Historia ya Qur'an

Mtibeli kama una majibu naomba tafadhali

Hilo eneo la Makka na Madina kwa karne hizo liligubikwa na ibada ya miungu zaidi ya 360 ambayo iliwekwa hapo Alkaaba.
Huyo Allah mwenyewe kwa zama hizo alikuwa na watoto watatu.

Muhammad yeye kutokana na uswahaba wake na Wakristo akiwemo huyo Waraqa ndiye alibadili mwelekeo wa hayo madudw.

Ila hakukuwa na Uislamu kabla ya MUHAMMAD
 
Mimi sioni kama kuna haja ya muda huu kujudge kuhusu maswala ya kiimani katika upande huu wa kidini.!
Kila mtu abaki na dini yake au Aamini anachokiamini.

1)Mtume Muhammad S.A.W kupewa utume akiwa na miaka 40 ilikua ni hekma aliyoitumia Mwenyezi Mungu.kwani kumpa katika umri huo wa miaka 40 kikawaida hata akili ya mtu inakuwa imekomaa kisawasawa na kutambulika ni mtu mzima na mpembuzi wa mambo.
Pia katika swala ilo la kiimani yalitokea mengi hivyo ilihitaji mtu ambae atakua tayari ni matured.! Na kuabudu ukisoma historia katika SIRA Muhammad S.A.W hakuwa akijihusisha na ibada yoyote iliyokua ikiendelea kipindi kile(ibada kuu-kuabudu masanamu,moto,jua,mwezi,wanyama nk) vitu ambavyo hata wewe ndugu yangu sio rahisi kukubadili kuviabudu ambayo vingine mwanadamu mwenyewe alishiriki kuvitengeneza.
Hivyo Muhammad S.A.W mara nyingi alikua akijitenga na kuwa mwenyewe katika sehemu pweke.
2) Mungu wake alikua Allah
03)swala la kibla lilikuja baada ya mtume kukakabidhiwa swala ambazo leo waislam tunaziswali kutwa mara 5 na katika historia ya Kibla hivyo kipindi hiko yeye hakuwa na Kibla
04) hakuwa na msikiti(elewa jibu no 1 na no 3)


05)hakuwa na utaratibu kabla hajapewa kitabu (Quran)
06)hakuwa akifunga Ramadhan kabla hajapewa kitabu (Quran)
07)hakuzuru Kaabah kabla hajapewa kitabu (Quran) na unaposema kulikua na midoli ama lah.? Unamamisha nini masanamu au.?
Kama ni masanamu yalikuwepo kabla ujinga ukiwa unatawala sana katika eneo lile kabla Muhammad S.A.W hajapewa Utume.!

Nawasilisha
 
Wewe unaongea kutokana na uelewa wako jinsi ulivyo.!
Katika mafundisho ya Dini ya kiislam.
Uislam upo toka Enzi nabii Adam anaumbwa na ndio nabii wa kwanza katika historia ya manabii wa kiislam.
Tunapoweka mezani nadharia ya uumbwaji wa binadamu chanzo chake kikiwa ni Kuumbwa na Mungu basi sisi Waislam tunaamini kuwa Adam ndio chanzo cha sisi wote tuliomo ulimwenguni.
Uislam upo tangu Kipindi cha Adam na Hawa. Na manabii/mitume wengi walikuja kuutangaza Uislam kabla ya Muhammad.
Muhammad yeye ndio Mtume wa mwisho na hakuna mwingine baadae yake yeye.!
Sisi waislam ndio tunaamini ivyo.
Wewe icho ulichoeleza ni mtazamo wako...
 

Allah hakuwa na watoto,na wala hatawahi kuja kuwa nao.hajazaa wala hajazaliwa na wala hakuna anaefanana nae.

Chanzo (Quran Surah Tul al Ikhlas)
 
alimjuaje huyo allah kabla ya kuelezewa na korani
03)swala la kibla lilikuja baada ya mtume kukakabidhiwa swala ambazo leo waislam tunaziswali kutwa mara 5 na katika historia ya Kibla hivyo kipindi hiko yeye hakuwa na Kibla
04) hakuwa na msikiti(elewa jibu no 1 na no 3)
alikuwa anaswali wapi
Mkuu kwanini hutaki kukiri kuwa kabla ya Mohamad na korani yake hakujawahi kuwa na uislam
tupe pia historia ya uislam
 
Nimeipenda hii
 
Huna unalolojua na hii inaongesha huna elimu
 
Sahihi
 
HISTORIA YA QUR'AN.

Sehemu ya Pili(2).

Katika Sehemu ya Pili ya Historia ya Qur'an tutaangalia Sura zilizoshuka Makka na Madina Kama ifuatavyo.... πŸ‘‡

SURA ZA MAKKA NA MADINA

Kutokana na historia ya kushuka kwake sura za Qur-an zimegawanywa katika makundi mawili - sura za Makka na sura za Madina.

