Historia ya Nasibu Abdul Juma(Diamond Platnumz)

SACO

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2011
Posts
2,623
Reaction score
3,397
FAHAMU MACHACHE USIYOYAJUA KUHUSU DIAMOND PLATNUMZ NA JINSI MAMA YAKE ALIVYOMPIGANIA

Jina lake halisi anaitwa Nasibu Abdul Juma maarufu kama "Diamond Platnumz", alizaliwa tarehe 2, October mwaka 1989 katika Hospitali ya Amana DSM mida ya saa 11 usiku.

Akiwa mdogo sana baba yake alimtelekeza yeye na mama yake, iliwabidi wahamie Tandale kwa bibi yake mzaa mama, hapo ndipo yakawa makazi yao, wakakabidhiwa vyumba viwili ilibidi wapangishe vyumba hivyo ili kuwapatia kipato maana hawakuwa na source ya kuwapatia kipato, ikabidi wawe wanalala chumba kimoja yeye, Mama yake na Bibi yake.

Mwaka 1995 alianza kusoma chekechea na msingi katika shule ya Chakula Bora iliyopo Tandale, Diamond alimtafuta Baba yake ili amsaidie japo vitu vidogo vidogo kama viatu vya shule lakini Baba yake alimkataa kata kata akidai hamtambui kama mtoto wake, Mzee huyo akazidi kula starehe na wanawake wengine akimuona mama diamond si kitu.

Mwaka 2000 Diamond akiwa darasa la 5 alionekana kuanza kupenda muziki, hivyo alianza kucopy baadhi ya nyimbo za wasanii waliokuwa wakubwa enzi hizo.

Mama yake alikuwa akimnunulia Diamond kanda za album za wasanii tofauti na kumuandikia baadhi ya nyimbo za wasanii hao ili mwanae aweze kuzishika na kuimba kirahisi, wakati mwingine hata kumpeleka katika matamasha tofauti tofauti ya tallent show ili mwanae apate nafasi ya kuimba, kitu ambacho baadhi ya ndugu wa familia waliona ni kama kumpotosha na kumuharibu mtoto huyo badala ya kumuhimiza kimasomo.

Story ya Maisha yake ni ndefu sana kwa leo tuishie hapa
 
Solomon also stated: "A wise son is the one that makes a father rejoice, and a stupid son is the grief of his mother."
 
Mambo ya kike hayo, we unajua kisa gani kilipelekea wazaze wake watengane?
Una ushahidi gani kwamba Baba yake alikataa kumsaidia?
 
Ndoa ina mambo mengi sana na wanoko huwa wanaongea wanaloona litauzika ila ukweli wanaujua wao.
Je kama mama alikuwa anachepuka mlitaka baba atangaze?
Kama mtoto aliyaona haya akauchuna je?
Sisi hayatuhusu kwani dunia hii ina mengi sana

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
DIAMOND YUPO SAWA KABISA. ADUI YAKO MUOMBEE NJAA TUU NA MABAYA. UTAKUWA MPUMBAVU UKIMUOMBEA SHIBE NA MEMA.

Kwa sababu ana shida ndio analialia asaidiwe? Qubaaf kabisa, Kasahau kabisa alivyomkana kuwatesa na kiwatelekeza.

Nyambaf
 
Back
Top Bottom