Historia yangu ya mapenzi iliyoniachia Makovu kiuchumi na kisa cha Maskini akipata matako hulia Mbwata

Historia yangu ya mapenzi iliyoniachia Makovu kiuchumi na kisa cha Maskini akipata matako hulia Mbwata

Paploman

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2019
Posts
1,759
Reaction score
3,465
Ukisikia usemi “ Maskini akipata matako hulia Mbwata” basi mimi ni mfano halisi wa hili, 2010 mwishoni kabisa nikiwa bado bwana mdogo tu, around 20’s na Bahati ikawa upande wangu nikawa tayari nimepata ajira katika moja ya taasisi inayolipa vizuri mno hapa nchini.

Account yangu ya bank ikawa inasoma zaidi ya 60m (48m nilikopeshwa na ofisi bila riba kama muajiriwa mpya nikajenge nyumba, 15m nilikopa CRDB changanya na vijisenti vingine), Bado nikawa na safari nyingi sana ilikuwa ni kawaida kumaliza mwezi na zaidi nikiwa sijui mlango wa ofisi yangu ukoje, nakula per diem tu za safari za kikazi huko site mikoani.

Kwa mawazo yangu mda huo, nikaona huu ni mda halisi wa kuwatafuna wale wote walionikataa hasahasa wanafunzi wa CBE na IFM, kiukweli hakuna mtu aliyekuwa na ubavu wa kunikataa kipindi hiki, nikiwa tayari nimeshanunua gari ambayo kwa asilimia kubwa niligeuza kama guest kwa mda huo, nilifanya utoporo wa kila aina.

Kama mjuavyo “He who dips his finger into honey does not dip it once” nikawa nimenogewa tepetepe na hii michezo.

Sasa kukawa kuna msichana ambae tulifahamiana nae kupitia facebook ni mnyarwanda kwa maelezo yake alikuwa anasoma college huko Rwanda, kwa muonekano wake alinivutia kwelikweli na tayari tulishakuwa wapenzi wa mtandaoni kwa mda kidogo, tukapanga ratiba ya yeye kuja Bongo tubanjuane, haha😀😀😀 “The goods of blind people are in their hands”

Yaani nikawa nimeshajimwambafai sana kwake kwamba mimi mambo yangu safi na familia yangu ni ya kishuwa na hata yeye nilimkatia tiketi ya ndege toka Rwanda. Ujinga ni mzigo sana wakuu nilianza kumpandisha ndege demu nisiyemjua kabla ya wazazi wangu waliohangaika na mimi katika mazingira magumu. Daaah

Demu alifika na nikampokea, Kweli alikuwa mzuri lakini kwa kutaka kujionesha kwamba nina pesa kama nilivomueleza awali ilinilazimu tuishi maisha ya VIP, nilipokuwa nasafiri kikazi tunaambatana naye na uzuri ofisi ilikuwa inatoa gari kwa ajili ya maofisa wake wanaosafiri kikazi.

Mtoto akawa amepagawa kabisa kuona anapanda V8 akaamini kabisa mimi na familia yangu mambo safi, akawa ananiambia “ Nikimaliza college tuoane unitafutie kazi hukuhuku Tz” 😀 Kwa kujimwambafy nikawa namjibu " Wewe maliza tu shule suala la kazi niachie mimi ni jambo dogo"haha,

Uzuri pia dereva tuliyekuwa nae alikuwa bado kijana na yeye ni mtu wa totozi pia na hakuwa na hiyana kabisa akijua mna mademu zenu anawaita "Boss", So suala la kukufata kutoka hoteli tulizofikia na kukutembeza kila mnapohitaji baada ya kumaliza majukumu kwake ilikuwa sio ishu na hii ikamuamisha zaidi huyu kiumbe kwamba mimi ni Boss mtoto. HAYA MAMBO HAYA😀

Huyu kiumbe ule mwezi na nusu aliokaa kwangu nilitumia pesa ambazo sijawahi kuzitumia tena katika historia ya maisha yangu na badala yake nikapitia magumu kwa kulipa mkopo hewa ambao sijaufanyia la maana mpaka mwaka 2015 ulipoisha.

Huyu msichana mpaka leo hii huwa anajua mimi natokea familia ya kishuwa sana japo sijawahi tena kuonana naye zaidi ya kutumiana picha tangu aliporudi kwao. Na alinifaidi kwelikweli kuliko msichana yeyote hata wife sidhani labda ni vile tunashare mali zetu kwa pamoja.

Tangu mwaka 2015, nikafanya upya reform ya mfumo mzima wa maisha yangu mpaka sasa nimepiga hatua kiasi chake lakini naamini ningejipanga mapema hapa mjini kwa sasa ningekuwa sishikiki.

Share hapa kisa chako CHA ULIMBUKENI WA MAPENZI kilichoathiri uchumi wako kwa kiasi kikubwa na ambacho unakijutia mpaka leo ukikumbuka.
 
Hii ndo shida ya kupata hela ukiwa kijana hasa usiye na critical thinking,

Huwa nakumbuka ushauri wa mama mmoja aliwahi sema ukipata pesa au madaraka ukiwa kijana utatesa kwenye jamii, unaweza haribu jamii, fanya utafiti mimi nazidi KUTHIBITISHA tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BOSS, Not all information is trustworthy, and some sources of information are intended to mislead or confuse people. For this reason, it is important to know that, not only young people have'nt the critical thinking skill to analyse information and evaluate its authenticity
 
I conquer with you, your Excellency, Unfeigned I intended to ponder out how most of youths fall under the same arena, am not despising you for whatever happened but as you're trying to share herein your experience in love matters in comparison With your age, it sounds how you're regretting sir.

All in all it's past, we have long way to go.

Thanks!

🤝👏 Thanks boss
 
Back
Top Bottom