeleza Waafrika kielimu. Tume hiyo iliundwa kutokana na Mmarekani Bi. CAROLYINE PHELPS STOKES, aliyefariki 1909, kuacha kitita cha fedha na wosia uliosema- "I bequeath $ 1,000,000 to my trustees to be used for the education of Negros, both in Africa and the United States". Tume hiyo ilizuru mataifa 10 ya Afrika ambapo ilikuja Tanganyika na Zanzibar na kukaa toka Machi 1924 hadi April 1924. Dr. AGGREY alikuwa Mwafrika pekee kwenye Tume hiyo katika kipindi hicho ambapo ubaguzi wa rangi ulikuwa umetamalaki duniani kote. Hata kuwa mjumbe katika Tume hiyo ilikuwa ni kwa mbinde!.

Wajumbe wa Tume hiyo walipowasili nchini walifikia NEW AFRICA HOTEL, moja ya hoteli kubwa 2 nchini wakati huo. Katika hali ya kusikitisha, Dr. AGGREY alikataliwa katakata kupewa chumba kutokana na kuwa mweusi na hivyo ikabidi akatafute hoteli Kariakoo!.

Ubaguzi huu ulimuhuzunisha sana lakini haukumkatisha tamaa. Akiwa Kariakoo, alijichanganya sana na Watanganyika na kupelekea kujuana na KLEIST SYKES, Mtanganyika msomi aliyekuwa akiongea Kiingereza na Kijerumani kwa ufasaha na mjuzi wa mambo mengi ambaye asili yake ilikuwa Afrika ya Kusini.

DR. AGGREY "alimpiga shule na kumpa nondo kali" Bw. KLEIST juu ya umuhimu wa kuanzisha chama kwa minajiri ya kupigania haki za Watanganyika. "Shule"hiyo ilimuingia vilivyo Dr. KLEIST, kama alivyokiri mwenyewe baadae, na hatimaye yeye na wenzake wakaanzisha chama cha AFRICAN ASSOCIATION (AA) mwaka 1929. AA ilibadilishwa na kuwa TANGANYIKA AFRICAN ASSOCIATION mwaka 1948. AA ndiyo ilikuwa chimbuko la TANU iliyoundwa tarehe 7.7.1954.

Tume ilipotoka hapa nchini ilikwenda Belgium Congo kuendelea na jukumu la kuwaendeleza waafrika. Baada ya kazi ya siku nzima ya kwanza, Gavana MARTIN RUTTEN aliialika Tume hiyo Ikulu kwaajili ya "dinner". Gavana huyo mbaguzi alichukia sana kumuona mtu mweusi kwenye Tume hiyo hivyo akamuamuru Dr. AGGREY asikanyage ndani bali abaki getini!. Dr. AGGREY akakaa hapo getini na walinzi kuanzia saa 1 hadi saa 8 usiku "dinner" hiyo ilipoisha na "hakuna rangi aliyoacha kuiona" kwani kulikuwa na kibaridi kikali na mbu wengi!.

Figisufigisu hizi za ubaguzi hazikumkatisha tamaa bali zilimuongezea morali zaidi wa kuwasaidia Waafrika wenzake kielimu. Tume hiyo ikaenda Angola ambako nako masaibu ya ubaguzi "hayakumuacha salama" na yaliendelea kumkumba ambapo ilibidi tu "apambane na hali yake". Kuna siku alionja "joto la jiwe" aliposukumizwa nje ya treni kwavile tu ni mweusi na hivyo kuumia mguu wa kulia na mkono wa kushoto na kulazimika kuchelewa mhadhara wake wa elimu!.

Tume hiyo, baadae, ikaenda Afrika ya Kusini ambako Dr. AGGREY alitoa Hotuba Bora kabisa kuwahi kutolewa na Mwafrika katika karne ya 20. Dr. AGGREY, kwa ufupi, alisema kuhusu elimu:

"By education I don't simply mean learning. I mean the training of the mind, in morals and in a hand that helps to make one socially efficient. Not simply the 3 Rs, but the 3 Hs ie the Head, the Hand and the Heart. No race or people can rise half slave, half free. The surest way to keep people down is to educate the men and neglect the women. If you educate a man you simply educate an individual but if you educate a woman, you educate a family."

"I am proud of my colour and whoever is not proud of his colour, is not fit to live. Keep your temper and smile. That is what JESUS CHRIST meant when he told men to turn the other cheek".

"I have no time for revenge, that is not African. Some white people ought to be transformed to Negros just for a few days so as to feel what we feel and suffer what we suffer. I prefer to be a spokesman of my entire country: Africa, My Africa!".

"My fellow Africans I don't care what you know, show me what you can do. Many of you who get educated don't work, but like to drink. You see white people drink and think you can drink too. You imitate the weakness of white people but not their greatness. You won't imitate the whiteman working hard!".

"If you play only the white notes on a piano, you get only sharps; if only the black keys, you get flats. But if you play the two together, you get harmony and beautiful music".

Baada ya kutoa hotuba hiyo, umati mkubwa uliokuwepo ulimbeba msobemsobe huku SMURTZ MCNAMARA, Kiongozi wa "White settlers, akitamka- "Damn his colour, He is a Saint!".

Kwa miaka mingi, hotuba hiyo ya kihistoria iliyosheheni "madini" lukuki, imekuwa ikinukuliwa na viongozi wengi duniani akiwemo marehemu Nelson Mandela, ambaye wakati akigombea urais, tarehe 2.2.1994, aliulizwa akishinda atawachukulia hatua gani makaburu waliomtesa kwa miaka 27, nae akajibu "My answer is very short: let me quote from one of the speeches of my idol, Dr. JAMES AGGREY, " I have no time for revenge. That is not African".

DR. AGGREY alikuwa mjuzi wa mambo mengi na "Hobby" yake kubwa ilikuwa ni kusoma vitabu vya kila aina hadi usiku wa manani. Alipokuwa akisinzia, alichukua kitambaa akachovya maji ya baridi na kujifunga kichwani na kuweka miguu kwenye karai la maji ya baridi! Aidha, DR. AGGREY alikuwa anaongea "Queens English" ya hali ya juu na alipelekea Waziri Mmarekani, Mh. HEC BRYANT aseme: "He is dark as dark, but very few in America can use English as he can!".

DR. AGGREY alifariki dunia mwaka 1927 na kuzikwa North Calorina, Marekani alikokuwa akiishi na kufundisha.

Nchini Ghana, kwa heshima ya Dr. AGGREY, picha yake iliweka kwenye moja ya noti za nchi hiyo (5 Cedi Bill)! Hii ilikuwa ni ajabu sana kwani marais wengi wa Afrika hupenda "kuuza sura kwenye noti!.

Kutokana na umuhimu wake katika historia ya nchini yetu, mtaa mmoja jijini ukapewa jina lake kama kumbukumbu "MTAA WA AGGREY". Mtaa huo uko maeneo ya Kitumbini kuelekea Kariakoo jijini Dar Es Salaam.

Huyu ndiye DR. JAMES EMMANUEL KWEGYIL AGGREY, Mghana mahiri mwenye mchango mkubwa katika historia ya nchi yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom