Historia ya Qur'an

Historia ya Qur'an

036.Je, Uislamu ulikuwepo kabla Mtume Muhammad s.a.w?

Naam, ulikuwepo kabla,Uislamu ndiyo Msingi ambao kila mteule wa Mungu Mwenyezi alikuwa akiwahubiria watu wake,kila Zama ilikuwa Ni juu ya watu kutakiwa wasilimu,
Ukisoma hapa utaona Quran.com/4/163 quran.com/42/13

Sasa Soma hapa

127. Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi.



128. Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.



129. Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.



130. Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema.



131. Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote.



132. Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu.



133. Je! Mlikuwapo yalipo mfikia Yaaqub mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is- hak, Mungu Mmoja tu, na sisi tunasilimu kwake.



134. Hao ni watu walio kwisha pita. Watapata waliyo yachuma, nanyi mtapata mtakayo yachuma; wala hamtaulizwa nyinyi waliyo kuwa wakiyafanya wao.



135. Na wakasema: Kuweni Mayahudi au Wakristo ndio mtaongoka. Sema: Bali tunashika mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa katika washirikina.



136. Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake.



137. Basi wakiamini kama mnavyo amini nyinyi, itakuwa kweli wameongoka. Na wakikengeuka basi wao wamo katika upinzani tu. Na Mwenyezi Mungu atakutosheni kukukingeni na shari yao, na Yeye ndiye Msikizi, Mjuzi.



138. Huko ndiko kupaka rangi kwa Mwenyezi Mungu, na nani aliye mbora wa kupaka rangi kuliko Mwenyezi Mungu? Na sisi ni wenye kumuabudu Yeye tu.



139. Sema: Mnahojiana nasi juu ya Mwenyezi Mungu, naye ni Mola wetu Mlezi na Mola wenu Mlezi, na sisi tuna vitendo vyetu na nyinyi mna vitendo vyenu? Nasi tunamsafia Yeye tu.



140. Au mnasema kuwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zao walikuwa Mayahudi au Wakristo? Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu? Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliye ficha ushahidi alio nao utokao kwa Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na hayo myafanyayo.



141. Hao ni watu walio kwisha pita. Wao watapata waliyo yachuma, na nyinyi mt apata mliyo yachuma, wala hamtaulizwa nyinyi yale waliyo kuwa wakifanya wao.



Qur'an 2
Uongo.
 
HISTORIA YA QUR'AN.

SEHEMU YA KWANZA 01.

Asalaam Alaykum Warahmatullah Wabaarakatuh, Kila Sifa njema anastahiri Mwenyezi Mungu Mola mlezi wa Walimwengu wote, na Sifa njema zimuendee Kipenzi chetu Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم na Radhi za Allah ziwashukie Maswahaba zake na wema waliotangulia.

Moja kwa moja niingie Katika DARASA Jipya la HISTORIA YA QUR'AN, historia ambayo imebeba mambo mengi mno yakujifunza. InshaaAllah, Fuatana na Mimi kuijuwa Historia ya Qur'an... 👇

Nini Maana ya Qur'an.

👉 Qur-an ni wahy (ufunuo) kwa Mtume Muhammad (s.a.w) kutoka kwa Allah (s.w) kupitia kwa Malaika Jibril (a.s). Au Ni Maneno ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم kupitia Malaika Jibril عليه سلم.

HISTORIA yake...

Qur-an ilianza kumshukia Mtume Muhammad (s.a.w) mwaka 610 A.D. alipokuwa na umri wa miaka 40. Mtume Muhammad (s.a.w) alianza kushushiwa Qur-an akiwa pangoni katika mlima Hira (Jabal Hira) katika usiku wa mwezi wa Ramadhani kama Qur-an yenyewe inavyotufahamisha:

👉 "Ni mwezi wa Ramadhani ambamo imeteremshwa hii Qur-an" (2:185)

👉"Hakika Tumeiteremsha (Qur-an) katika Laylatul-Qadr (usiku wenye hishima kubwa). Na jambo gani litakujulisha (hata ukajua) ni nini huo usiku wenye hishima kubwa? Huo usiku wa hishima ni bora kuliko miezi elfu. Huteremka Malaika na roho (Jibriil) katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao kwa kila jambo. Ni amani (usiku) huo mpaka mapambazuko ya alfajiri." (9 7:1-5)

