Hitalafu za Huduma za Amazon (AWS) imesababisha kutopatikana kwa Application nyingi Duniani ikiwemo snapchat, Fortnite na Canva

Hitalafu za Huduma za Amazon (AWS) imesababisha kutopatikana kwa Application nyingi Duniani ikiwemo snapchat, Fortnite na Canva

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351
Kitengo cha huduma za mtandaoni cha Amazon, Amazon Web Services (AWS) kimekumbwa na hitilafu na kusababisha changamoto ya upatikanaji wa huduma kwa makampuni mbambali duniani.
Huduma zilizopata changamoto ni pamoja na tovuti na programu kadhaa maarufu, zikiwemo game ya Fortnite, mtandao wa Snapchat na ya Duolingo.
Huduma zingine zilizopata hitlafu ni pamoja na kampuni ya AI ya Perplexity, mfumo wa kubadilishana sarafu za kidigitali (Cryptocurrency) Coinbase na Jukwaa maarufu la kuuza na kununua hisa Robinhood.
IMG_2753.jpeg

IMG_2750.jpeg


AWS (Amazon Web Servicees ) hutoa huduma za kuhifadhi data, huduma za kompyuta mtandao (cloud computing), na huduma zingine za kidijitali kwa makampuni, serikali na watu binafsi.

Taarifa rasmi ya AWS imesema wanaendelea na jitihada za urejeshaji wa huduma, huku wakigusia kuwa 'Suala la DNS limepunguzwa kikamilifu'
DNS (Mfumo wa Jina la Kikoa) hufanya kazi kama ramani ya mtandaoni, ikitafsiri majina ya tovuti kuwa taarifa ambayo kompyuta inaweza kuchakata kwa haraka.
Pia wamekili changamoto zinazoendelea: "Maombi mengine yanaweza kupunguzwa wakati tunafanya kazi kufikia utatuzi kamili", na wameahidi kutatua tatizo mapema iwezekanavyo, na kama kutakuwa na maelezo ya ziada basi watashirikisha wateja wao.

Tatizo lilikuwa hitilafu ya ndani ya AWS DNS, katika kituo cha huduma za kuhifadhi data cha DynamoDB chaa US-EAST-1 (Northern Virginia).
US-EAST-1 ni mojawapo ya server kubwa ya AWS inayoitegemea katika huduma zake, changamoto yeyote katika kituo hiki kunaweza kuathari huduma nyingi za mtandaoni niani kote.

Huduma ya Alexa pia imeathirika kwa sehemu kubwa, pamoja na taasisi za kifedha kutoka mataifa mbalimbali
Hii ni orodha ya huduma zilizo athiriwa na changamoto ya AWS kulingana na taarifa za Internet Access Downdetector
  • Snapchat
  • Amazon
  • Amazon Web Services
  • Roblox
  • Amazon Alexa
  • Ring
  • Max
  • Chime
  • Robinhood
  • Spectrum
  • Venmo
  • Blink Security
  • McDonald’s App
  • Reddit
  • Canvas by Instructure
  • Fortnite
  • Epic Games Store
  • Amazon Prime Video
  • VRChat
  • Life360
  • Hulu
  • Lyft
  • Xfinity by Comcast
  • Roku
  • United Airlines
  • Signal
  • Dead By Daylight
  • Fanduel
  • Clash Royale
  • Peloton
  • CharacterAI
  • Disney+
  • SimpliSafe
  • T-Mobile
  • New York Times
  • Verizon
  • Internet Movie Database (IMDb)
  • Whatnot
  • AT&T
  • Amazon Music
  • My Fitness Pal
  • Rocket League
  • Playstation Network
  • Steam
  • Canva
  • Rainbow Six Siege
  • Ubisoft Connect
  • Pokemon Go



IMG_2752.jpeg


IMG_2749.jpeg

IMG_2748.jpeg
 
Wenzetu wana akili, watachukua hiyo kama challenges ya kusonga mbele zaidi baada ya kutatua hilo tatizo.
 
Shida nini? DNS migration? Cloud switching and routing?
The root cause was identified as a DNS resolution issue affecting the DynamoDB API endpoint, leading to increased error rates and latencies that cascaded across at least 37 dependent AWS services and third-party platforms.
 
The root cause was identified as a DNS resolution issue affecting the DynamoDB API endpoint, leading to increased error rates and latencies that cascaded across at least 37 dependent AWS services and third-party platforms.
Hii kazi ya DNS MIGRATION nimetoka kuifanya juzi juzi tu hapo nimeimaliza jana, ni kazi ambayo process zake inatakiwa uwe umeandaa vyema ili kuwe na zero downtime otherwise ndio hayo ya AWS lazima yatokee...
 
Back
Top Bottom