Historia ya Qur'an

Historia ya Qur'an

Neno Uislamu ni la asili ya Kiarabu lenye maana ya kutii au kusalimisha matakwa ya mtu kwa Mwenyezi Mungu wa kweli wa pekee, ajulikanaye kwa Kiarabu kama “Allah”.

Mtu ambaye amesalimisha matakwa yake kwa Mwenyezi Mungu (Allah) huuitwa “Mwislamu”.

Dini ya Kiislamu haikupewa jina kutokana na jina mtu au watu, wala halikuamuliwa na kizazi chochote cha wanadamu kama vile Ukristo ambao ulipewa jina kutokana na “Yesu Kristo”, Ubudha unatokana na jina la Gautama Buddha, Kunfushian, unatokana na Confucius, Umaksi ulipewa jina la Karl Marx; Uyahudi unatokana na jina la kabila la Yuda na Ubaniani (Uhindu) unatokana na jina la Hindu.

Uislamu (kutii amri za Mwenyezi Mungu) ni dini aliyopewa Adam, mtu wa kwanza na mtume wa kwanza wa Mwenyezi Mungu, na Uislamu ndio dini ya mitume wote walio tumwa na Mwenyezi Mungu kwa wanadamu. Kwa kuongezea, jina la Uislamu lilichaguliwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe na limetajwa wazi wazi katika kitabu cha mwisho cha Allah (Quran).

Allah alimfunulia mwanadamu katika kitabu cha mwisho alicho mfunulia Mwanadamu. Katika ufunuo wa mwisho, uitwao kwa Kiarabu Al-Quran Allah ameeleza yafuatayo:

- “… Leo Nime kukamilishieni Dini yenu, na kukutimizieni neema Yangu, na Nime kupendeleeni Uislamu uwe Dini yenu…” [Quran 5:3]

“Na anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haita kubaliwa kwake…”

[Quran 3:83]

Kwa hiyo, Uislamu haudai kuwa ni dini mpya iliyoletwa Arabuni na Mtume Muhammad katika karne ya saba, lakini Uislamu ni mwendelezo wa sehemu ya mwisho ya dini ya Allah, kama ilivyofunuliwa toka mwanzo kwa Adam na mitume waliomfuatia.
yaani kwa kifupi hata "allah" mwenyewe ameanza kujulikana 500 years baada ya Yesu kupaa. kabla ya hapo alikuwepo Mungu wa Israel tu ndiye wa kweli, na miungu mingine miiingi duniani kote. sasa mood kuja na story zake za kupotosha Biblia, amewaharibu sana na siku zote huwa hamna hoja.
 
Unataka kuniambia wayahudi wakimjua Mungu kwa jina la Yesu ?
 
036.Je, Uislamu ulikuwepo kabla Mtume Muhammad s.a.w?

Naam, ulikuwepo kabla,Uislamu ndiyo Msingi ambao kila mteule wa Mungu Mwenyezi alikuwa akiwahubiria watu wake,kila Zama ilikuwa Ni juu ya watu kutakiwa wasilimu,
Ukisoma hapa utaona Quran.com/4/163 quran.com/42/13

Sasa Soma hapa

127. Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi.

128. Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.

129. Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

130. Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema.

131. Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote.

132. Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu.

133. Je! Mlikuwapo yalipo mfikia Yaaqub mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is- hak, Mungu Mmoja tu, na sisi tunasilimu kwake.

134. Hao ni watu walio kwisha pita. Watapata waliyo yachuma, nanyi mtapata mtakayo yachuma; wala hamtaulizwa nyinyi waliyo kuwa wakiyafanya wao.

135. Na wakasema: Kuweni Mayahudi au Wakristo ndio mtaongoka. Sema: Bali tunashika mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa katika washirikina.

136. Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake.

137. Basi wakiamini kama mnavyo amini nyinyi, itakuwa kweli wameongoka. Na wakikengeuka basi wao wamo katika upinzani tu. Na Mwenyezi Mungu atakutosheni kukukingeni na shari yao, na Yeye ndiye Msikizi, Mjuzi.

138. Huko ndiko kupaka rangi kwa Mwenyezi Mungu, na nani aliye mbora wa kupaka rangi kuliko Mwenyezi Mungu? Na sisi ni wenye kumuabudu Yeye tu.