Tunajifunza kutokana na aya hizi kuwa mwezi wa Ramadhani umetukuzwa kutokana na Qur-an kuanza kushuka katika mwezi huu. Pamoja na funga kufaradhishwa kwa umma za Mitume wote wa Allah (s.w); kwa ummat Muhammad (s.a.w),funga imefaradhishwa iwe katika mwezi wa Ramadhani ili iwe ni pamoja na kusherehekea kushuka kwa Qur-an na kilele cha sherehe hii kinakuwa katika usiku wa hishima (Laylatul-Qadr) ambamo Qur-an ilianza kushuka. Mtume (s.a.w) alikuwa akizidisha kusoma Qur-an katika mwezi huu na alikuwa akikaa Itiqaf katika kumi la mwisho la Ramadhani ili aweze kudiriki kilele cha sherehe. Usiku wenye hishima (Laylatul-Qadr) ulifichwa kwa Mtume (s.a.w) lakini alifunuliwa na Mola wake kuwa unapatikana katika kumi la mwisho la Ramadhani. Ni sunnah kwa Waislamu kuzidisha kusoma Qur-an katika mwezi mzima wa Ramadhani na kukaa Itiqaf katika kumi la mwisho, ili kushiriki kikamilifu katika sherehe ya kumbu kumbu ya kuanza kushuka Qur-an.

Historia ya kuanza kushuka Qur-an kwa Mtume Muhammad (s.a.w) kupitia kwa Malaika Jibril (a.s) inasimuliwa vyema katika Hadith ya bibi 'Aisha (r.a) ifuatayo:
Bibi 'Aisha (r.a) amesema:" Kilichoanza katika Wahyi wa Mtume (s.a.w) ni ndoto za kweli. Alikuwa Mtume (s.a.w) haoti chochote isipokuwa kilitokea kama alivyoota. Kisha akaona ni bora kujitenga. Akawa anakwenda Jabal Hira kujilinda na maovu. Basi alikuwa anakwenda Jabal Hira akifanya ibada masiku mengi na alichukua masurufu kwa ajili hiyo. Masurufu haya kila yalipokwisha alirudi tena kwa Bibi Khadija, aliyemtayarishia masurufu kama yale (ya kwanza) mpaka ikambainikia haki akiwa pangoni Hira. Basi akamjia Malaika (Jibril) humo pangoni akamuamrisha kusoma, Mtume (s.a.w) alijibu: "Sijui kusoma". Alinibana kwa nguvu mpaka nikahisi taabu. Kisha akaniachia na kuniamrisha tena kusoma na nikajibu: Sijui kusoma: Kisha akanibana tena kwa nguvu kwa mara ya pili mpaka nikahisi taabu. Kisha akaniachia na kuniamrisha tena kusoma. Nilijibu tena, "sijui kusoma". Akanikumbatia tena kwa nguvu kwa mara ya tatu mpaka nikahisi mashaka, kisha akaniachia na akasema:

👉 "Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba. Amemuumba mwanaadamu kwa pande la damu. Soma na Mola wako ni Karimu sana.Ambaye amefundisha kwa msaada wa kalamu.Amemfundisha mwanaadamu mambo aliyokuwa hayajui." (96:1-5)

Mtume wa Mwenyezi Mungu alirejea na Wahy huu, huku akitetemeka kwa khofu aliyokuwa nayo. Alikwenda kwa mkewe Khadijah na akamhadithia yale yote yaliyomtokea kisha akasema;

"Nakhofia kuwa kitu kinaweza kunitokea ". Khadijah alijibu: "Hapana! Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu hatakufedhehesha. Unakaa vizuri na kuwafanyia wema ndugu na jamaa zako, unawasaidia masikini na fukara, unawakirimu wageni na unawasaidia waliokabiliwa na matatizo. "Kisha Bibi Khadijah alimchukua Mtume (s.a.w) mpaka kwa bin-ami yake, Waraqa bin Naufal bin Asad bin Abdul Uzza, ambaye alikuwa Mkristo. Waraqa wakati huo alikuwa mzee sana na alikuwa hawezi kuona tena. Khadijah alimuambia Waraqa "Sikiliza hadithi ya mpwa wako, Ewe Bin-ami yangu" Waraqa aliuliza, "Ewe Mpwa wangu umeona nini?" Mtume wa Mwenyezi Mungu alimuhadithia habari yote kama alivyoona. Waraqa akasema: "Huyu ni yule mtunza siri (Malaika Jibril) ambaye Mwenyezi Mungu alimtuma kwa Mussa. Natamani ningelikuwa kijana na kuishi mpaka wakati huo watu wako watakapokukataa na kukufukuza." Mtume wa Mwenyezi Mungu akauliza: "Watanifukuza?" Waraqa akajibu kuwa watafanya hivyo na akasema, "Yeyote aliyekuja na kitu kama hicho ulichokuja nacho alifanyiwa uadui na watu wake, na ningejaaliwa kubakia hai mpaka siku hiyo watu wako watakapokufukuza, ningelikusaidia kwa hali na mali." Lakini baada ya muda mfupi Waraqa alifariki na Wahyi mwingine ulikawia kuja kwa kipindi kirefu. (Sahihi Bukhari)
Tunajifunza kutokana na Hadith kuwa kabla Mtume (s.a.w) hajaanza kushushiwa Qur-an kupitia kwa Malaika Jibril (a.s) alikuwa akipata Wahy kwa njia ya ndoto.
Qur-an yote kwa ujumla imehifadhiwa katika ubao mtukufu wa Allah (s.w) ulio katika Arshi yake kama tunavyofahamishwa katika Qur-an:

👉"Bali hii ni Qur-an tukufu iliyotolewa katika Lawhi Mmahfuudh (huo ubao uliohifadhiwa)." (85:21-22)

Kisha kutoka Lawhi Mmahfuudh Qur-an ilishushwa mpaka wingu wa kwanza. Kisha kutoka humo ikashushwa kidogo kidogo kwa Mtume (s.a.w) kupitia kwa Malaika Jibril (a.s) kwa kipindi chote cha Utume cha miaka 23.

👉"Kwa hakika hii (Qur-an) ni kauli (aliyokuja nayo) Mjumbe Mtukufu (Jibril), Mwenye nguvu na cheo cha hishima kwa Mwenyezi Mungu. (81:19-20)

Kama tunavyojifunza katika Hadith, aya za mwanzo kumshukia Mtume (s.a.w) ni aya tano za mwanzo za suratul-’Alaq. Aya zilizofuatia katika sura hii (96:6-19) zilishuka siku za baadaye.

Aya ya mwisho kumshukia Mtume (s.a.w) alipokuwa katika Hija ya kuaga (Hijjatul Wadaai) ni aya ya tatu ya suratul Maida (5:3) ambayo imeashiria mwisho wa wahy wa Qur-an katika sehemu ifuatayo:

👉 "Leo waliokufuru wamekata tamaa katika dini yenu, basi msiwaogope, bali niogopeni mimi. Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kukutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe dini yenu" Qur'an (5:3)

Pia tunajifunza kutokana na historia ya kushuka Qur-an kuwa sura ya kwanza kushuka nzima (ikiwa na aya zote) ni Suratul-Fatiha (Al-hamdu) na imekuwa ndio sura ya kwanza katika msahafu. Katika mtiririko wa kushuka suratul-Fatiha ni Wahy wa tano. Sura ya mwisho kushuka ikiwa nzima ni Suratun-Nasr, sura ya 114 katika utaratibu wa kushuka.

Inaendelea... InshaaAllah

Allah Ni Mjuzi Zaidi.
Nasoma satanic verses of islam by Salman Rushdie. Hizi nyingine porojo
 
Hoja ipi na unakataa ushahidi nimekuwekea kuwa biblia ziko tofauti ??
Unataka tena urudi tena mwanzo
Kazi kweli kweli
Huna ushahidi wowote ndo maana unachukua video za watu wengine unaita ushahidi

Wewe akili Yako imeshikiliwa kama ulikua hujui
 
Tena nimekuwekea na video uone hao wanaokuandikia biblia wanavyoongea , unasema unasave mb
Wanaandika wapi na wakati wameziliwa wamekuta biblia na watakufa wataiacha
Ndo maana nakuambia unatatizo kubwa la kifikra yaan unaamin kwenye nguvu kuliko kutumia akili

Mtu ambaye anaakili au busara hawezi lazimisha jambo lake lieleweke
 
Wanaandika wapi na wakati wameziliwa wamekuta biblia na watakufa wataiacha
Ndo maana nakuambia unatatizo kubwa la kifikra yaan unaamin kwenye nguvu kuliko kutumia busara

Mwenye tatizo ni wewe kwani nimekuambia uangalie documentary hutaki , au hufahamu kiengereza ??
 
Ndugu zako unaowasujudu wanakimbilia Ulaya kwenda kula nguruwe, wewe huko huku Bongo kushabikia dini yao kitu ambacho nduguzo wanakikimbia huko makwao.


Mbona mnakimbilia huku Zanzibar mumejazana wengine mnalala kwenye mapaa ya nyumba za Michenzani kwa mamia mnakamatwa ??
 
Lakini Muslim mnafurahisha
"Aliyeniona mimi amemwona baba."

Wacha tuangalie muktadha:

“Filipo akamwambia, Bwana, tuonyeshe Baba, nasi yatutosha. Baba; nawe wasemaje basi, Utuonyeshe Baba?

Yohana 14:8-9

Filipo alitaka kumwona Mungu kwa macho yake mwenyewe, lakini hii haiwezekani kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kufanya hivyo. Biblia inasema:

"Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote,"

Yohana 1:18

"Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote,"

1 Yohana 4:12

"Na Baba mwenyewe aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamjaiona."

