Historia ya pesa ya sarafu Tanzania

Historia ya pesa ya sarafu Tanzania

Swahili AI

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2016
Posts
10,174
Reaction score
89,364
Baada ya vita ya dunia mwaka 1919, Bara na Zanzibar pamoja na Kenya na Uganda zilikuwa chini ya himaya ya mwingereza ingawa kwa mikataba tofauti. Kuanzia hapo nchi hizo zilianza kutumia sarafu moja.

Katika kipindi kifupi kuanzia mishoni mwaka 1919 hadi kati kati ya mwaka 1920, bara walitumia rupie za kijerumani pamoja na rupie za kiingereza zilizokuwa zikitumika nchini Kenya, Uganda na Zanzibar.

Baada ya hapo, sarafu mpya ya Florin ya Afrika Mashariki iliingizwa kwenye mzunguko badala ya rupie na rupee. Kwa bahati mbaya sarafu hii ya Florin haikudumu muda mrefu na mwanzoni mwa mwaka 1921 ikabadilishwa na Shillingi ya Afrika ya Mashariki.

Kwa hali hiyo kuna sarafu chache sana za Florin zilizotolewa katika kipindi hicho na sikufanikiwa kupata picha yake. Sarafu ya Shilingi ya Afrika Mashahariki ni kati ya sarafu imara sana zilizokaa kwenye mzunguko kwa muda mrefu bila kufanyiwa mabadiliko yoyote.

Ilitolewa katika vipande vya senti 1, senti 5, senti 10, senti 50(nusu shillingi) na shilingi 1. Upande mmoka wa sarafu hizo ulionyesha jina la mtawala wa himaya ya uingereza, na upande wa pili ama ulikuwa na ama pembe za tembo au picha ya simba dume. Pembe za tembo zilikuwa kwenye sarafu za senti 1, senti 5 na senti 10 wakati simba dume alikuwa kwenye sarafu za senti hamsini na shilingi moja kama ifuatavyo

Nyuma ya sarafu

ykeFIeEXdcoeC1oVy07Pk7v6792psK7qOeZBwutYtAIpm-WM5uhkYHnxkal_SjEVVCSxhEJtpE39R-oQg4hh3H8HEXRy8pd8jg=w5000-h5000


LvkBAGOn6cC6in63pAAAiEuyHB4QNj5iypXJ2nJV14naLh3A8LRba92NM07S9x-9mjT70fKRk-FSdmsAV1nTajNicxRq4ai5zp2OOqRG=w5000-h5000

Upande ulioonyesha mtawala wa uingereza ulifanyiwa mabadiliko ya mara kwa mara kulingana na mabadiliko ya kiutawala. Kuanzia mwaka 1921 mpaka mwanzoni mwa mwaka 1936 wakati wa utawala wa Mfalme George wa tano sarafu zilikuwa na sura ifuatayo.
IKu34Z21JpA75SBA6ciiBaphZCA3Bru9twYpRHk3bGHfAhgTQiGmuBmMfBPPgO31RAGCGUer1pVb6K1meetS4PR1RKejTRTTSC0=w5000-h5000


hbwYAo0e5mRJW4ITBRkCFgZiTbjuuJbZFJ9iF3O9aBbD8dOodCN_OBv2Dn93OAFNvD1_HY9iB-B1BuQ_UGCxqkmb6s25twuQM_9p=w5000-h5000

Baada ya kifo cha Mfame George wa tano na utawala kuchukuliwa na Mfalme Edward wa nane, ni sarafu moja tu iliyobadilishwa kwa vile mfalme huyu alivuliwa madaraka baada ya muda mfupi tu kutokana na uamuzi wake wa kuoa mwanamke aliyekuwa ameachika Marekani. Sarafu iliyobadilika wakati huo ilikuwa ya senti tano tu, ambayo ilionekana kama ifuatavyo

senti 5

pYsDiqQlC4yiaAMmkccI32ZF1NYRjYfXZxg5Q-Y9y8N8hajaygA7CECUWXK4ejTjTkbEWrk1Gc-zAWi_Hj1dYnLf9ACDCpTgGQaYjZI=w5000-h5000

Mfalme George wa sita aliyekuwa mdogo wa mfalme Edward wa nane alichukua madaraka mwishoni mwa mwaka huo huo wa 1936.