Sura za Makka ni zile zilizomshukia Mtume (s.a.w) katika kipindi cha Utume cha Makka kilichodumu kwa miaka 13. Maudhui ya sura za Makka kwa kiwango kikubwa yamejikita katika kujenga imani za watu kwa kutoa hoja madhubuti zilizozingatia mazingira ya wakazi wa Makka wa kipindi hicho. Muundo wa sura za Makka ni ule wa kishairi. Nyingi ya sura za Makka zimeundwa na aya fupi zenye kufikisha ujumbe moja kwa moja kwa mtindo wa kishairi uliozingatia mazingira ya watu wa Makka wa wakati ule.

Katika siku za mwanzo za kushuka kwa Qur-an, watu wa Makka walidhania kuwa Qur-an ni mashairi aliyotunga Muhammad (s.a.w), lakini baada ya kupitia aya zake kwa makini, kama alivyofanya bingwa wa washairi wa wakati huo, Labiid bin Rabiah, na baada ya kushindwa kutoa angalau sura moja mithili ya sura ya Qur-an, kimaudhui na kimuundo, ilidhihiri wazi kuwa Qur-an si mashairi bali ni Wahy kutoka kwa Allah (s.w).

Sura za Madina ni zile zilizomshukia Mtume (s.a.w) baada ya kuhamia Madina katika kipindi cha pili cha Utume wake kilichodumu kwa miaka 10.

Maudhui ya sura za Madinah yamejikita kwenye kuunda na kuendesha Dola ya Kiislamu. Nyingi ya sura za Madina zina aya ndefu zenye kufafanua mambo kwa uwazi ili kuwawezesha Waislamu kutekeleza wajibu wao katika kusimamisha na kuhami dola ya Kiislamu. Pia aya nyingi za Madina zimeshehenezwa na maamrisho na makatazo mbali mbali ili kuunda jamii imara itakayoweza kusimamisha Ukhalifa katika ardhi.

Inaendelea, InshaaAllah

Allah Ni Mjuzi Zaidi.
 
Nashukuru kinachoniudhi wamejikita kwenye dhihaka sio kujifunza
 
Kabla ya kushushiwa quran muhamad alikua anamuabudu Mungu kwa taratibu zipi kumbuka taratibu zote za kusali za uislamu zimetoka na quran aliyoshushiwa
Hapana Ila nitakupa maele
Walikuwa wana

036.Je, Uislamu ulikuwepo kabla Mtume Muhammad s.a.w?

Naam, ulikuwepo kabla,Uislamu ndiyo Msingi ambao kila mteule wa Mungu Mwenyezi alikuwa akiwahubiria watu wake,kila Zama ilikuwa Ni juu ya watu kutakiwa wasilimu,
Ukisoma hapa utaona Quran.com/4/163 quran.com/42/13

Sasa Soma hapa

127. Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi.



128. Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.



129. Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.



130. Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema.



131. Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote.



132. Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu.



133. Je! Mlikuwapo yalipo mfikia Yaaqub mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is- hak, Mungu Mmoja tu, na sisi tunasilimu kwake.



134. Hao ni watu walio kwisha pita. Watapata waliyo yachuma, nanyi mtapata mtakayo yachuma; wala hamtaulizwa nyinyi waliyo kuwa wakiyafanya wao.



135. Na wakasema: Kuweni Mayahudi au Wakristo ndio mtaongoka. Sema: Bali tunashika mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa katika washirikina.



136. Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake.



137. Basi wakiamini kama mnavyo amini nyinyi, itakuwa kweli wameongoka. Na wakikengeuka basi wao wamo katika upinzani tu. Na Mwenyezi Mungu atakutosheni kukukingeni na shari yao, na Yeye ndiye Msikizi, Mjuzi.



138. Huko ndiko kupaka rangi kwa Mwenyezi Mungu, na nani aliye mbora wa kupaka rangi kuliko Mwenyezi Mungu? Na sisi ni wenye kumuabudu Yeye tu.



139. Sema: Mnahojiana nasi juu ya Mwenyezi Mungu, naye ni Mola wetu Mlezi na Mola wenu Mlezi, na sisi tuna vitendo vyetu na nyinyi mna vitendo vyenu? Nasi tunamsafia Yeye tu.



140. Au mnasema kuwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zao walikuwa Mayahudi au Wakristo? Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu? Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliye ficha ushahidi alio nao utokao kwa Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na hayo myafanyayo.



141. Hao ni watu walio kwisha pita. Wao watapata waliyo yachuma, na nyinyi mt apata mliyo yachuma, wala hamtaulizwa nyinyi yale waliyo kuwa wakifanya wao.

Quran 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…