Yohana 5:37

Lakini walikuwa wakisikiliza sauti ya Yesu na kumtazama akiwa amesimama mbele yao! Yesu alikuwa anatuambia tu kwamba matendo yake mwenyewe na miujiza inapaswa kuwa uthibitisho wa kutosha wa kuwepo kwa Mungu bila Mungu kushuka kimwili na kujiruhusu kuonekana kila wakati mtu ana shaka. Hii ni sawa na kwa mfano:

1)Yohana 8:19: "Wakamwambia, Baba yako yuko wapi? Yesu akajibu, Ninyi hamnijui mimi, wala Baba yangu; kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu."

2)Yohana 12:44 "Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi, bali yeye aliyenipeleka."

3)Yohana 15:23 "Yeye anichukiaye mimi anamchukia na Baba yangu."

4)Mathayo 10:40-41 "Awapokeaye ninyi, anipokea mimi (Yesu), naye anipokeaye mimi, anampokea yeye aliyenituma. Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki."

5) Waamuzi 13:20-22 inasema: “Ikawa, huo mwali wa moto ulipopaa juu mbinguni, kutoka katika madhabahu, ndipo malaika wa BWANA akapanda katika mwali wa moto wa madhabahu, Manoa na mkewe wakatazama. wakaanguka kifudifudi, lakini malaika wa BWANA hakumtokea tena Manoa na mkewe.” Ndipo Manoa akajua ya kuwa yeye ni malaika wa BWANA.” Manoa akamwambia mkewe, Hakika tutakufa, kwa sababu tumemwona Mungu."

Ikiwa tunataka kusisitiza kwamba wakati Filipo alipomwona Yesu (AS), alikuwa amemwona Mungu "Baba" kimwili kwa sababu Yesu "ndiye" Baba na wote wawili ni "Utatu," na Yesu ni "mwili" wa Mungu, basi. hii itatulazimisha kuhitimisha kuwa Yohana 1:18, 1 Yoh 4:12, Yoh 5:37..nk. yote ni uongo.


Je, Filipo ndiye pekee ambaye "alimwona baba"? Hebu tusome:

"Si kwamba mtu amemwona Baba, ila yeye atokaye kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba."

Yohana 6:46

Ni nani huyu "aliye wa Mungu" na amemwona Baba unayemwuliza? Hebu tuulize tena Biblia:

“Yeye aliye wa Mungu husikia maneno ya Mungu;

Yohana 8:47.

Na

"Mpenzi, usifuate uovu, bali wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu; bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu."

3 Yohana 1:11.

Je, watu wote ambao wamefanya mema pia wamemwona Mungu kimwili?

"Hakuna uoni unaoweza kumshika, lakini uwezo wake uko juu ya uoni wote. Yeye ni Mpole, Mjuzi wa kila kitu."

Qur'ani Tukufu, Al-Anaam(6):103

"Na Musa alipoufikia wakati na mahala tulipo kuwawekea, na Mola wake Mlezi akamwambia, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nionyeshe ili nikutazame. [Mwenyezi Mungu] akasema: Huwezi kuniona, lakini tazama mlima, ukisimama mahali pake, basi utaniona. Basi Mola wake Mlezi alipoudhihirishia mlima akauvunjavunja na Musa akaanguka na kupoteza fahamu, alipozinduka akasema: Umetakasika! Mimi nimetubu kwako na mimi ni wa kwanza wa Waumini.

Qur'ani Tukufu, Al-Aaraf(7):143
Lakini Muslim mnafurahisha, hivi kwa matendo ya Yesu, mafundisho yake, miujiza yake, ujaji wake, uondokaji wake. Hivi Mohammad anaweza ongeza kitu juu ya neno la Yesu?
 
Lakini Muslim mnafurahisha

Lakini Muslim mnafurahisha, hivi kwa matendo ya Yesu, mafundisho yake, miujiza yake, ujaji wake, uondokaji wake. Hivi Mohammad anaweza ongeza kitu juu ya neno la Yesu?
Sijakuelewa , weka vizuri zaidi ufahamike
 
Naomba kuuliza, Quran hii ya leo ni ile ile aliyoshushiw mtume??
Yaani neno kwa neno hadi nukta ni vile vile kama ilivyoteremshwa??.
 
Mbona mnakimbilia huku Zanzibar mumejazana wengine mnalala kwenye mapaa ya nyumba za Michenzani kwa mamia mnakamatwa ??
Binafsi sioni sababu ya kwenda Zanzibar kwa sababu raha zote zipo hapa Dar, hao uwaonao wewe huko ni walalahoi wanaokuja kujiuza tu huko kwa wazungu
 
Back
Top Bottom