huwa sina tabia ya kulalamikia upuuzi ambao hauathiri maendeleo yangu. Sijasema kuwa mimi ni Mchagga, ila nimekuambia kuwa nina asili ya huko, jua kutofautisha vitu viwili,
sawasawa?
Hilo la kuwa kila anaetoka Musoma ni Mkurya si kweli, tangu nikiwa mdogo najua kuwa kuna Wazanaki, Wajita, Warianchoka, Wajaluo, Waruuri n.k n.k. Na hakuna siku ambayo Wazanaki wali-claim kuwa wao ni Wakurya kabla ya kuja kuenguliwa kwenye Ukurya baadaye, kama unavyotaka kutuaminisha hapa. Ama kuhusu Mt. Kilimanjaro, so far kuna makabila mawili ya kudumu yanayopatikana arround, Wachagga na Wataita kwa upande wa Kenya, unaweza kuwaongeza na Wapare, ingawa wako mbali kidogo na mlima, pia kuna makabila ya kifugaji, hawa huwa siwapi sana nafasi kwa kuwa si wakaazi wa kudumu.
Back to topic: Bado hujanipa vigezo vya kiutamaduni ambavyo vinachambulika, ili tuweze kuyachambua hayo makundi matatu, tujiridhishe kuwa si Wachagga.
Patiently waiting...