Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nkumbison,Na Nani?
Nkumbison,
Niwie radhi kwa kujibu swali kwa kuuliza swali.
Unadhani nani anastahili kusahihisha historia hii?
Usikatishwe tama na hawa middle class wetu ambao wamemezeshwa akili za kiuchwara za kusoma kitu SIO kwa lengo al kuelewa BUT kuuliza maswali,na matokeo yake unapata msomi kama huyu anauliza swali la kipuuzi kama hili,juzi kati tumeambia kitu muhimu mno,jibu hoja kwa hoja bora zaidi na hii ndio raha ya debate,sio kuipiga rungu hoja,kisa wewe na familia yako mpo ni a comfort zone,kinachotokea kwa jirani yako sio tatizo lako,binafsi nina hamu sana ya kujua hii historia ya nchi yangu,ninajitahidi kusoma majarida mbalimbali na nimenufaika nayo,historia ya nchi yetu imepindishwa mno kwa manufaa ya wateule wachache,na pls mtoa hoja kama unajua au una ushahidi wowote kuwa Rais wetu wa awmu ya kwanza kama katika masomo yake ,aliwahi kwenda SA na kusoma pale Fort Hare University nitashukuru mno nikielewa hili.keep up good work ur doing na usikate tama kabisa.HISTORIA YA TANU INAHITAJI MAREKEBISHOKunradhi: Hiyo picha katika gazeti ni ya Hamza Kibwana Mwapachu (1913 - 1962) si ya Abdulwahid Kleist Sykes (1924 - 1968).
Huu uzi mpaka sasa tupo watatu tuu muda naandika hapa.Usikatishwe tama na hawa middle class wetu ambao wamemezeshwa akili za kiuchwara za kusoma kitu SIO kwa lengo al kuelewa BUT kuuliza maswali,na matokeo yake unapata msomi kama huyu anauliza swali la kipuuzi kama hili,juzi kati tumeambia kitu muhimu mno,jibu hoja kwa hoja bora zaidi na hii ndio raha ya debate,sio kuipiga rungu hoja,kisa wewe na familia yako mpo ni a comfort zone,kinachotokea kwa jirani yako sio tatizo lako,binafsi nina hamu sana ya kujua hii historia ya nchi yangu,ninajitahidi kusoma majarida mbalimbali na nimenufaika nayo,historia ya nchi yetu imepindishwa mno kwa manufaa ya wateule wachache,na pls mtoa hoja kama unajua au una ushahidi wowote kuwa Rais wetu wa awmu ya kwanza kama katika masomo yake ,aliwahi kwenda SA na kusoma pale Fort Hare University nitashukuru mno nikielewa hili.keep up good work ur doing na usikate tama kabisa.
Nkanini,Usikatishwe tama na hawa middle class wetu ambao wamemezeshwa akili za kiuchwara za kusoma kitu SIO kwa lengo al kuelewa BUT kuuliza maswali,na matokeo yake unapata msomi kama huyu anauliza swali la kipuuzi kama hili,juzi kati tumeambia kitu muhimu mno,jibu hoja kwa hoja bora zaidi na hii ndio raha ya debate,sio kuipiga rungu hoja,kisa wewe na familia yako mpo ni a comfort zone,kinachotokea kwa jirani yako sio tatizo lako,binafsi nina hamu sana ya kujua hii historia ya nchi yangu,ninajitahidi kusoma majarida mbalimbali na nimenufaika nayo,historia ya nchi yetu imepindishwa mno kwa manufaa ya wateule wachache,na pls mtoa hoja kama unajua au una ushahidi wowote kuwa Rais wetu wa awmu ya kwanza kama katika masomo yake ,aliwahi kwenda SA na kusoma pale Fort Hare University nitashukuru mno nikielewa hili.keep up good work ur doing na usikate tama kabisa.
Ni marekebisho yapi unayataka ?HISTORIA YA TANU INAHITAJI MAREKEBISHOKunradhi: Hiyo picha katika gazeti ni ya Hamza Kibwana Mwapachu (1913 - 1962) si ya Abdulwahid Kleist Sykes (1924 - 1968).
Nkumbison,Huu uzi mpaka sasa tupo watatu tuu muda naandika hapa.
Kwahiyo huyo middle class ni mimi na unaamini nimemezeshwa akili za uchwara. Nakushukuru sana na hongera kwa hilo.
Naomba unisaidie kunionesha Hoja ya mleta uzi ni ipi?
Uliyoyaandika ni kama mimi ningempinga kwa kuleta kitu ambacho kipo tofauti na hiko unachoamini nilikaririshwa kiasi unazani naweza kumkatisha tamaa mwenzetu huyu.
Ukilielewa swali langu la kwanza utagundua lengo ni kumtaka afunguke hayo yanayotakiwa kuwepo katika historia husika. Ni sawa na mama akikwambia huyu sio baba yako basi itabidi akwambie baba yako ni nani hiyo ndio hoja ila unaambiwa ibadirishwe hayo mabadiliko hayawekwi.
ananiuliza tena nani aibadirishe?
Hivi kati ya mwenye kutenda kosa na mwenye kuliona nani ana nafasi ya kumwelekeza mwenzake?
kama mleta uzi na wewe mwenye akili za kuelewa na si kukariri mnapajua hii historia ilipokosewa kwanini msituelekeze na sisi wengine direct hapa ilikua hivi wakasema hivi ama vile then tutaujua ukweli halisi, na sio kunibeza mimi huku mnaishia kulalamikia kitu msichokijua hata nyie.