139. Sema: Mnahojiana nasi juu ya Mwenyezi Mungu, naye ni Mola wetu Mlezi na Mola wenu Mlezi, na sisi tuna vitendo vyetu na nyinyi mna vitendo vyenu? Nasi tunamsafia Yeye tu.

140. Au mnasema kuwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zao walikuwa Mayahudi au Wakristo? Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu? Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliye ficha ushahidi alio nao utokao kwa Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na hayo myafanyayo.

141. Hao ni watu walio kwisha pita. Wao watapata waliyo yachuma, na nyinyi mt apata mliyo yachuma, wala hamtaulizwa nyinyi yale waliyo kuwa wakifanya wao.

Qur'an 2
Sasa kama uislamu ulikuwapo kabla Quran ya nini tena?
 
yaani kwa kifupi hata "allah" mwenyewe ameanza kujulikana 500 years baada ya Yesu kupaa. kabla ya hapo alikuwepo Mungu wa Israel tu ndiye wa kweli, na miungu mingine miiingi duniani kote. sasa mood kuja na story zake za kupotosha Biblia, amewaharibu sana na siku zote huwa hamna hoja.

Ukifungua "Al-Kitaab Al-Muqadis(الكتاب المقدس)' (yaani Kitabu Kitakatifu), bibilia itumiwayo na wakristo wanaozungumza lugha ya Kiarabu neno Allah limetumiwa kila penye neno Mungu au Yehova.
 
Ukifungua "Al-Kitaab Al-Muqadis(الكتاب المقدس)' (yaani Kitabu Kitakatifu), bibilia hitumiwayo na wakristo wanaozungumza lugha ya Kiarabu neno Allah limetumiwa kila penye neno Mungu au Yehova.
hiyo ni tafsiri tu, ila kiukweli allah sio Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo, ni kamungu kengine kabisa. na hicho ndicho kinachowafanya msimwamini Mungu wa kweli, ati kwasababu kwa kiarabu neno "Mungu" ni allah basi ndio huyo ambaye sote tunamwabudu. kama kwa kiarabu neno allah ni Mungu, mbona India kuna miungu zaidi ya 10,000 kuna mungu ng'ombe, nyani n.k, kwahiyo ni sawa na kusema india kuna allah zaidi ya 10,000 unafikiri ndio maana yake?

kwenye Biblia ya kiarabu walikuwa wanajaribu kuwatafsiria tu waarabu pengine wataelewa. ila bado ni wagumu kuelewa hadi leo.

pia,mfano Yesu ninyi mnaita isa bin mariam, ukitaja jina la issa mapepo yanasherehekea, ila ukitaja Jina la Yesu, mapepo yakatimka, hujiulizi kwanini? ukienda kuswali kesho kaseme kwa nguvu YESU uone kitakachotokea. utaleta mrejesho hapa. hadi swala itavurugika. ila ukitaja ISSA, shwari tu. hapo ndio mjue kitabu chenu kimejaa maneno yasiyo ya Mungu wa kweli.
 
sasa tuambie jina la Mungu ni lipi ?? ni Yesu ??
 
HISTORIA YA QUR'AN.

SEHEMU YA KWANZA 01.

Asalaam Alaykum Warahmatullah Wabaarakatuh, Kila Sifa njema anastahiri Mwenyezi Mungu Mola mlezi wa Walimwengu wote, na Sifa njema zimuendee Kipenzi chetu Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم na Radhi za Allah ziwashukie Maswahaba zake na wema waliotangulia.

Moja kwa moja niingie Katika DARASA Jipya la HISTORIA YA QUR'AN, historia ambayo imebeba mambo mengi mno yakujifunza. InshaaAllah, Fuatana na Mimi kuijuwa Historia ya Qur'an... 👇

Nini Maana ya Qur'an.

👉 Qur-an ni wahy (ufunuo) kwa Mtume Muhammad (s.a.w) kutoka kwa Allah (s.w) kupitia kwa Malaika Jibril (a.s). Au Ni Maneno ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم kupitia Malaika Jibril عليه سلم.

HISTORIA yake...