Sarafu zilizotengezwa wakati wa utawala wake zilikuwa na sura za aina mbili. Sura ya kwanza ilionyesha mfalme kama GEORGIVS VI. Sarafu za aina hii zilitolewa kati ya mwaka 1937 hadi mwaka 1946; zilikuwa na sura ifuatayo.

3HL9bRkku6CNiI7FAKvBLMSqc62EinGcLIYwXFpIvVKXBKOfNCLFZpXTW6v-tbhXjD3fELJ3Y8foJPLBSg_q-7nuBD9oWAaxq7Gy=w5000-h5000


JNgEmSo1tJzI9nlpTWMI-cfS5rc-XRYz2DIsm04N3cVmU6mHBHrs7N02p7TnIYTuNCU-rf8y3kVTxTu-ZXH8SkkbCOu_dWS6CFQWqA=w5000-h5000

Sarafu za aina ya pili cghini ya Mfalme george wa sita silikuwa na maneno ya GEORGIVS SEXTVS REX. Hizi zilitolewa kati ya

mwaka 1949 hadi mwaka 1952 alipofariki. sarafu hizo zilionekana kama ifuatavyo.
2FiQAfy1kE4fXFcpRgEzsoEixEo9usnh7k7jMZWi5Isvm68uNfWXuF7Tiy2MIZPrMkSQvShvta6wF3P_kR0vBC0gPkozZnpJRMYOlNcF=w5000-h5000


SxNCAXF-S6Wl39Pl9yMg8ZASISlm0z5jrOiejhAvJDHqVByhz_U7mksA37KzZVYcSOz8LNsrOqGoRGV44RMJa6Os5T1mMDw427OVZQA=w5000-h5000

Baada ya mfalme George wa sita kufariki, alirithiwa na binti yake Malkia Elizabeth wa pili mwaka 1952. Chini ya malkia huyu sarafu ziliokena kama ifuatavyo.

DwL-5iFNuh3KDI2bvMuBJNSAlQ4fsLszhyPCxqBNMwnYJrPP6ufstcySDqcBs0e9oOPU40g1hr_UCW1LEYTqVaIevUsw-4w0sQdW2s8R=w5000-h5000


RSc5Bt3bIuDuE6ykMv_VyRUAAYkAWxuveyGis035N-tSqVuyc6wbEID-j6t6Pp2VcHmUjp6RbhIMlqXfbvJZIVFpqYCDjeGnXbpN1oDz=w5000-h5000

Sarafu hizi zilendelea kutumika hata baada ya kupata uhuru wetu. Kwa mafano sarafu zilizotolewa mwaka 1963 (baada ya uhuru)
zilionekana ifutavyo.

9hpMuxv82eK--Nfw3yXfey-TlxfYy5eL6cft79xzkaRCMauO5ORkOQf3RvXYTA04ZeALktu8Kpy5vyR9MMewDS4rKRlLTaJw9Q=w5000-h5000

Ilipofika mwaka 1964, kukafanyika mabadiliko kidogo katika sura ya sarafu yetu kwa kuondoa maneno yanayoonyesha mtawala wa himaya ya kiingereza. Sarafu za senti tano na senti kumi zilizotolewa mwaka 1964 zilikuwa zinaonekana kama ifuatavyo.

I4udK57kk4T05cmFZ1P7IQ9egx1cMQm9jJ5dBSrr9phQAaLH-GR15MdYuHtq3KvAYm_I5g1UeIB60d8YYpwlIjlJn0j-oJ0tqQ=w5000-h5000

Hata hivyo sarafu ya pamoja ya Afrika Mashariki ilifikia kikomo chake mwaka 1966 wakati Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki ilipovunjwa na kuundwa kwa benki kuu za Tanzania, Kenya na Uganda. Sijaelewa sababu ya kuvunjika kwa bodi hiyo ya sarafu, bado ninafanya utafiti. Nikizpta nitawagawieni.
 