Kama mnaijua hiyo historia haya tupeni madini na sisi tuliodanganywa, kinyume na hapo yote uliyoyaandika kunihusu mimi na wenye mtazamo kama mimi yote yakuhusu wewe.
dingi007,Ni marekebisho yapi unayataka ?
Unatumia vyanzo vipi kurekebisha historia hiyo ? Usilete vyanzo vyenye mlengo na Dini yoyote.
Mazaya,Huyu mzee huyu
Mikocheni,,,Hizi pumba uwe unasimulia wajukuu wako
Watanzania hatuna muda na uongo wako
Kuna harufu ya kutaka dini itambuliwe kama ilipigania Uhuru kitu ambacho si Sawa kwasababu Tanzania haina udini, vyama vyote vya kidini viliuliwa ili kuweka umoja wa kitaifa kikaanzishwa Tanu.Nkumbison,
Inataka kuandikwa kitabu kizima kuhusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na nafasi ya Mwalimu Nyerere katika historia hii.
Kama nitataka kueleza niliyoshuhudia katika kulazimisha historia hii isomweshayo hivi sasa kuwa ndiyo historia yeynyewe, tutakesha hapa.
Jaribio la kwanza la kuandikia historia ya TANU ilikuwa mara tu baada ya uhuru kupatikana na ni TANU wenyewe ndiyo walitaka historia ya uhuru ihifadhiwe wahusika wenyewe wakuu wakiwa hai ili pasiwe na makosa.
Kazi hii alikabidhiwa Abdul Sykes na Dr. Wibard Kleruu.
Kazi hii ilizusha sintofahamu na Abdul Sykes akajitoa lakini Dr. Kleruu alikamilisha mswada ambao haukuchapwa kwa wakati ule.
Mmoja katika vijana wa TANU Youth League aliuchukua mswada huu bila ya idhini ya TANU na akakichapa kitabu.
TANU ilipogundua ikamuonya asichape kitabu kile tena.
Kitabu hiki hakina tofauti na kitabu kilichoandikwa na Chama Cha CCM Kivukoni, ''Historia ya Chama Cha TANU 1954 - 1977,'' (1981).
Kitabu hiki cha Chuo Cha Kivukoni nilipokisoma kilinisikitisha sana kwani kwa uhakika hakukuwa na historia ya TANU kwa ukweli wake bali ni kabrasha lililojaa habari za TANU lakini si historia kwani waasisi wenyewe wa TANU hawakutajwa ndani ya kitabu ukimtoa Julius Nyerere.
Labda msomaji atataka kujua iweje mimi niseme kuwa kitabu hiki hakikuandika historia ya TANU.
Mimi sijaijua historia ya TANU kwa kusoma au kufundishwa shule au kokote kule.
Nimeijua historia ya TANU kwa sababu wazee wangu ndiyo walioasisi chama hicho na historia yao hii inakwenda nyuma hadi mwaka wa 1929 walipoasisi African Association.
Hawa wazee ndiyo walionifunza mimi historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.
Kuhofia kupotea wa historia hii ndipo nilipoamua kuandika kitabu na kwa makusudi ili nipige ndege wawili kwa jiwe moja niliamua kueleza historia ya TANU kupitia maisha ya Abdul Sykes kwa kuwa walioandika historia ya TANU waliamua kwa makusudi kulifuta jina lake katika historia ya Tanganyika.
Kitabu cha maisha ya Abdul Sykes kilieleza historia ya TANU na lilikuwa jibu sawia kwao hao wote waliojaribu kuibadili historia ya uhuru wa Tanganyika.
Kitabu kimechapwa London mwaka 1998 kwa Kiingereza na tafsiri ya Kiswahili ikachapwa Nairobi mwaka wa 2002 na kinakwenda toleo la tatu Kiingereza na toleo la nne Kiswahili.
Juu ya kuisahihisha historia ya TANU bado makosa yanaendelea kama tulivyomsikia Mzee Msekwa.
Nkumbison,Kuna harufu ya kutaka dini itambuliwe kama ilipigania Uhuru kitu ambacho si Sawa kwasababu Tanzania haina udini, vyama vyote vya kidini viliuliwa ili kuweka umoja wa kitaifa kikaanzishwa Tanu.
Nkumbison,
Unajitia hofu pasi na sababu.
Mchango wa Waislam kama jamii katika mapambano ya uhuru unafahamika na hakuna ubaya wowote kuifadhi historia yake.
Kunena,Mzee navutiwa kujifunza zaidi, napenda kufahamu unadhani ni kwanini wazee hawa hawakutambuliwa katika historia ya TANU?!...ilhali kina Bibi Titi wanatambulika?!....nikiri habari za wazee wa Kariakoo gerezani kina Sykes nimezisikia kwako juu ya ushiriki wao katika harakati za Uhuru.
Sasa tutaitambuaje historia iliyosahihi ilhali haujui hata kwa nini hawakuandikwa, umejaribu kuulizia kwa walioiandika ya sasa kwanini wahusika wengine hawajawekwa katika hiyo historia ya TANU?Kunena,
Hata mimi sijui kwa nini.