HIV, AIDS cure news 2016: Viable cure still elusive, experts say

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
With the scourge of HIV/AIDS continuing to plague mankind, the 21st International AIDS Conference saw the participation of thousands of attendees from different walks of life in order to pursue the eradication of this illness.

According to Vine Report, this event was held in Durban, South Africa from July 18 to 22. The event saw scientists, advocates, philantrophists and even those afflicted by HIV all coming from 180 different countries to share their own experiences and further their cause in search of a cure. After all, this illness has claimed the lives of countless people throughout the years due to its ability to stop the body from fighting other infections. But with everyone's efforts, HIV/AIDS has seen a significant drop in cases annually.

The executive director of UNAIDS, Michel Sidibe, said that research and innovation are much needed in order to come up with a vaccine and a subsequent cure. According to the AIDS Map, no country has yet achieved the UNAIDS vision of having 90 percent of HIV-positive people diagnosed, 90 percent of diagnosed people on therapy and 90 percent of the treated people virally suppressed. So far, 41 percent of HIV-positive people globally has received antiretroviral therapy (ART), and the coverage of healthcare still remains low in a lot of locations.

The North Carolina Health News points out that while humanity is making great strides in terms of making a viable cure, there is still little indication about the time needed to realistically produce it. They asked Wes Thompson, a participant in the International AIDS Conference, about it, and he said that the destruction of the latent or hidden virus remains to be the greatest challenge to finding a cure. As such, it will need to have a multi-pronged approach, so a cure is still far from being released.

For now, people are advised to focus on preventive measures and wait until more updates are made.

Pamoja na jitihada nyingi zinazofanywa, dawa haijapatikana hivyo watu waendelee kuishi kwa tahadhari.
 
dada inakaa unafanya research sana ya huu ugonjwa ebu nisaidie adhari za hizi arvs na je mtu akitumia anaweza kuongeza miaka mingp? na je ukianza kutumia zinaeeza kukuzingua kwa Muda gani na Ile adha yake ikaisha
 
dada inakaa unafanya research sana ya huu ugonjwa ebu nisaidie adhari za hizi arvs na je mtu akitumia anaweza kuongeza miaka mingp? na je ukianza kutumia zinaeeza kukuzingua kwa Muda gani na Ile adha yake ikaisha
Mkuu kuanzia mwaka 2006 kulikua na mabadiliko makubwa sana ya ARV's, zilikuja dawa bora ambazo zina side effect chache, pamoja na hayo unatakiwa kuwa kwenye kitengo ambako wanakuangalia afya yako mara kwa mara. Dawa zikianza kukusumbua watatafuta dawa ya kukubadilishia. ARV's ziko nyingi lakini ninavyofahamu ukiwa unakunywa bila kuacha kwa muda unaotakiwa (adherence) unaweza kuishi na ugonjwa kwa miaka kati 40-50 tangu ugundulike kuwa unao.
 
Lakini dada Jana si ulikuja na habari za wale madaktari wa kule Denmark ambazo zilikua zinaleta matumaini ya kwamba in the near future Aids inaweza kuwa historia?sasa leo imekuwaje tena umekuja na habri hizi za kukatisha tamaa?
 
Lakini dada Jana si ulikuja na habari za wale madaktari wa kule Denmark ambazo zilikua zinaleta matumaini ya kwamba in the near future Aids inaweza kuwa historia?sasa leo imekuwaje tena umekuja na habri hizi za kukatisha tamaa?
Si ya kukatisha tamaa, ukweli ni kuwa mpaka sasa hakuna dawa ya kutibu iliyoko sokoni. Dawa zinazoleta matumaini bado ziko kwenye utafiti, lakini mambo yanaelekea kuwa mazuri. Dhumuni la kuweka yote haya ni kuwapa moyo waathirika kuwa kuna mwanga mbele ambako si mbali.
 
Lakini dada Jana si ulikuja na habari za wale madaktari wa kule Denmark ambazo zilikua zinaleta matumaini ya kwamba in the near future Aids inaweza kuwa historia?sasa leo imekuwaje tena umekuja na habri hizi za kukatisha tamaa?
yaani inavyoonekana soon huu ugonjwa utakua historia coz Kuna mahali nimepata hii kuwa kwa wale ambao wameshatumia arvs na wale virus wanatulia wanampango wa kuleta arvs ya sindano hii inadungwa unatulia tena miezi mitatu ndiyo unaenda tena kudungwa na hii kuondoa adha ya wale watumiaji wa dawa wanazokutana nazo huoni ni mapinduzi mapya? cha msingi ni watu kubadilika na kufuata masharti tuu.
 