Benki Kuu ya Tanzania ilitoa sarafu nne za kwanza mara tu baada ya kuundwa 1966. Sarafu hizo zilikuwa za senti tano, senti ishirini, senti hamsini na shilingi moja. sarafu hizo zilionekana kama ifuatavyo:

senti 5
4kfMa0IBS1nZ1CZoElkvSWa7-FVagcvEKlFQCqZFcc-4aVwfXh19mFdMkt2GsdYtdOeEbvuVTmnsHop0mb4_KlGkmd3EtywEuI-h1bwuJY9_8Q=w5000-h5000

senti 20
zd4mGE8VWn7bDxybAU9FGi9GD8td1mgBc4RFAG_tg-1Ek6jFb0j6DFMPtbASvmOEkaNbkGPybxfPyad_CJLoo3JDKci3PvAB0_K3N-gKRh9iuqs=w5000-h5000


senti 50
0G49K6g5d5gjrLNUYHNmBETBjU0dYIkDJHFFXMM0JLRYaUWT4_dZ-RNIMRqCy_58RjLjo9SjwC2T-lRMDfuodnavpu1dyH7kKmHHUSjSRwHJ5Nc=w5000-h5000


Shilingi 1
-63UuhFPBVZ8JxkP7B5Ju6nue1aEJqlusenosGPuN35tiL5sW6dKKhwMm1O_q6Ml4bGvKR9esaimHg50Cm7O7B8lWPr5smksqft-s9CXvGHzUkPWrw=w5000-h5000


Sarafu hizi zinaendelea kutumika hadi leo ingawa thamani ya shilingi imeshuka kiasi kuwa zinaonekana hazina thamani yoyote. Ilipofika mwaka 1971 wakati wa sherehe za miaka kumi ya uhuru, sarafu mpya ya shilingi tano iliyokuwa na pembe kumi na mbili ilitolewa. Wakati huo exchange rate ya dola kwa shilingi ilikuwa ni shilingi tano kwa dola moja ya kimarekani. Kwa hiyo sarafu hii ya shilingi tano ilijuikana pia kama "dola" au "DALA" ingawa kwenye mikoa ya ziwa ilijulikana zaidi kama "Scania." Nadhani mnakumbukua chanzo cha neno "dala dala" ni kutokana na nauli ya mabasi hayo wakati huo kuwa shilingi tano. Sarafu hii ya miaka kumi ya uhuru haikudumu sana na mwaka 1972 ikabadilishwa sura na kuwa na pembe kumi kama ifuatavyo.

Shilingi 5
g-rm_GtAyw825VZqF1RBx0Ub9mmkhoBVOIQ-N2IZM7A4uPLeJTpOCN23c-IkzGblDkmyrofKB6AmXWPb0FPMF9p6blxpfw13DXDC7Bi7-QYMvYCgjg=w5000-h5000


Kuna taarifa kuwa mwaka 1974 sarafu mpya za shilingi 25 na shilingi 1000 zilitolewa ingawa benki kuu haikutunza picha zake. Ingawa sikuweza kupata sura ya sarafu ya shillingi 1000, nimefanikiwa kupata picha ya sarafu ya shillingi 25 ambayo ilikuwa na sura ifuatayo:

shilingi 25
Jc5fNxP0sTRRnRtiIjHaSZQydGWdKg9seRnGsL7WHMkQkeyBaK2FeApzqMfOJzfQFbeug6gXpxZ2AbAn_rUbdxUkE4g8mmF07y-cFPlccpNpkq2BLA87GeQvUhtpNFHF6ajA0VlgN6p0QkdmaKN9emg=w5000-h5000


Mara baada ya kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977, thamani ya pesa ilianza kupunguka pole pole kiasi kuwa kulikuwa na haja ya kuwa na sarafu kati ya senti ishirini na senti tano. Hivyo sarafu ya senti kumi iliingizwa kwenye mzunguko; sarafu hii ilikuwa kama ifuatavyo.

senti 10
PLDb7fqRoflfZ93D1Oco7yNpgFIbAgpYXGhVmfH9ikUewifm5ASNzfCafoTqeudb4O-4GxIDIW9TDdeRFXd9Bvceoc319ajPJKAGU0TLjaGzMoQ=w5000-h5000


Kufuatia mkutano wa FAO uliofanyika Arusha mwezi September mwaka 1978, sarafu chache za shillingi 5 zilitolewa kukumbukia mkutano huo; sarafu hizo zikuwa na sura ifuatayo

Shillingi 5
xfAnVlVTA1cvrEtlPLZ2LIJJvjiy0s06UzcjjasyOpfU4Hg5gFXm49NWCPd3CElpJKyB-1TfgMR-yrsvmGai4yTRFwGnmZNfQYY=w5000-h5000


Baada ya hapo, hakukuwa na sarafu mpya hadi mwaka 1982 wakati wa sherehe za miaka 20ya uhuru ambapo sarafu mpya ya shillingi 20 ilitolewa ikiwa na sura ifuatayo.

