The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 1,497
- 2,681
Kuna uhakika na kuaminika kwamba, Wasambaa ni moja ya makundi ya Wabantu wanaotokea Afrika Magharibi na Kaskazini wakipitia nchi za Ethiopia na Kenya. Wasambaa ni tawi lilomegega kutoka kwa Waasu/Wapare. Wachaga n.k. pindi wakiwa safarini kuja Tanganyika miaka zaidi ya mia nane (800) iliyopita. Haya majina ya Wasambaa, Wachaga, Wapare n.k. hayakuwepo pindi hao Wabantu walipokuwa wanaingia Tanganyika, isipokuwa wamepeana wenyewe kundi na kundi kupitia utani na umaarufu au asili ya eneo.
Utawala wa Wasambaa ulikuwa imara sana na ngome maarufu ni huko Vugha ikawa Bumbuli pia kulikuwa na chifu, ila Vugha ndiyo inaonekana makao makuu ya Wasambaa hata kabla ya Mbegha kuingia Usambara.
Huyo miaka ya 1800 alitoroka huko Kilindi na kuja Usambaani kupitia Zia Bumbuli.
Mbegha (pia: Mbega baada ya 1700) ni jina la mtu muhimu katika historia ya Washambaa anayekumbukwa kama mfalme wao au mwene mkuu wa kwanza katika kundi hili. Familia ya watawala iliyoanzishwa naye hujulikana pia kama nasaba ya Kilindi.
Kufuatana na "Habari za Wakilindi, Mbegha kiasili alikuwa mtoto wa Mwarabu aliyetoka Pemba na kuhamia Kilindi na mke wake Mngulu. Inaonekana ya kwamba waliishi baadaye kati ya Wangulu. Mbegha anakumbukwa kama mtoto kigego aliyetangulia kupata meno ya juu iliyotazamiwa kama ishara mbaya kati ya makabila mbalimbali na mara nyingi waliuawa. Labda kwa sababu babake alikuwa Mwislamu mtoto aliruhusiwa kuishi lakini baada ya kifo cha wazazi na kakaye alinyimwa urithi wake na nduguye waliomkumbuka kama kigego na kumshtaki kuwa ni mchawi.
Mbegha aliamua kuondoka katika ukoo uliomkataa akawa mwindaji aliyeishi msituni. Alikuwa stadi sana kwa sababu alikuwa kati ya watu wa kwanza waliotumia mbwa wa kuwinda akampenda hasa mbwa wake " Chamfumu". Alipata umaarufu kwa sababu alifaulu kupunguza nguruwe mwitu waliokuwa tishio kubwa kwa wakulima na mazao kwa hiyo walimheshimu na kumpenda. Vijana walikuja kukaa naye akawafundisha mbinu za uwindaji.
Alisemekana kujua pia mbinu za uganga zilizomsaidia kuwinda, kuwashinda maadui na pia kuponya watu.
Baada ya kuondoka katika Ungulu alihamia kwanza Kilindi alipokumbukwa kutokana na babake na pia umaarufu wake kama mwindaji. Chifu wa mji akampatia nyumba akawa rafiki wa mwana wa chifu. Siku moja walipoenda pamoja kuwinda huyu kijana aliuawa na nguruwe mwitu na Mbegha aliona hawezi kurudi Kilindi akiogopa hasira ya chifu akaamua kuhama tena akiongozana na vijana 14 na mbwa zake. (Hapa ndio palipoweka alamu mpya kwa wasambaa hadi leo, kifo cha mtoto wa chifu wa Kilindi)
Pamoja na kundi lake walizunguka wakapiga kambi huko Zirai kando ya Usambara. Wazee wa Bumbuli wakamkaribisha kuja kwao (Kama kawaida ya ukarimu wao) na chifu Mbogho wa Bumbuli alimpa binti yake kama mke akampandisha kuwa chifu pamoja naye.
Sifa zake zilisambaa kati ya Washambaa. Wakati ule Washambaa wa Vuga walikuwa na vita dhidi ya Wapare wakaona wapate usaidizi wa Mbegha. Kiongozi wa Vuga akamwendea akamwomba kuhamia kwao na kuwa mwene wao (Mfalme). Mbegha aliomba kibali cha mkwe wake chifu Mbogho, akaongozana na watu wa Vuga pamoja na mke na shemeji yake.
Huku Vuga alikaribishwa kwa mapigo ya ngoma kubwa watu wengi wakaja kumkaribisha wakamjengea nyumba alipoingia. Mkewe alikuwa mjamzito tayari, akamwandalia kitanda kilichofunikwa kwa ngozi ya simba aliyowahi kuua safarini kuelekea Vuga. Mtoto aliyezaliwa juu ya ngozi ya simba akapewa jina la Simba akawa mrithi wake wa baadaye akipewa pia jina rasmi la Buge. Kutokana na jina hili watawala wa Vuga waliendelea kutumia cheo cha Simba Mwene. Baadaye huyu mwana wa kwanza alikuwa chifu wa Bumbuli kwa kibali cha baba.
Mbegha aliendelea kuoa mabinti kutoka koo za Washambaa mbalimbali na kuweka wanawe kutoka kio hizi kama watawala na wawakilishi wake juu ya vijiji vya mama zao. Kwa njia hii aliunganisha Usambara na koo za Washambaa na kuweka msingi kwa utawala wa kifalme katika Usambara uliosimamia sehemu kubwa ya Tanzania ya kaskazini kabla ya kuja kwa Wazungu.
Watawala wa nasaba yake waliomfuata Vuga waliendelea kuoa wake wengi na kuweka wana wao kama wata