HIV-AIDS Day: Mungu Awarehemu Wote Mliotutangulia

HIV-AIDS Day: Mungu Awarehemu Wote Mliotutangulia

SHERRIF ARPAIO

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2010
Posts
9,539
Reaction score
5,919
Nachukua fursa hii kuwakumbuka ndugu, jamaa na marafiki wote waliopoteza maisha yao kutokana na janga hili la HIV-AIDS. Toka balaa hili lilipoingia Tanzania katikati ya miaka ya 80's limeleta maafa, simanzi na uharibifu mkubwa kwenye jamii yetu. Kila mmoja wetu atakuwa kwa namna moja ama nyingine amepoteza ndugu, jamaa, marafiki, ama majirani etc.
Naomba kila mwanaJF akae kimya japo kwa dakika moja kuwakumbuka wote tuliowapoteza, tunaowajua na tusiowajua.
Vilevile tusipuuzie janga hili kwani Ukimwi bado upo na unaendelea kuua. Tuwe makini katika kuzingatia maadili na heshima. Kwa waliobahatika kuoa ama kuolewa, tafadhali kuweni waaminifu kwa wake/waume zenu. Mwenyezi Mungu atuepushe na balaa hili sisi waja wake, na tuendelee kuonyesha upendo na ukarimu na kuwasaidia waathirika wote na yatima wote bila kuwabagua.
Mungu azidi kuwabariki nyote!
RIP All Victims of HIV-AIDS!!!
 
Umekuja na wazo zuri,
Kweli ninao wapendwa wengi ambao walikwisha tangulia mbele za haki
kutokana na janga hili,
R.I.P. wote waliotangulia kutokana na janga la ukimwi.
 
RIP waliotangulia...
tusiwabague wenye tatizo hili, kwani lenyewe halibagui...
 
RIP waliotangulia

Mwenyezi Mungu awarehemu, mpumzike kwa amani. Amen
 
innalilah wainnahyrajghuun. mbele yao nyuma yetu. M/MUNGU atusamehe sisi na wao madhambi yetu tuliyoyayatanguliza, tunayoyajua na tusiyoyajua, TUNAMUOMBA M/MUNGU AWAPE HERI HUKO WALIKOLALA, TUNAMUOMBA PIA AWAPUNGUZIE UZITO WA KABURI. INSH ALLHA.
 
Shukrani mkuu kwa wazo zuri ubarikiwe sana. Mungu awape pumziko la milele Amen.
 
Shukrani mkuu kwa wazo zuri ubarikiwe sana. Mungu awape pumziko la milele Amen.

Nimeisoma hii thread na imenifanya niwakumbuke wengi waliotutangulia yaani kuanzia majirani, classmates, marafiki, ndugu tena wa karibu sana, duu! huu Ukimwi ni balaa. RIP
 
Back
Top Bottom