Qur-an ilianza kumshukia Mtume Muhammad (s.a.w) mwaka 610 A.D. alipokuwa na umri wa miaka 40. Mtume Muhammad (s.a.w) alianza kushushiwa Qur-an akiwa pangoni katika mlima Hira (Jabal Hira) katika usiku wa mwezi wa Ramadhani kama Qur-an yenyewe inavyotufahamisha:

👉 "Ni mwezi wa Ramadhani ambamo imeteremshwa hii Qur-an" (2:185)

👉"Hakika Tumeiteremsha (Qur-an) katika Laylatul-Qadr (usiku wenye hishima kubwa). Na jambo gani litakujulisha (hata ukajua) ni nini huo usiku wenye hishima kubwa? Huo usiku wa hishima ni bora kuliko miezi elfu. Huteremka Malaika na roho (Jibriil) katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao kwa kila jambo. Ni amani (usiku) huo mpaka mapambazuko ya alfajiri." (9 7:1-5)

Tunajifunza kutokana na aya hizi kuwa mwezi wa Ramadhani umetukuzwa kutokana na Qur-an kuanza kushuka katika mwezi huu. Pamoja na funga kufaradhishwa kwa umma za Mitume wote wa Allah (s.w); kwa ummat Muhammad (s.a.w),funga imefaradhishwa iwe katika mwezi wa Ramadhani ili iwe ni pamoja na kusherehekea kushuka kwa Qur-an na kilele cha sherehe hii kinakuwa katika usiku wa hishima (Laylatul-Qadr) ambamo Qur-an ilianza kushuka. Mtume (s.a.w) alikuwa akizidisha kusoma Qur-an katika mwezi huu na alikuwa akikaa Itiqaf katika kumi la mwisho la Ramadhani ili aweze kudiriki kilele cha sherehe. Usiku wenye hishima (Laylatul-Qadr) ulifichwa kwa Mtume (s.a.w) lakini alifunuliwa na Mola wake kuwa unapatikana katika kumi la mwisho la Ramadhani. Ni sunnah kwa Waislamu kuzidisha kusoma Qur-an katika mwezi mzima wa Ramadhani na kukaa Itiqaf katika kumi la mwisho, ili kushiriki kikamilifu katika sherehe ya kumbu kumbu ya kuanza kushuka Qur-an.

Historia ya kuanza kushuka Qur-an kwa Mtume Muhammad (s.a.w) kupitia kwa Malaika Jibril (a.s) inasimuliwa vyema katika Hadith ya bibi 'Aisha (r.a) ifuatayo:
Bibi 'Aisha (r.a) amesema:" Kilichoanza katika Wahyi wa Mtume (s.a.w) ni ndoto za kweli. Alikuwa Mtume (s.a.w) haoti chochote isipokuwa kilitokea kama alivyoota. Kisha akaona ni bora kujitenga. Akawa anakwenda Jabal Hira kujilinda na maovu. Basi alikuwa anakwenda Jabal Hira akifanya ibada masiku mengi na alichukua masurufu kwa ajili hiyo. Masurufu haya kila yalipokwisha alirudi tena kwa Bibi Khadija, aliyemtayarishia masurufu kama yale (ya kwanza) mpaka ikambainikia haki akiwa pangoni Hira. Basi akamjia Malaika (Jibril) humo pangoni akamuamrisha kusoma, Mtume (s.a.w) alijibu: "Sijui kusoma". Alinibana kwa nguvu mpaka nikahisi taabu. Kisha akaniachia na kuniamrisha tena kusoma na nikajibu: Sijui kusoma: Kisha akanibana tena kwa nguvu kwa mara ya pili mpaka nikahisi taabu. Kisha akaniachia na kuniamrisha tena kusoma. Nilijibu tena, "sijui kusoma". Akanikumbatia tena kwa nguvu kwa mara ya tatu mpaka nikahisi mashaka, kisha akaniachia na akasema:

👉 "Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba. Amemuumba mwanaadamu kwa pande la damu. Soma na Mola wako ni Karimu sana.Ambaye amefundisha kwa msaada wa kalamu.Amemfundisha mwanaadamu mambo aliyokuwa hayajui." (96:1-5)

Mtume wa Mwenyezi Mungu alirejea na Wahy huu, huku akitetemeka kwa khofu aliyokuwa nayo. Alikwenda kwa mkewe Khadijah na akamhadithia yale yote yaliyomtokea kisha akasema;

