Historia ya Qur'an

Historia ya Qur'an

Wakati wa Yesu kulikuwa na makundi kadhaa ya Wayahudi.
1. Wafarisayo
2. Sedukayo
3. Essenes
4. Zealots
5. wakristo (Wafuasi wa Yesu)

Liwe kundi lolote hata wayahudi wa Bongo , mimi naongelea kabla kuzaliwa Yesu , Mungu wakimjua kwa jina lipi ?? Yesu ??
 
google huyo mhindi, kuna video yake walimchukua alipokuwa anakufa, alipiga kelele balaa, ilionyesha kama alikuwa anakuona anakoelekea, kwenye ziwa la moto na kiberiti, na ilikuwa too late for him, ameudanganya ulimwengu, there was no turning back, alikufa kwa mateso. laiti kama angeweza kurudi angewaambia, na hata angewaambia wala msingemwamini.
Hiyo video uliiona wewe na Roho Mtakatifu wako,

kuna video yupo kitandani na bado akisilimisha wagalatia
 

Yaani aya hiyo ndiyo sawa na aya hii ??

Na pale Mwenyezi Mungu atakapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu? (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwisha yajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi mkubwa wa yaliyo fichikana.​



LAZIMA UTAKUWA UNAUMWA ; UNAHITAJI PSYCHOLOGIST
 
Usijadili kilokole.
Jadili kwa Hoja.
Historia inaonyesha Hapo Makka Allah alikuwa anaabudiwa kama Mungu mkuu Chief God kabla hata ya huyo Muhamad kuwako. Na simulizi zinaonyesha waumini waliamini alikuwa na watoto watatu.

Kabla ya mtume kuwa mtume alikuwa anaabudu dini gani?
Watoto wa Allah (mungu wa Abdallah) waliitwa Al Lat, Manat na Al Uzza kutokana na simulizi za imani kabla ya uislam. Quran inakataza kuamini hii nadharia katika Surah 53. Ila nastaajabu kwanini Al Lat, Manat na Al Uzza bado ni sehemu ya hija takatifu.
 
Yaani aya hiyo ndiyo sawa na aya hii ??

Na pale Mwenyezi Mungu atakapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu? (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwisha yajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi mkubwa wa yaliyo fichikana.​



LAZIMA UTAKUWA UNAUMWA ; UNAHITAJI PSYCHOLOGIST
huu ndio uongo mkubwa sana mood aliuleta, na ndio sababu mojawapo zinamfanya anaungua moto kuzimu sasaivi. Yesu Kristo sio Issa bin maryam, ni vitu viwili tofauti. hata ukitaja majina haya mawili mashetani yanayajua, hata majini yanatambua, unalijuahilo na unajitoa tu ufahamu.
 

"Aliyeniona mimi amemwona baba."

Wacha tuangalie muktadha:

“Filipo akamwambia, Bwana, tuonyeshe Baba, nasi yatutosha. Baba; nawe wasemaje basi, Utuonyeshe Baba?

Yohana 14:8-9

Filipo alitaka kumwona Mungu kwa macho yake mwenyewe, lakini hii haiwezekani kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kufanya hivyo. Biblia inasema:

"Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote,"

Yohana 1:18

"Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote,"

1 Yohana 4:12

"Na Baba mwenyewe aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamjaiona."

Yohana 5:37

Lakini walikuwa wakisikiliza sauti ya Yesu na kumtazama akiwa amesimama mbele yao! Yesu alikuwa anatuambia tu kwamba matendo yake mwenyewe na miujiza inapaswa kuwa uthibitisho wa kutosha wa kuwepo kwa Mungu bila Mungu kushuka kimwili na kujiruhusu kuonekana kila wakati mtu ana shaka. Hii ni sawa na kwa mfano:

1)Yohana 8:19: "Wakamwambia, Baba yako yuko wapi? Yesu akajibu, Ninyi hamnijui mimi, wala Baba yangu; kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu."

2)Yohana 12:44 "Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi, bali yeye aliyenipeleka."

3)Yohana 15:23 "Yeye anichukiaye mimi anamchukia na Baba yangu."

