Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 15,415
- 29,584
Kuna namna moja ya ujinga ambao baadhi ya Watanzania wenzetu wanao - kupima ubora wa mtu kwa kutumia vigezo vya kifedha au kiuchumi. Utakuta mtu anapayuka kama mwendawazimu huyu kiongozi anafaa sana, ukiuliza kwa nini anakuambia ametuletea daraja, au amejenga zahanati, au amesaidia kukusanya mapato mengi ya kodi nk.
Sasa unawauliza, unajua kiongozi wa zamani Adolf Hitler aliifanyia Germany mambo makubwa kiasi gani?Utakuta mara nyingi hawajui. Ndio unawaeleza kuwa Adolf Hitker wa Germany aliipandisha Germany kutoka taifa masikini baada ya vita kuu ya dunia ya kwanza hadi kuwa taifa lenye nguvu ya kuweza kupigana na nchi karibu zote duniani. Hata hivyo, Hitler alikuwa muuaji mkubwa wa raia wa Germany waliompinga au kwa sababu za kibaguzi tu, kama kutaka kuwa na kizazi cha Wajerumani wa mbegu bora.
Sasa je, historia inamwona Hitler kama kiongozi aliefaa kwa sababu tu aliifanya Germany kuwa taifa tajiri na lenye nguvu? Kumbuka, leo hii ukimsifia Hitler kwa mazuri na makubwa aliyofanya Germany unaweza kuuwawa na watu fulani, kwa kutonesha vidonda vyao.
Tujiongeze jamani na kujitoa ujinga. Ubora wa mtu haupimwi kwa vigezo vya madaraja na makusanyo ya TRA peke yake. Kiongozi bora ni yule anaeunganisha watu bilakujali itikadi zao za kisiasa au kidini, anasimamia vema uchumi na rasilimali za taifa, anaheshimu utu wa watu wengine, anafuata haki za binadamu na kuongoza kwa misingi ya demokrasia na utawala wa sheria kulingana na katiba ya nchi. Nje ya sifa hizi kiongozi huyo HAFAI.