HISTORIA FUPI YA KABILA LA WAMAKONDE
Kama ulikua hujui chanzo Cha Wamakonde kuweka NDONYA na kuchanja CHALE wacha nikufahamishe;-
Wamakonde ni kabila linalo patikana katika wilaya zote za Mkoa wa Mtwara ila Masasi na Nanyumbu wapo kwa asilimia ndogo na kwani wenyeji wa Masasi Ni Wamakua na wenyeji wao Nanyumbu ni Wayao.
Kama ulikua hujui ;-Rais Benjamin William Mkapa sio mmakonde Ni Mmakua,
Wamakonde wamejipatia umaarufu mkubwa nchini Tanzania kutokana na kuwa na ukakamavu na shughuli za uchongaji wa vinyago. Tofauti kubwa kati ya Wamakonde wanaoishi Kusini mwa Mto Ruvuma (Msumbiji) na Kaskazini mwa Ruvuma (Tanzania) ni aina ya urembo wa ndonya. Wale wa Msumbiji wana ndonya ndogo juu ya midomo yao wakati wa Tanzania wana ndonya kubwa zaidi midomoni mwao.
Wamakonde huonekana kwa uzuri wao, wapo waliochanja sehemu za juu ya mdomo, masikio na uso. Inaaminika kuwa chanzo cha kuchanja, kutoboa midomo na kuweka ndonya ilikuwa kujilinda dhidi ya wafanyabiashara wa watumwa ambao walibeba watumwa kwenda kwenye mashamba huko Ulaya.
Ndonya na Chale ziliwakasirisha sana wafanyabiashara wa Kiarabu kwa kuona kuwa watu hao hawapendezi. Wamakonde wengine wa Msumbiji waliamua kuchonga meno yao, ili kujilinda, kwamba mtu ambaye angeingia katika himaya yao akiwa hajachanja, hana ndonya na hajachonga meno, walimuona ni adui yao na kama ni mweusi, ni mpelelezi wa Waarabu ili wavamie kuwachukua kwenda utumwani.
Tabia hizi zikawa ni desturi na mila zao na zikawa kama urembo ndani ya kabila la Wamakonde. Baada ya kukomeshwa kwa biashara ya watumwa, mila hizi zilianza kutoweka na wengi wameachana nazo.
Hicho unachokiona hapo Puani ndio inaitwa NDONYA Ni mti wa mpingo huchongwa na kuwekwa katika kuweka hutobolewa hadi fizi za juu yaani akicheka unauona umetokeza kwa ndani upande wa juu ya mdomo.
Makala hii imeletwa kwenu na Dhulkad Madara kutoka morogoro