CRICKET
JF-Expert Member
- Oct 17, 2013
- 334
- 84
1) TATIZO la Vijana wetu wa KIZAZI KIPYA kutojua Mambo Muhimu kuhusiana na HISTORIA YA NCHI YETU ni tatizo kubwa.
2) Kwa MAONI YANGU, KAZI YA ZIADA inatakiwa ifanyike KUIELIMISHA JAMII ambayo, kwa asilimia kubwa, imeanza kuingia GIZANI kuhusu UZALENDO na HISTORIA YA NCHI!
3) VIJANA wetu wala si wa kulaumiwa, bali kuonewa huruma! Mfano, wee jaribu kuulizauliza vijana wanaosoma SEKONDARI, walio VHUO VIKUU na walio kazini (ikiwa ni pamoja na WAZAZI, WAALIMU na WAANDISHI WA HABARI) kuhusu yafuatayo (ili uone ni wangapi wanajua mangapi) :
a) Tarehe ya TANZANIA kupata UHURU.
b) Tarehe ya TANGANYIKA kupata UHURU.
c) Tarehe ya MUUNGANO wa TANZANIA na ZANZIBAR.
d) Tarehe ya Muungano wa TANGANYIKA na ZANZIBAR.
e) Tarehe ya ZANZIBAR kupata UHURU.
f) Tarehe ya MAPINDUZI YA ZANZIBAR.
g) ZANZIBAR ilitawaliwa na nani?
h) Kinjekitile ni nani, alizaliwa na kufa lini, na UMUHIMU wake katika Historia ya Nchi yetu.
i) Mkwawa ni nani, alizaliwa na kufa lini na UMUHIMU wake katika Historia ya Nchi yetu.
4) Siku hizi, si kila mtu anajua watu wafuatao (nimewataja kama mfano tu) ni akina nani na UMUHIMU wao katika Historia ya Nchi yetu:
a) Shaaban Robert.
b) Milambo.
c) Filbert Bayi.
d) Mwinga Mwanjala.
e) Suleiman Nyambui.
f) Familia ya Matumla.
g) Abdulrahman Babu.
h) Issa Shivji.
i) Familia ya Karume.
j) Edward Moringe Sokoine.
k) Rashid Mfaume Kawawa.
l) Joseph Sinde Warioba.
m) Salim Ahmed Salim.
n) Bibi Titi Mohammed.
o) Sokoine alikufaje? Mzee Karume alikufaje?p p) Kreluu ni nani na Mwamwindi ni nani?
5) Ni watu wangapi wa KIZAZI KIPYA wanajua kwamba Ukumbi wa Bunge wa zamani ni Karimjee Hall na lini BUNGE lilihamia Dodoma?
6) POINTI YANGU NI NINI? Hili ni TATIZO KUBWA LA KITAIFA na linahitaji kushughulikiwa vizuri zaidi na SERIKALI pamoja na JAMII nzima.
7) Kwa MAONI YANGU, "ELIMU" hii haitakiwi itolewe "DARASANI" tu (kwa watu waliosoma MASOMO SANAA) bali ni ELIMU inayotakiwa kutolewa KITAIFA (kufuatia MWAMKO WA KITAIFA). ELIMU hii inatakiwa itolewe kupitia TV, RADIO, MAGAZETI, MITANDAO, MAJUKWAA YA KISIASA, MAJUMBANI NA MASHULENI bila kujali mtu anasoma nini (combination gani)!
8) Vinginevyo, tutaendelea KUTOKOMEA GIZANI KWA UMBUMBUMBU huku tukijivunia Majina Mazuri ya Mitaa na Mashule (Mfano, Shaaban Robert) ambayo hamna anayejua maana yake hasa!
9) Ahsante.
BJC. DSM. 25.10.2017. 0910hrs.