Hivi Aliens na UFOs ni tatizo la Amerika na Ulaya Tuuu?

Hivi Aliens na UFOs ni tatizo la Amerika na Ulaya Tuuu?

Wanaukumbi,

Kwa wale wenye mazoea ya kusikiliza au kujisomea habari za UFOs (unidentified Flying Objects) au Aliens (watembezi/viumbe wanaofika hapa duniani toka sayari zingine) watakubaliana na mimi kwa kiasi kikubwa kabisa kwamba visa na matukio yanayo-ripotiwa ni kutoka ama Amerika ya kaskazini (USA na Canada) na kwa uchache kabisa Ulaya. ...

kuna UFO nyingi tu zinazunguka angani, nyingine ni kwasababu ya intelligensia ya mataifa yaliyoendelea kwa ajili za kiusalama ila watu wanatumia evidence na taarifa hizo kuwa na imagination ya vitu fulani kama sahani hizo kwenye picha.

ukumbuke UFO stands for Unidentified Flying Objects. ndege za kivita nyingi hazina identification/alama za kusomeka kwenye radar etc. Hizo pia ni UFO, ila sio hizi sahani.
 
UFO iliwahi kuonekana nchini zimbabwe kwenye shule moja ambapo ilishuhudiwa na wanafunzi baadaye katika kutoa maelezo wanafunzi wale walichora picha zikielezea walichoona ambapo ilikuwa ni sawa na yale yaliyo kwenye historia ya viumbe hao
 
hizo conspirancy ukizifuatilia sana zinaogofya.
 
Usa waliiba vitu vyote vya kale kutoka afghanistan na iraqi siku nyingi

Twambie waliiba lini maana akili zetu waafrika ni kama viongozi wetu walivyo hata umaskini tuliona nao eti ni wazungu waliuleta
 
Wanaukumbi,

Kwa wale wenye mazoea ya kusikiliza au kujisomea habari za UFOs (unidentified Flying Objects) au Aliens (watembezi/viumbe wanaofika hapa duniani toka sayari zingine) watakubaliana na mimi kwa kiasi kikubwa kabisa kwamba visa na matukio yanayo-ripotiwa ni kutoka ama Amerika ya kaskazini (USA na Canada) na kwa uchache kabisa Ulaya.

Ni nadra sana kusikia hadithi za "abductions by aliens" au UFOs landings tokea bara letu la Africa au Asia. Sasa nauliza, ni kipi kinafanya matukio haya yanajazana toka eneo moja? Ina maana hawa Aliens hawana data za kuchukua kwa wakaaji wa Africa? Ina maana hizi UFOs hazina hata haja ya kushuka kando ya Kampala au Tunduma?

Ili kuondoa taswira kuwa mada hii haina takwimu hapa chini ni muhtasari wa matukio ya UFOs kwa mwaka huu 2015. Utaona Afrika nje ya Misri na Afrika Kusini ni patupu.
Kwa takwimu hizi, Marekani na Canda peke yao wana karibu 90% ya mgawo.



Source: Worldwide UFO Sightings Up 35% Year Over Year | <b><i><a href="http://www.educatinghumanity.com">Educating Humanity</a></i></b>



Hebu Tuchangie

cc Eiyer, Mkuu wa chuo, Makanyaga, n00b, Millah, Papa Mopao, Kitty Galore, Nyambush,


pitia website hii:
www.http://whatdoesitmean.com/
 
Kwa nini Alliens Na UFO waje kwetu wakati kila siku wachawi wanapaa angani na ungo mpaka wengine wanagongana

huko huko
 
Wakiwa juu wanaona africa kama inawaka hiv mana jangwa la sahara lilivyokubwa na ukame africa kwaio wanaamua watue kwenye neema huko nje." Mawazo 2
 
nazani hamumfahamu jamaa anaitwa Monstgala hapa jukwaani
ngoja aje hapa mpate somo

.made in mby city.
 
Last edited by a moderator:
Kuhusu uwepo wa aliens hilo hatuna ushahidi wakutosha kuhitimisha iwapo viumbe hao wapo, tunapokuja kwenye simulizi za ziara za viumbe hawa kuja duniani hizi hazina ukweli wowote ni "conspiracies" tu. Vyombo visivyotambulika vipaavyo angani ni kweli vinaonekana mara kwa mara duniani kote lakini hatuwezi sema ni aliens moja kwa moja kwani ikiwa hujatambua ulichokiona basi hufahamu ulichokiona "if you don't know what you've seen, you don't know what you've seen" sasa watu wanatengeneza stori zilizojawa uwongo mwingi kuchochea au kuhalalisha mambo wasiyojua, UFO's nyingi huwa ni vifaa vya kiusalama vya majeshi,weather balloons, sometimes hata low orbiting satellites na pia atmosphere mara nyingine huweza kutengeneza illusions tu angani ambazo watu wanaweza kuzihusisha na mambo yasiyo ya sayari hii.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom