Historia ya Mtibwa sugar

Historia ya Mtibwa sugar

Iamjac16

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
214
Reaction score
53
1615825797461.png

Mtibwa Sugar Sports Club inayopatikana katika mkoa wa Morogoro wilaya ya Mvomero takribani kilometa mia moja (100) kutoka Morogoro mjini ilianzishwa na wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa. Madhumuni ya awali ilikuwa kushiriki ligi katika ngazi ya wilaya na kutoa burudani kwa wafanyakazi. Mnamo mwaka 1989 timu ya mpira wa miguu ya mtibwa Sugar ilianza kushiriki ligi daraja la nne (4th division league) na kupanda ngazi kwa ngazi hadi daraja la kwanza mnamo mwaka 1996. Mashindano ya ligi daraja la kwanza.

Mtibwa Sugar ilianza kuonyesha matamanio ya dhati ya kucheza ligi kuu miaka mitano tu baada ya kuanzishwa kwake mwaka 1988.

Hilo lilipelekea kuanza kuwasaini wachezaji wakali. Salhina Mjengwa mmoja wa wafungaji bora wa muda wote klabuni hapo, John Thomas Masaki ambaye alikuwa mfungaji mkali kutokea Singida, Said Msham aliyesajiliwa kutoka Majimaji, Christopher Michael aliyetokea Tiger ya Tunduma, Loui John, Kassim Mwabuda ambao walisajiliwa kutokea Coastal ya Tanga wote hawa walisajiliwa mwaka 1995 wakati ambao klabu iliamua kwa dhati kuitoa timu hiyo katika ligi daraja la tatu hadi ligi kuu.

Usajili ‘bab-kubwa’ waipa taji la kwanza
Abubakary Mkangwa alikuwa mchezaji-mfungaji aliyekuwa akichipukia vizuri , Moja Liseki, Yusuph Macho, golikipa Steven Nemes, Zubeiry Katwila wote hawa walikuwa mastaa waliosajiliwa kutoka Yanga na Simba na kocha John Simkoko kwa msaada wa mratibu wa timu hiyo Jamal Bayser mwaka 1998.

Mlinzi wa kushoto Kassim Issa naye alisajiliwa mwaka huo na kuungana na kina Mjengwa, Masamaki, Geofrey Magori, Mayanga, Meck Mexime na wengineo.

Siku ya mwisho wa msimu wa 1999 katika mchezo wa kukumbukwa sana katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro kwa mara ya kwanza Mtibwa Sugar FC ikatawazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu baada ya kuifunga Yanga 2-1 katika mchezo wa kusisimua ambao hadi kufikia dakika ya 86 ilionekana wazi Yanga wanakwenda kushinda ubingwa wa nne mfululizo kwani walikuwa mbele kwa goli 1-0 na matokeo hayo ama sare yalikuwa yakiwapa taji lingine baada ya kutwaa mfululizo misimu ya 1996, 1997 na 1998, Salum Mayanga kocha wa sasa wa timu ya Taifa ametoka nayo sana timu hii, toka ligi daraja la tatu.

Marehemu Said Mhando pia ni kati ya watu walisaidia sana kuifikisha Mtibwa hapa ilipo sasa. Wakati tunatwaa ubingwa wa kwanza mwaka 1999 Mayanga alikuwa mchezaji, lakini mara nyingi alikuwa akimsaidia kocha simkoko. Yanga walikuwa wakihitaji sare ili kushinda ubingwa na walikuwa tayari wanaongoza mchezo hadi kufikia dakika tatu kabla ya kumalizika, lakini mambo yalikuja kugeuka dakika za majeruhi .

Timu ya kwanza kutoka nje ya Yanga na Simba kutetea ubingwa wa ligi kuu bara

Mara baada ya kikosi cha Simkoko kushinda ubingwa wa kwanza wa ligi kuu mwaka 1999 ikiwa ni miaka miwili tangu wapande ligi kuu mwaka 1997, timu hiyo iliendeleza makali yake na kufanikiwa kumaliza juu ya Yanga na Simba na kutwaa ubingwa wa ligi kuu mwaka 2000.

Usajili mzuri tuliofanya kipindi hicho na maandalizi mazuri kabla ya kuanza kwa msimu . Prisons ndiyo timu iliyokuwa ikiwapa sana tabu kwa sababu nao walikuwa ‘fit’ kama, lakini Yanga na Simba hazikuwa zikifua dafu
 
Naipenda sana timu hii, sema wanakaujinga fulani, wanatengeneza wachezaji wazuri na wanauzwa timu inakosa consistency kabisa, kwa timu iliyokuwa na historia nzuri inavurugwa na viongozi wasio na maono na nia ya kuondoa utawala wa Simba na yanga kabisa

Sent from my Infinix X652 using JamiiForums mobile app
 
Usajili bora wa mtibwa ni ule wa mwaka 1997! Vijana wadogo kama Meck Mexime, Kamba Lufo, Abubakari Mkangwa, Masumbuko Hassan, Geoffrey Magori n.k waliingia ktk timu! Mbali na hao Mtibwa wamepita watu wa maana haswa, hapa kuna kina Salum Mayanga, Manyika, Saidi Mhando (alikuwa kipa baadae akawa mshambuliaji), Niko Nyagawa, Mussa Mgosi, Victor Costa, Abdala Juma (aliwahi kuwa mfungaji bora) Patrick Batwel, Oddo Nombo, Ramadhani Ngubiagai, Abdi Kassim, Zuberi Katwila, Christopher Gaga, Mengi Matunda.....daah wengi sana wamepita pale Manungu! Hadi hawa wa juzi kina Kichuya, Mzamiru, Dante, Mo Ibrahim, Juma Abdul na wengineo! Hii timu sijui kwa nini inapotea siku hizi!
 
Mwaka 1991/92 ligi daraja la 4 mkoa Morogoro mpaka nusu ya kwanza ya mchezo ilifungwa 2-0 na Shujaaa SC
Ikasawazisha nusu ya pili kwa mbeleko mpaka dk 90 matokeo yalikuwa 2-2
 
Back
Top Bottom