4)Mathayo 10:40-41 "Awapokeaye ninyi, anipokea mimi (Yesu), naye anipokeaye mimi, anampokea yeye aliyenituma. Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki."

5) Waamuzi 13:20-22 inasema: “Ikawa, huo mwali wa moto ulipopaa juu mbinguni, kutoka katika madhabahu, ndipo malaika wa BWANA akapanda katika mwali wa moto wa madhabahu, Manoa na mkewe wakatazama. wakaanguka kifudifudi, lakini malaika wa BWANA hakumtokea tena Manoa na mkewe.” Ndipo Manoa akajua ya kuwa yeye ni malaika wa BWANA.” Manoa akamwambia mkewe, Hakika tutakufa, kwa sababu tumemwona Mungu."

Ikiwa tunataka kusisitiza kwamba wakati Filipo alipomwona Yesu (AS), alikuwa amemwona Mungu "Baba" kimwili kwa sababu Yesu "ndiye" Baba na wote wawili ni "Utatu," na Yesu ni "mwili" wa Mungu, basi. hii itatulazimisha kuhitimisha kuwa Yohana 1:18, 1 Yoh 4:12, Yoh 5:37..nk. yote ni uongo.


Je, Filipo ndiye pekee ambaye "alimwona baba"? Hebu tusome:

"Si kwamba mtu amemwona Baba, ila yeye atokaye kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba."

Yohana 6:46

Ni nani huyu "aliye wa Mungu" na amemwona Baba unayemwuliza? Hebu tuulize tena Biblia:

“Yeye aliye wa Mungu husikia maneno ya Mungu;

Yohana 8:47.

Na

"Mpenzi, usifuate uovu, bali wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu; bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu."

3 Yohana 1:11.

Je, watu wote ambao wamefanya mema pia wamemwona Mungu kimwili?

"Hakuna uoni unaoweza kumshika, lakini uwezo wake uko juu ya uoni wote. Yeye ni Mpole, Mjuzi wa kila kitu."

Qur'ani Tukufu, Al-Anaam(6):103

"Na Musa alipoufikia wakati na mahala tulipo kuwawekea, na Mola wake Mlezi akamwambia, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nionyeshe ili nikutazame. [Mwenyezi Mungu] akasema: Huwezi kuniona, lakini tazama mlima, ukisimama mahali pake, basi utaniona. Basi Mola wake Mlezi alipoudhihirishia mlima akauvunjavunja na Musa akaanguka na kupoteza fahamu, alipozinduka akasema: Umetakasika! Mimi nimetubu kwako na mimi ni wa kwanza wa Waumini.

Qur'ani Tukufu, Al-Aaraf(7):143
 
Watoto wa Allah (mungu wa Abdallah) waliitwa Al Lat, Manat na Al Uzza kutokana na simulizi za imani kabla ya uislam. Quran inakataza kuamini hii nadharia katika Surah 53. Ila nastaajabu kwanini Al Lat, Manat na Al Uzza bado ni sehemu ya hija takatifu.


Katika Kitabu cha Ezekieli (Sura ya 40-47), anatuambia kuhusu safari aliyofanyiwa na Bwana (au Malaika) katika maono yake...kutoka kwa maelezo yake hadi safari hii tunaweza kuhitimisha mambo yafuatayo. ...:

1) Mahali na Wakati:

Ezekieli:

40.1 Katika mwaka wa ishirini na tano wa kuhamishwa kwetu, mwanzoni mwa mwaka, siku ya kumi ya mwezi, mwaka wa kumi na nne baada ya mji huo kupigwa, siku iyo hiyo mkono wa BWANA ulikuwa juu ya yangu, na kunileta huko.

40:2 Katika maono ya Mungu akanileta mpaka nchi ya Israeli, akaniweka juu ya mlima mrefu sana, ambao juu yake palikuwa kama ukuta wa mji upande wa kusini.