Na kama unafuata masharti na daktari wako anakuamini, anaweza kukupa mzigo wako wa mwaka mzima.
 
Ni kweli uwezekano wa kupatikana dawa ya huu ugonjwa upo,sema tu kunaonekana kuna siasa na biashara nyingi ndani yake,ndo maana leo unasikia hivi mara kesho hivi ilimradi tabu tupu,lakini kwa hilo unalolisema la sindano litakua jambo poa sana kwa kua litawapunguzia usumbufu wa kwenda mara kwa mara kufata dawa kwenye vituo vya utoaji dawa japo inaonekana itasababisha wengi kujisahau kurudi kupiga sindano ingine maana miezi mitatu ni mingi kwa mtu anayetumia dawa.
 
Siamina katika hilo mkuu:
nchi za ulaya zinagharamia matibabu kwa raia wao na wanawapa the best ARV's zilizoko sokoni.
Wana idadi kubwa sana ya wasenge ambao ni waathirika ambao wamepigania sana haki za HIV+ kwenye society.
Kwanini wapoteze pesa nyingi kuwatibu watu hawa kama dawa ipo.
Dawa itakapotoka itatangazwa na WHO.
 
Vipi ile dawa ya pale Muhimbili tuliyoambiwa enzi zile sijui ni kina dr Pallangyo yule kama nitakuwa nimekumbuka jina sawa sawa huyu ndo aliyekuwa anasimamia huo mradi majibu yake vipi? mbona mpake leo kimya? nakumbuka zamani kulikua na dawa iltangazwa pia kama sikosei ilikua inaitwa Kemron na yenyewe vipi mpaka wa leo sijui imeishia wapi,sio vita ya biashara na makampuni makubwa ya ulaya? maana hatupati mrejesho zile tafiti zimeishia wapi?ndo maana tunaposhibishwa maneno maneno na watu hupelekea kuamini kwamba kunakua na baadhi ya mambo nchi zilizoendelea kama zinataka kufaidika nayo katika hili suala.
 
Simfahamu Dr Pallangyo, na sifahamu mengi yanayoendelea Muhimbili. Nisiingie sana kwenye siasa lakini dawa zinazotoka na ghali sana kwa mwezi kwa mgonjwa mmoja. Ukweli ni kuwa nchi za Afrika zina wagonjwa wengi sana na maambukizi yanaendelea, kumudu gharama ya dawa ni mzigo mkumbwa kwa serikali zetu. Hivyo dawa zinazopatikana kuokoa maisha ni kheri zigaiwe kwa wananchi.
 

Kwani sisi si tulikua tunapata pesa ya kutoka Global fund na Bill Gates na mkewe? na pia kama sikosei kampuni ya Smithkline Beecham pamoja na kampuni za india si zilikubali kupunguza bei kwa nchi maskini?bado mzigo ni mkubwa kwa serikali?
 
Kwani sisi si tulikua tunapata pesa ya kutoka Global fund na Bill Gates na mkewe? na pia kama sikosei kampuni ya Smithkline Beecham pamoja na kampuni za india si zilikubali kupunguza bei kwa nchi maskini?bado mzigo ni mkubwa kwa serikali?
Ni kweli mkuu, cha muhimu ni kulinda afya zetu.
 
ata dawa ikipatikana haiwezi ruhusiwa Bila who kuthibitisha mkuu haya mambo yamekaa kisiasa sana mkuu
 
Ni kweli mkuu, cha muhimu ni kulinda afya zetu.

Ni kweli hilo ndo la msingi kuliko yote, nashukuru sista kwa michango yako yenye manufaa tafadhali endelea kutu update kwa habari zaidi,usiku mwema.
 
ata dawa ikipatikana haiwezi ruhusiwa Bila who kuthibitisha mkuu haya mambo yamekaa kisiasa sana mkuu
Uzuri wake ikipatikana WHO itaangalia uwezekano wa kuisambaza kote, mwanzoni walizembea wakijua ni janga la Afrika, kumbe dunia imekua kijiji kidogo.
 
ata dawa ikipatikana haiwezi ruhusiwa Bila who kuthibitisha mkuu haya mambo yamekaa kisiasa sana mkuu
NI kweli kabisa Mkuu wao ndo wenye Mamlaka yote sema mpaka waidhinishe huwa inachukua muda mrefu sana wakati watu wanazidi kuumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…