SHERRIF ARPAIO
JF-Expert Member
- Aug 25, 2010
- 9,539
- 5,919
Nachukua fursa hii kuwakumbuka ndugu, jamaa na marafiki wote waliopoteza maisha yao kutokana na janga hili la HIV-AIDS. Toka balaa hili lilipoingia Tanzania katikati ya miaka ya 80's limeleta maafa, simanzi na uharibifu mkubwa kwenye jamii yetu. Kila mmoja wetu atakuwa kwa namna moja ama nyingine amepoteza ndugu, jamaa, marafiki, ama majirani etc.
Naomba kila mwanaJF akae kimya japo kwa dakika moja kuwakumbuka wote tuliowapoteza, tunaowajua na tusiowajua.
Vilevile tusipuuzie janga hili kwani Ukimwi bado upo na unaendelea kuua. Tuwe makini katika kuzingatia maadili na heshima. Kwa waliobahatika kuoa ama kuolewa, tafadhali kuweni waaminifu kwa wake/waume zenu. Mwenyezi Mungu atuepushe na balaa hili sisi waja wake, na tuendelee kuonyesha upendo na ukarimu na kuwasaidia waathirika wote na yatima wote bila kuwabagua.
Mungu azidi kuwabariki nyote!
RIP All Victims of HIV-AIDS!!!