Historia ya Professor wa chuo cha Udsm aliyeuawa kwa bomu

Historia ya Professor wa chuo cha Udsm aliyeuawa kwa bomu

Babu Sisu

New Member
Joined
Sep 3, 2023
Posts
3
Reaction score
3
Miaka ya 1970 katika chuo cha kikuu cha Dar-es-salaam (UDSM) kulikuwa kuna Professor mmoja maarufu aliefahamika kwa jina la Walter Rodney alikuwa ni raia wa Guyana nchi inayopatikana bara la Amerika kusini

Rodney alikuwa ana PHD ya Historia ya Afrika aliyoipata katika chuo kikuu cha London kilicho nchini Uingereza, Elimu hiyo ilimjenga akawa mwanaharakati aliyepinga mifumo ya kikoloni barani afrika na kupigania haki ya mtu mweusi

Alianza safari yake kama Professor katika chuo cha West Indies kilichopo nchini Jamaica, lakini hakuridhishwa na uongozi wa serikali ya Jamaica ambao uliokuwa unalinda maslahi ya wazungu licha ya taifa hilo kuwa huru

Alizunguka mitaani kuwaelimisha wananchi historia ya Afrika na jinsi ya kupigania haki zao na aliikosoa serikali ya Jamaica kwa kuwatenga wananchi wa kawaida na kulinda maslahi ya mabeberu wa magharibi

Serikali ya Jamaica ilimfukuza na kumfungia Rodney kukanyaga katika nchi yao walihofia angeweza kufanya mapinduzi kwa serikali kwa itikadi zake kali

Kulizuka maandamano makali nchini Jamaica yaliyoitwa "Rodney Riot" wananchi walipinga uamuzi wa serikali kumfukuza Rodney waliyemuona kama mkombozi

Aliamia Tanzania akafanya kazi kama professor katika chuo kikuu cha Dar-es-salaam (UDSM) pia akaendelea na harakati zake za kisiasa

Alikuwa na urafiki mzuri na Julius Nyerere maana alisapoti mfumo wa ujamaa uliokuwa na lengo la kuweka usawa katika jamii na alisafiri vijijini mbalimbali kutoa somo kuhusu mfumo wa ujamaa pia aliunga mkono azimio la arusha lililofanyika mwaka 1967

Wakati huo Tanzania ilikuwa ni makao ya ukombozi Afrika, Nyerere na Rodney waliwakaribisha na kuwapa ushauri vyama vya siasa vilivyokuwa vinapigania uhuru wa nchi zao kama Frelimo(Msumbiji), ANC(Afrika Kusini) na MPA (Angola)

Akiwa chuo cha UDSM alianzisha umoja wa wanafunzi wanamapinduzi ulioitwa USARF lakini alitofautiana na mwalimu Nyerere baada ya umoja huo kukosoa serikali ya TANU, Nyerere aliuvunja umoja huo kwa kuleta itikadi ya kigeni ya Markixist ambayo ingesababisha machafuko, lakini urafiki wao haukuvunjika waliendelea kushirikiana

Aliondoka Tanzania mwaka 1974 na kurudi nchi kwao Guyana baada ya kuishi na kufundisha chuo kikuu cha Dar es salaam kwa kipindi cha miaka mitano na aliandika kitabu maarufu cha "How Europe undeveloped Afrika" kilikuwa kikielezea jinsi mataifa ya ulaya yanavyoinyonya afrika na kuifanya ibaki kuwa masikini

Rodney alikuwa ni mpinzani wa serikali ya nchini kwake alinyimwa nafasi ya kufundisha chuoni (professor) akiogopwa kuwa anaweza akafanya mapinduzi kama angepewa nafasi hiyo kwa itikadi kali alizokuwa nazo

Alihamishia nguvu zake kwenye siasa akaanzisha chama pinzani cha WPA (Working People Alliance)
kilichokuwa kinapinga ufisadi, udikteta na ubaguzi wa kisiasa uliokuwa unafanywa na serikali iiiyoongozwa na Forbes Burnham

Utawala wa Burnham ulikuwa ni wa kikatili sana ulikuwa ukiwaua kwa siri wapinzani walitumia mbinu ya kijasusi ya kudukua mawasiliano yao yaliwawezesha kujua siri zao

Rodney aligundua kuwa serikali ya Guyana ilitumia majasusi ili kujua siri zao alipata wazo la kuunda kifaa cha mawasiliano ambacho hakiwezi kudukuliwa na serikali kwa ajili ya usalama wa wanachama wa chama chake

Aliwasiliana na kaka yake Donald ambae alikuwa ni miongoni mwa wanachama wa WPA akamwambia kuwa amtafute mtaalamu wa IT ambae atabuni kifaa cha mawasiliano kitachoshindwa kudukuliwa na serikali kwa ajili ya usalama wao pindi wanapowasiliana

Taarifa za siri za kubuni kifaa kipya cha mawasiliano iliwafikia majasusi wa Jeshi la Guyana wakamteua Sajenti wa jeshi katika kitengo cha IT aitwae Gregory Smith asimamie mpango wa kusuka kifaa kipya cha mawasiliano kilichoitajika na Rodney

Zoezi la kusuka kifaa cha mawasiliano lilikamilika Gregory alichukua kifaa hicho akawakabidhi Rodney na Donald waweze kukifanyia majaribio ili kuona kama kitafaa kwa mawasiliano ya siri bila kujua kuwa kifaa hicho kilitengenezwa na majasusi wa jeshi la Guyana waliotega bomu kwa siri ndani ya kifaa hicho

Pimdi walipokabidhiwa kifaa na Gregory walipewa masharti kuwa wanatakiwa wajaribu kifaa hicho wakiwa ndani ya gari kwa kubonyeza button nyekundu ili kujua kama kifaa kitafanya kazi

Rodney na kaka yake waliingia ndani ya gari na kuondoka na kisha kwenda kusimama nje ya ukuta wa gereza la Georgetown walitoa kifaa hicho kwa lengo la kuwasiliana kwa siri na wafungwa wa kisiasa wapinzani waliokuwa wamefungwa katika gereza hilo

Ghafla mlipuko ulitokea katika gari ya Rodney ni baada ya kubonyeza button ya kifaa cha mawasiliano bila kujua kuwa ilikuwa ni button ya bomu lililokuwa limewekwa kwa siri na majasusi

Rodney alifariki papo hapo lakini kaka yake Donard alinusurika katika mlipuko huo akapata kusimulia yote yaliyotokea

Siku ya tukio hilo ilikuwa ni tarehe 13 Juni 1980, Walter Rodney alifariki kwa mipango ya binadamu akiwa na umri wa miaka 38

Serikali ya Guyana ilikana kuhusika na kifo cha Rodney ikasema kwamba huenda alikuwa anafanya majaribio ya bomu ili kutumia kufanya uhalifu kwa serikali iliyopo madarakani hata vyombo vya dola vilitoa ushirikiano dhaifu kesi hiyo ikashindwa kufanyiwa uchunguzi

Kelele zilipigwa sana na familia ya Rodney wakitaka serikali ya Guyana kuunda tume kuchunguza kifo cha Walter Rodney lakini miaka yote kelele hizo zilizopuuzwa bila ya kusikilizwa

Mwaka 2014 Rais wa Gunaya Donald Ramotar aliunda tume ya kuchunguza mauaji wa Walter Rodney ambapo majibu yalionesha kuwa Serikali ya Rais wa wakati huo Forbes Burnham ndio ilisuka mpango wa kifo cha Rodney

Walimtumia Jasusi wao wa Jeshi Gregory Smith na baada ya kutekeleza tukio hilo aliyoroshwa kwa siri akaenda kuishi French Guiana akatumia jina feki la Cyril Johnson ili asijulikane alifariki mwaka 2002 akiwa nchini humo

Baada ya ripoti ya tume ya uchunguzi wa kifo cha Rodney kusomwa serikali ya Guyana iliomba radhi na ikamtambua Walter Rodney kama shujaa wa Taifa

c2ec3c5a46b41bfc53f0fdf25a57ebc7 (1).jpg
 
Back
Top Bottom