FirstLady1
JF-Expert Member
- Jul 29, 2009
- 16,789
- 5,401
- Thread starter
-
- #21
mkuu mpeleke hospitali ya wilaya yako na muulizie mteknolojia wa maabara wa wilaya au mratibu wa ukimwi wa wilaya.watampima na kuamua hatua zinazotakiwa kufuatwa.
Kuna muongozo maalum wa suala hili.
Nina wasiwasi na uelewa wa hao wahudumu wa AMREF!
Word!
Kwa hilo suala la kushinda na mtoto mmmhhhhh!...pana kazi kidogo...inabidi uwe mpole sana kwake, usije ukamkata hela za mshahara kisa kavunja glass zako, atalipiza kisasi kwa njia isiyofaa!
NEVER ON EARTH!Na kama ipo twende tukaweke records kwenye WORLD GUINNESS BOOK OF RECORDS...Nitalipia Meal and Accomodation nad Transport!
KAPIMA KWA KUTUMIA VIPIMO KAMA HIVYO AMREF
Pole FirstLady... Huu ulio nao ni mtihani. Ushauri wangu utaelemea zaidi kwa hapo nyumbani ambapo pakutia wasi... Mie naona hadi kukuambia kwake huyo binti hali yake halisi inaonesha ni walau ni kwa kiasi gani mwaishi nae vizuri, kuwa yupo huru to the extent anaweza kukuambia kitu chake nyeti kama hicho. Kama tunavyoelewa mara nyingi waathirika wa HIV/AIDS ni wasiri na hawapendi watu wajue else kama wanamuamini saana huyo mtu.
Kwa upande wa matunzo ya mtoto; from my understanding ni kuwa mtoto ni mdogo but sio mdogo sana kwa level ya uchanga... Ni hatari mtoto kuhudumiwa na muathirika kama huyo mtoto ni mdogo kuliko kama huyo mtoto mkubwa kidogo - hivo kwa kiasi fulani wasi wasi wako unaweza pungua kidogo.
Kikubwa nadhani ni bora kutumia vipimo vikubwa na katika hospitali ambayo wana kitengo cha kueleweka cha HIV/AIDS related.
Naona watu wanaconfuse vipimo vinavyotumika ktk research institutes na vipimo vinavyotumika kila siku ktk hizi hospitali zetu.Mimi naona utahangaika sana tu kuzunguka,maana hata huko utakapokwenda sidhani kama utawapangia watumie vipimo gani;wanaweza kutumia hivyo hivyo na matokeo yakatoka hayo hayo.Kwa nini usisubiri tu hiyo miezi mitatu?
Na kuhusu usalama wa mwanao siko sure 100% kama kuna risk kiasi hicho,maana hata kama atakuwa ameathirika huyu house girl hakuna mwenye uhakika wa lini hasa, maana kwa kipindi chote hicho amekuwa akimuhudumia bila tatizo.Anyway,to be in the safe side unaweza ukatafuta njia nyngine kama labda kumrudisha kijiji hadi hiyo 3 moths ipite.
On the other hand,sina hakika wewe una mtazamo gani juu ya social discrimination ya watu waishio na VVU!Maana unapokuwa unafikiria kumtenga huyu binti,usisahau kuwa wewe(kwa mtazamo wangu) ndiye mtu ambaye huyu binti amesurrender maisha yake kwako;just imagine mpaka ameona wewe ndiye mtu pekee wa kushare naye hisia alizonazo,halafu u-weigh out na impact ya kumtimua kwa kisingizio cha kusubiri miezi mitatu!
Vipi kama angekaa kimya halafu akaamua kufanya hicho tunachokutaka uamini kwamba anaweza kukifanya kwa mwanao?Naamini wewe ni mtu mzima,una maamuzi yako;na bahati nzuri umekuja humu,sio kutuomba ushauri wa nini cha kumfanya huyu binti,bali kutaka uhakika wa uwezekano wa majibu kutoka namna hiyo!
Tafakari...
Mmh wahi angaza ukajiridhishe shosti usipime mtaani, kuanza kula mashudu mapema kuna imalisha CD4
Wapendwa hebu nisaidieni juu ya hili...
Binti yangu wa kazi mwenyeji wa Sehemu za Ngara kila nikienda likizo na yeye nampa likizo...
jmos karudi toka kwao akiwa mnyonge na amepungua sana ,nikaomba kujua linalomsibu,
Bila shida akanambia dada nina tatizo
tarehe 4-1-2013 nilipima huko kwetu ikaonekana nimeathirika akaanza kupiga mayowe ..nilitaka kujiua ila mungu tu kanisaidia
Sasa naomba nisaidie twende kupima ili nihakikishe kama ni kweli maana Dr aliyenipima aliwahi kunitongoza sasa sijui labda alikuwa anatania,,nikambembeleza na kumpa maneno ya matumaini mpaka akarudi normal
Ok nikamwambia haina neno tutaenda ..nikamvutia muda
Jana tukaenda Amref akafanyiwa counceling na kumchukua damu kwa kutumia vipimo viwili ..
Kipimo cha kwanza kikaonyesha postive kingine nigative wakaitana na kuamua warudie tena majibu yakatoka vile vile
mmoja akasema hana ,mwingine akawa hana uhakika ,nimeambiwa nimrudishe baada ya miezi mitatu..
Kinachonichanganya mie naenda job asubuhi sana na kurudi jioni sana binti huyu ndo anamwandaa mtoto kwenda shule na kazi nyingine nakosa amani ingawa nimeshamwambia awe makini na kazi zake mpaka hapo atakapocheki tena
Je inawezekana ni mzima?
lakini inawezekanaje kipimo kimoja kiaonyesha postive na kingine negative??