Katika mistari hii 2 Ezekieli anatambua muda wa safari hii (mwanzoni mwa mwaka, siku ya kumi ya mwezi).. Kwa kweli sina uhakika wa hali ya hewa hii ni Tafsiri SAHIHI ya mstari huo (au ya kile ambacho Ezekieli hakika ilimaanisha) au Hapana...lakini Wayahudi walikuwa wakitumia miezi ya Lunar kama Waislamu..na inajulikana kuwa siku ya 10 ya mwezi wa MWISHO ni Eid Al Adha wakati wa hija ya Makka kila mwaka...Chochote ninachokipata. kufanana kati ya tarehe 2 (Eid Al Adha na Safari ya Ezekiel) ..Hadithi iliyobaki itaweka wazi ingawa..!

lakini Vipi kuhusu MAHALI?..Vema..hebu tusome:

“Mungu akanileta mpaka nchi ya Israeli, akaniweka juu ya mlima mrefu sana, ambao juu yake palikuwa kama umbo la mji upande wa kusini.”

Mji uko KUSINI kwa Ardhi ya Israeli, Ambapo umezungukwa na Milima...Mji huu ni nini?...Bila shaka Meka iko tu kusini mwa Ardhi ya Israeli na imezungukwa na Milima..Bado.. Ushahidi zaidi unafuatwa katika maelezo yake mahali hapo..!

2) Sura ya Mahali hapo:

Ezekieli anatueleza sura ya mahali hapo katika Sura ya 40-43..:

42:15 Naye alipokwisha kuipima nyumba ya ndani, akanileta nje mpaka lango lililoelekea upande wa mashariki, akalipima pande zote.

42:16 Akaupima upande wa mashariki kwa mwanzi wa kupimia, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia pande zote.

42:17 Akaupima upande wa kaskazini, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia pande zote.

42:18 Akaupima upande wa kusini, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia.

42:19 Akazunguka upande wa magharibi, akapima mianzi mia tano kwa mwanzi wa kupimia.

42.20 Akaupima pande zote nne; ilikuwa na ukuta pande zote, urefu wake mianzi mia tano, na upana wake mia tano, ili kutenganisha patakatifu na mahali patakatifu.

Kulingana na sura hii, eneo hili lina umbo la mraba

3) Nyumba Tukufu: (Al Ka'aba):

41.4 Akaupima urefu wake, dhiraa ishirini; na upana, dhiraa ishirini, mbele ya hekalu; akaniambia, Hapa ndipo patakatifu pa patakatifu.

Kwa mujibu wa SURA hii ya MAHALI PATAKATIFU, nayo ni ya mraba..na inafahamika kuwa Al Ka'aba pia ni jengo la 4square...Je, kuna nyumba nyingine takatifu yenye sura sawa katika Ukristo au Uyahudi?..!

Zaidi zaidi, Ezekiel anatabiri upanuzi wa Nyumba ..Tusome:

41.7 Palikuwa na upana, na mzunguko wa pande zote, kuelekea juu hata vyumba vya mbavuni; kwa maana upepo wa kuizunguka nyumba uliendelea kwenda juu kuizunguka nyumba; kwa hiyo upana wa nyumba ukazidi kwenda juu, na hivyo ndivyo chumba cha chini hadi cha juu kabisa kwa katikati.
 
Wewe unaongea kutokana na uelewa wako jinsi ulivyo.!
Katika mafundisho ya Dini ya kiislam.
Uislam upo toka Enzi nabii Adam anaumbwa na ndio nabii wa kwanza katika historia ya manabii wa kiislam.
Tunapoweka mezani nadharia ya uumbwaji wa binadamu chanzo chake kikiwa ni Kuumbwa na Mungu basi sisi Waislam tunaamini kuwa Adam ndio chanzo cha sisi wote tuliomo ulimwenguni.
Uislam upo tangu Kipindi cha Adam na Hawa. Na manabii/mitume wengi walikuja kuutangaza Uislam kabla ya Muhammad.
Muhammad yeye ndio Mtume wa mwisho na hakuna mwingine baadae yake yeye.!
Sisi waislam ndio tunaamini ivyo.
Wewe icho ulichoeleza ni mtazamo wako...
Circular reasoning fallacy
 
Njoo uthibitishe ya kuwa Biblia ilikuwepo.
Ukisoma huo mstari hapo chini utaona yesu anafungua kitabu cha isaya ambacho kipo kwenye biblia na ndo mara ya kuanza kuanza huduma yake maana yake biblia ilikuwepo na dini ya kiyahudi walikua wanaitumia na mpaka leo wanaitumia

