Hapo ndio umejimaliza kabisa kwa sababu aliyetunga wa South Africa ni methodist.
Tanzania ilipata uhuru 1961, Zambia 1964 na Africa Kusini 1994; hadithi ya kuku na yai.
Lakini Enoch Mankayi Sontonga ndiye inasemekana alianzisha ile ya South Africa. Huyu alikuwa ni choir master na methodist ambayo ni movement ya protestant christianity. Hapa cha msingi ni kwamba asili ya huu wimbo ni kanisani kwa ushahidi wote.
Mkuu reasoning yako inafurahisha sana. Kwenye post moja umesema ni wimbo wa kikatoliki. Na hapa unasema umetungwa na methodists wa Afrika Kusini. Sasa unachotaka kusema ni kipi? Tangu lini methodism ni movement? Ninachofahamu ni kuwa methodism ni denomination moja ya ukristo, labda wewe una uelewa mzuri zaidi wa maana hii.
Lakini kama wimbo wa ANC asili yake ni kanisani kibaya ni nini? unataka asili yake iwe kaswida au taarab? Nilichosema ni kuwa wimbo wa Taifa wa Tanzania ni copycat ya Wimbo wa ANC, ambao pia Zambia wanautumia. Haijalishi kama mtunzi ni Methodist, Islamist au pagan, lakini si kweli kama wimbo wa taifa wa Tanzania ulitungwa Peramiho.
Unaposema Tanzania ilipata uhuru mwaka 1961 una maana gani? Tanzania haijawahi kutawaliwa, labda kama una maana Tanganyika labda naweza kuelewa kiasi. Sijui elimu yako, mimi elimu yangu ni ya msingi lakini najua kiasi kuwa Tanzania haijawahi kutawaliwa. Inaonekana wewe si mtanzania, na kama ni mtanzania basi huenda hata darasa la tatu hjafika na hujui kuwa nchi inayoitwa Tanzania ni muungano wa nchi mbili, moja ilikuwa inaitwa Tanganyika na nyingine inaitwa Zanzibar. Tanganyika iliwahi kuwa koloni la mdachi, na baadaye protectorate iliyokuwa chini ya mwingereza, Zanzibar iliwahi kupitiwa na mreno, kutawaliwa na sultani na kusimamiwa na mwingereza. Nchi mbili zilipoungana na kuunda nchi inayoitwa Tanzania haikuwahi kuwa chini ya mkoloni.
Afrika Kusini ilitawaliwa na mwingereza na ilipata uhuru mwaka 31.05. 1910, sio 1994. Mwaka huo unaouita ni wa uhuru ni mwaka ambao utawala wa kibaguzi wa waafrikaner ulikomeshwa baada ya uchaguzi wa kura moja, mtu mmoja, bila msingi wa rangi.
Uhuru wa Afrika Kusini wa mwaka 1910 au kuondolewa kwa sera ya ubaguzi wa rangi mwaka 1994...hakuna uhusiano na wimbo wa chama wa ANC ambacho kimekuwepo kabla ya Tanzania.
Mkuu kama unaweza kuja kwenye internet na ukasoma, unaweza kupata mengi tu ya kukuelimisha, usije ukadhani hapa JF ni kijiwe cha vilaza, ukaongopa na watu wakaamini.
I hope you will not take this personal.