Shillingi 20.
C-lscth_x-Bhq4bZg__uwJFDIPvES9G0jpFG58FteloRO2kuPXI9_mTAuzeUw1iVAT-j5GMvAUGD0gfRRbLWOvzQYaQGQqWFzhE=w5000-h5000


Hiyo ndiyo iliyokuwa sarafu ya mwisho kutolewa wakati wa utawala wa Nyerere. Rais Mwinyi alipochukua madaraka mwaka 1985, aliendelea na sarafu zenye picha ya Nyerere hadi mwaka 1986 zilipotolewa sarafu zenye picha ya Mwinyi. Sarafu za senti tano,
kumi, na ishirini hazikutolewa tena. Sarafu zilizotolewa wakati huo zilikuwa za senti 50, Shilingi 1, shilingi tano na shilingi kumi ambayo ilikuwa na sura ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Sarafu hizo ni hizi hapa:


senti hamsini

rds9y0QAB_bqZvQygUQzlX9jHPXL6rNMzoCMTsFPYy2UkTVwUhFV7ZEIDPHh9RfTyU6mJTHPPIs9BGDX_V7YAhAxp0d83svMgUquKBbdRA=w5000-h5000


Shilingi moja

919p4ZRlW8iyppnU1B8PshR6OgKbLfl4j0AN3XwrlBG_22Gh4DP5B__iTq1Z3CwOhQwRlY4rsEvWbmOfUEdXraLOPOxTcsc7mgL5gDkFZEIZ=w5000-h5000


Shilingi tano
t58vm9AT2rWR7TXpyPG2QCN5sGPkupwAucy1ILw6yUIsEO0uNLmhxbArNBJFkFtg-Xu2zrcap0F2HcmhWkQc5XRGSGLQuE_y4ld2I9daWSjRLA=w5000-h5000


Shilingi 10
ypubDDkgtFnTV8GY4laVaukSqIykX0393Iqh-2gfJM23SfXD7mx6R5hXcc5s9CzzJG5ySBn7a10rt5eSMuTJ_3cZcTGYV8xp_ZDjxqVm8GWLESs=w5000-h5000



Kadri thamani ya shilingi ilivyoendelea kudorora, ilibdi kutengeneza sarafu nyingine ambapo sarafu ya shilingi 20 ilitolewa mwaka 1990 ikiwa na sura ya Mwinyi kama ifuatavyo.

Shilingi 20

7QGaBz1ZiZ2VDZbiswpXbMIeHpALOBRvA4cHAmfgbm0q1O0SeqXfycWx1zrpGU62py0plPe6YCEp1uSVI86Pu9VLUxTBKd04Re3NI5knkM3V-20=w5000-h5000


Mwaka huo huo sarafu nyingine ya shilingi 5 ilitolewa kwa kumbukumbu ya jengo jipya la benki kuu. Kwa bahati mbaya sikufanikiwa kupata picha yake. Mwishoni mwa utawala wa mwinyi, thamani ya shilingi ilikuwa chini kiasi kuwa sarafu ya Baba wa Taifa yenye thamani ya shilingu kumi ilikuwa inakimbilia kuishiwa nguvu yake. Hivyo sarafu mpya yenye sura wa baba wa taifa ikatengezwa ikiwa na thamani ya shillingi 100.

Shilingi 100
MhQl0BQO9tMYSxARJa55RjTd6OyTcXDW5gGDibhj30ERzlRsjR8WBx-sf6n_rfER591SQozaNJ1E7955ZXBO6POz__AutOQl_YNApZts-CHZzwjF=w5000-h5000
 
Rais Mkapa alipoingia madarakani mwaka 1995, akapiga marufuku matumizi ya sura za raisi aliyeko madarakani kwenye sarafu: alipendelea sura za waasisi wa taifa tu na picha alama za asili za nchi ndizo zitumike. Hata hivyo hakutaka kuondoa kabisa sura ya rais Mwinyi kwenye sarafu, hivyo ikatengezwa sarafu mpya ya shilingi 50 iliyokuwa na sura ya Mwinyi kama ionekanavyo hapo chini iliyotolewa mwaka 1996.