Luka 4:16-20
16 Baadaye Yesu akaenda Nazareti, mahali alipokulia. Siku ya sabato alikwenda katika sinagogi kama kawaida yake. Akasimama ili asome Maandiko. 17 Akapewa kitabu cha nabii Isaya, akakifungua mahali palipoandikwa: 18-19 “Roho wa Bwana yu juu yangu. Amenichagua kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatan gazia wafungwa kuwa wako huru, kuwaambia vipofu kuwa wanaweza kuona tena; na kuwaweka huru wanaoonewa, na nitangaze mwaka ambao Bwana atawabariki watu wake.”20 Akakifunga kitabu, akamrud ishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.
 
Propaganda hizo mkuu. Waislam hujipa moyo
036.Je, Uislamu ulikuwepo kabla Mtume Muhammad s.a.w?

Naam, ulikuwepo kabla,Uislamu ndiyo Msingi ambao kila mteule wa Mungu Mwenyezi alikuwa akiwahubiria watu wake,kila Zama ilikuwa Ni juu ya watu kutakiwa wasilimu,
Ukisoma hapa utaona Quran.com/4/163 quran.com/42/13

Sasa Soma hapa

127. Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi.



128. Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.



129. Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.



130. Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema.



131. Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote.



132. Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu.



133. Je! Mlikuwapo yalipo mfikia Yaaqub mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is- hak, Mungu Mmoja tu, na sisi tunasilimu kwake.



134. Hao ni watu walio kwisha pita. Watapata waliyo yachuma, nanyi mtapata mtakayo yachuma; wala hamtaulizwa nyinyi waliyo kuwa wakiyafanya wao.



135. Na wakasema: Kuweni Mayahudi au Wakristo ndio mtaongoka. Sema: Bali tunashika mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa katika washirikina.



136. Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake.



137. Basi wakiamini kama mnavyo amini nyinyi, itakuwa kweli wameongoka. Na wakikengeuka basi wao wamo katika upinzani tu. Na Mwenyezi Mungu atakutosheni kukukingeni na shari yao, na Yeye ndiye Msikizi, Mjuzi.



138. Huko ndiko kupaka rangi kwa Mwenyezi Mungu, na nani aliye mbora wa kupaka rangi kuliko Mwenyezi Mungu? Na sisi ni wenye kumuabudu Yeye tu.



139. Sema: Mnahojiana nasi juu ya Mwenyezi Mungu, naye ni Mola wetu Mlezi na Mola wenu Mlezi, na sisi tuna vitendo vyetu na nyinyi mna vitendo vyenu? Nasi tunamsafia Yeye tu.



140. Au mnasema kuwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zao walikuwa Mayahudi au Wakristo? Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu? Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliye ficha ushahidi alio nao utokao kwa Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na hayo myafanyayo.



141. Hao ni watu walio kwisha pita. Wao watapata waliyo yachuma, na nyinyi mt apata mliyo yachuma, wala hamtaulizwa nyinyi yale waliyo kuwa wakifanya wao.



Qur'an 2
 
Ukisoma huo mstari hapo chini utaona yesu anafungua kitabu cha isaya ambacho kipo kwenye biblia na ndo mara ya kuanza kuanza huduma yake maana yake biblia ilikuwepo na dini ya kiyahudi walikua wanaitumia na mpaka leo wanaitumia

Luka 4:16-20
16 Baadaye Yesu akaenda Nazareti, mahali alipokulia. Siku ya sabato alikwenda katika sinagogi kama kawaida yake. Akasimama ili asome Maandiko. 17 Akapewa kitabu cha nabii Isaya, akakifungua mahali palipoandikwa: 18-19 “Roho wa Bwana yu juu yangu. Amenichagua kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatan gazia wafungwa kuwa wako huru, kuwaambia vipofu kuwa wanaweza kuona tena; na kuwaweka huru wanaoonewa, na nitangaze mwaka ambao Bwana atawabariki watu wake.”20 Akakifunga kitabu, akamrud ishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.

Hiyo ni biblia ipi unayoongelea , KJV, RSV , Douay , NIV , Mormon bible au ipi kati ya maelfu ya biblia tofauti ??
 
Back
Top Bottom