"Nakhofia kuwa kitu kinaweza kunitokea ". Khadijah alijibu: "Hapana! Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu hatakufedhehesha. Unakaa vizuri na kuwafanyia wema ndugu na jamaa zako, unawasaidia masikini na fukara, unawakirimu wageni na unawasaidia waliokabiliwa na matatizo. "Kisha Bibi Khadijah alimchukua Mtume (s.a.w) mpaka kwa bin-ami yake, Waraqa bin Naufal bin Asad bin Abdul Uzza, ambaye alikuwa Mkristo. Waraqa wakati huo alikuwa mzee sana na alikuwa hawezi kuona tena. Khadijah alimuambia Waraqa "Sikiliza hadithi ya mpwa wako, Ewe Bin-ami yangu" Waraqa aliuliza, "Ewe Mpwa wangu umeona nini?" Mtume wa Mwenyezi Mungu alimuhadithia habari yote kama alivyoona. Waraqa akasema: "Huyu ni yule mtunza siri (Malaika Jibril) ambaye Mwenyezi Mungu alimtuma kwa Mussa. Natamani ningelikuwa kijana na kuishi mpaka wakati huo watu wako watakapokukataa na kukufukuza." Mtume wa Mwenyezi Mungu akauliza: "Watanifukuza?" Waraqa akajibu kuwa watafanya hivyo na akasema, "Yeyote aliyekuja na kitu kama hicho ulichokuja nacho alifanyiwa uadui na watu wake, na ningejaaliwa kubakia hai mpaka siku hiyo watu wako watakapokufukuza, ningelikusaidia kwa hali na mali." Lakini baada ya muda mfupi Waraqa alifariki na Wahyi mwingine ulikawia kuja kwa kipindi kirefu. (Sahihi Bukhari)
Tunajifunza kutokana na Hadith kuwa kabla Mtume (s.a.w) hajaanza kushushiwa Qur-an kupitia kwa Malaika Jibril (a.s) alikuwa akipata Wahy kwa njia ya ndoto.
Qur-an yote kwa ujumla imehifadhiwa katika ubao mtukufu wa Allah (s.w) ulio katika Arshi yake kama tunavyofahamishwa katika Qur-an:

👉"Bali hii ni Qur-an tukufu iliyotolewa katika Lawhi Mmahfuudh (huo ubao uliohifadhiwa)." (85:21-22)

Kisha kutoka Lawhi Mmahfuudh Qur-an ilishushwa mpaka wingu wa kwanza. Kisha kutoka humo ikashushwa kidogo kidogo kwa Mtume (s.a.w) kupitia kwa Malaika Jibril (a.s) kwa kipindi chote cha Utume cha miaka 23.

👉"Kwa hakika hii (Qur-an) ni kauli (aliyokuja nayo) Mjumbe Mtukufu (Jibril), Mwenye nguvu na cheo cha hishima kwa Mwenyezi Mungu. (81:19-20)

Kama tunavyojifunza katika Hadith, aya za mwanzo kumshukia Mtume (s.a.w) ni aya tano za mwanzo za suratul-’Alaq. Aya zilizofuatia katika sura hii (96:6-19) zilishuka siku za baadaye.

Aya ya mwisho kumshukia Mtume (s.a.w) alipokuwa katika Hija ya kuaga (Hijjatul Wadaai) ni aya ya tatu ya suratul Maida (5:3) ambayo imeashiria mwisho wa wahy wa Qur-an katika sehemu ifuatayo:

👉 "Leo waliokufuru wamekata tamaa katika dini yenu, basi msiwaogope, bali niogopeni mimi. Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kukutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe dini yenu" Qur'an (5:3)

Pia tunajifunza kutokana na historia ya kushuka Qur-an kuwa sura ya kwanza kushuka nzima (ikiwa na aya zote) ni Suratul-Fatiha (Al-hamdu) na imekuwa ndio sura ya kwanza katika msahafu. Katika mtiririko wa kushuka suratul-Fatiha ni Wahy wa tano. Sura ya mwisho kushuka ikiwa nzima ni Suratun-Nasr, sura ya 114 katika utaratibu wa kushuka.