Shilingi 50
0dBt-vXb34v2Zb0dfRWUXsXG7lXKtOIRNWz7CLgrR4Qeu3KoliHHKmhGDlOL72T_EDYCyc-wZ42rbqsvRWcfMOhafQvd-aJngHtGLlS5or8DUQ=w5000-h5000


Wakati huo huo sarafu tatu zilitolewa kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 35 ya uhuru pamoja ni michezo ya 26 ya olimpiki iliyofanyika Atlanta Marekani mwaka huo. Sarafu hizi zilionyesha wachezaji wa kutupa tufe, riadha, na karate kama ifuatavyo.

tufe
oo-jqjw-Uv5OHOvjIHpGR1ZgwqOl_ebV4tfpo0PWQk2NydDmNIeoQok6ZVzgR0Kct4AyO-nJmVJYE6cjl12HYAVRCdt6BC3a0KvQ4dqpLJw=w5000-h5000


riadha
EjtBVoFNVOCnj102mFzLiRx40jixsNp69aAqApzPmtElAALrQpvCGeppqOtVlTzQhZ5ILUJMI9UzE1yYbriTOnYA-0XbiPdBPkqJm4N43L4=w5000-h5000



karate
-vCbjSw7pq19U55ohinyGfkQnL80oagTb02GuZyCDkJyNERHBIHIDf_WdupWiERJzBd8zWP43DHCw2TCmHWPpr1ociwUW2mPZ8aNybg8NaE=w5000-h5000


Mwaka 1997 kulitolewa sarafu mbili mpya: moja ilikuwa na thamani ya shillingi 500 ikiwa inakumbukia miaka 75 tangu malkia Elizabeth mama wa malkia Elizabeth II alipotembelea nchi yetu mwaka 1923. Sarafu ya pili ilikuwa na thamani ya shillingi 200 ikiwa inatukuza mbuga za wanyama pori wa Afrika. Sarafu hizo zilikuwa na sura zifuatazo

Shilingi 200

qnKDKBm7LlxkLqi2wTSkpHJ179AjqaPPywSACB0Xp7m0mTliGyhfFAlU55scphppj3tEQFYi6SRDsBT9Nc4Ifxt2qCnHAOA_eand3Ar1Mw=w5000-h5000



Shilingi 500
BOdLNeHFYRgZbiVovstcYic77v-0aJNhxzYmQ2NW9dNgeAin9QYI4tEJg1f8T-IOZrUvTb3ayBaq1iD2Xw--gc90c5IkLDxJ0R2K7oflYN5YX68=w5000-h5000


Mwaka 1998, ilitolewa sarafu nyingine ya kudumu ya shilingi 200 kuchukua nafasi ya sarafu zote za kumbukumbu zilizokuwa na thamani hiyo. Sarafu hiyo ilikuwa na picha Karume na inaonekana kama ifuatavyo:

Shilingi 200
gcLn4104zfYR6ufRIaiCPXK_2iP8YMcxrACj-e8BUloP8XV0jnlu_4EdwCu3WE15ydErclJwpTnaOHFZp0ogLtuCyiB0PeQHuQQ=w5000-h5000


Mwaka huo huo, ilitolewa sarafu nyingine ya thamani ya shilingi mia tano kutukuza mbuga za Serengeti. Sarafu hiyo ilikuwa na sura ifuatayo.

Shilingi 500
l3oriqpIt1sNqfEhjNVDyJ8W1Uhzes7BKzTap2If4NEgKApZTH60MDX9r8B9MB0xAE5bG9ZMrHw-mAGl7uaA7PyYN3WRebQV8KIToCSz-TY4=w5000-h5000
 
Huu uzi ulipaswa ushinde lile shindano la jf
Miaka yote mitano kwa kutumia ID yako hii hujawahi kuona uzi wa Historia ya Sarafu ulioandikwa na Kichunguu mwaka 2007(mwaka mmoja baada ya JF kuanzishwa)!?, tena upo Pinned.

 
Nashukuru sana kwa historia na kumbukumbu hizi, tulipokuwa wadogo huko kijijini tulikuwa hatujui hata hizo za mzungu, mara ya kwanza kuona pesa ni chifu wetu alikutana nasi watoto akatupa juu chenji za sarafu za senti tano na kila mmoja akaokota nami nikapata senti tano yenye kishimo katikati
 
Back
Top Bottom