Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #21
Nkumbison,Sasa tutaitambuaje historia iliyosahihi ilhali haujui hata kwa nini hawakuandikwa, umejaribu kuulizia kwa walioiandika ya sasa kwanini wahusika wengine hawajawekwa katika hiyo historia ya TANU?
Kama wewe au na wengine hamuijui historia ya kweli nakushaurini msome kitabu cha Abdul Sykes.
Nimekiandika baada ya kuona kuwa historia iliyoandikwa si historia ya kweli.
Mimi naijua historia ya kweli ya TANU kwa kuwa walioasisi chama hicho ni wazee wangu na historia hiyo haikuanza mwaka wa 1954 bali 1929 wazee wangu walipoasisi African Association na kwa bahati nzuri wameacha nyaraka, picha na mswada wa historia hii.
Vyote hivi viko ndani ya kitabu changu.