Inaendelea... InshaaAllah

Allah Ni Mjuzi Zaidi.
Quran imeshushwaje mwezi wa ramadhani wakati uislam ulianza baada ya kushushwa kwa Quran na Muhammad ndiye aliyekuwa muislam wa kwanza

Kama una aya inaosema kuwa manabii kabla ya Muhammad walikuwa na mwezi wa ramadhani onyesha hapo au reference yoyote kama ipo

Pia kwanini Allah ashushe hadithi ambazo zilikuwa tayar zipo kwenye biblia?
 
hiyo ni tafsiri tu, ila kiukweli allah sio Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo, ni kamungu kengine kabisa. na hicho ndicho kinachowafanya msimwamini Mungu wa kweli, ati kwasababu kwa kiarabu neno "Mungu" ni allah basi ndio huyo ambaye sote tunamwabudu. kama kwa kiarabu neno allah ni Mungu, mbona India kuna miungu zaidi ya 10,000 kuna mungu ng'ombe, nyani n.k, kwahiyo ni sawa na kusema india kuna allah zaidi ya 10,000 unafikiri ndio maana yake?

kwenye Biblia ya kiarabu walikuwa wanajaribu kuwatafsiria tu waarabu pengine wataelewa. ila bado ni wagumu kuelewa hadi leo.

pia,mfano Yesu ninyi mnaita isa bin mariam, ukitaja jina la issa mapepo yanasherehekea, ila ukitaja Jina la Yesu, mapepo yakatimka, hujiulizi kwanini? ukienda kuswali kesho kaseme kwa nguvu YESU uone kitakachotokea. utaleta mrejesho hapa. hadi swala itavurugika. ila ukitaja ISSA, shwari tu. hapo ndio mjue kitabu chenu kimejaa maneno yasiyo ya Mungu wa kweli.

View: https://www.youtube.com/watch?v=Tpmlk5P5TBo
 
Huyu jamaa anapotosha sana kwa kudokoa dokoa hadithi na kuzitafsiri kivyengine.
Kuhusu Kuja kwa maajuja nakuwekea hii usikilize vizuri huyo jamaa anapotosha sana hatari sana

View: https://www.youtube.com/watch?v=kF4kSOdcEA8

Mbona kinachosemwa ni kile kile anachosema Ustadhi Hamza, kwamba njia pekee ya kuwashinda Mahajuja Mahajuji ni kwa kupitia Issa bin Mariamu!

Hamza kapotosha wapi?
 
google huyo mhindi, kuna video yake walimchukua alipokuwa anakufa, alipiga kelele balaa, ilionyesha kama alikuwa anakuona anakoelekea, kwenye ziwa la moto na kiberiti, na ilikuwa too late for him, ameudanganya ulimwengu, there was no turning back, alikufa kwa mateso. laiti kama angeweza kurudi angewaambia, na hata angewaambia wala msingemwamini.
 
Ni wapi Mohammed aliweza kuandika Kwa mkono wake mwenyewe, toa ushahidi wa kueleweka.

Pia ni wapi Mohammed aliweza kusoma maandiko yaliyo andikwa , nje ya Qur'an, TOA ushahidi
 
Mbona kinachosemwa ni kile kile anachosema Ustadhi Hamza, kwamba njia pekee ya kuwashinda Mahajuja Mahajuji ni kwa kupitia Issa bin Mariamu!

Hamza kapotosha wapi?

Sikiliza vizuri au una lengo lako jengine hapo hapajasemwa njia ya kuwashinda Juja wa maajuja ni kupitia Issa bin mariam au kiengereza huelewi vizuri nikuwekee ya kiswahili ??
 
google huyo mhindi, kuna video yake walimchukua alipokuwa anakufa, alipiga kelele balaa, ilionyesha kama alikuwa anakuona anakoelekea, kwenye ziwa la moto na kiberiti, na ilikuwa too late for him, ameudanganya ulimwengu, there was no turning back, alikufa kwa mateso. laiti kama angeweza kurudi angewaambia, na hata angewaambia wala msingemwamini.

Alikuwa akiwasilimisha wagalatia kitandani ndio video ninayoiyona , hiyo video yako labda uliangalia wewe na Roho mtakatifu wako
 
Back
Top Bottom