Industry ya muziki huwa iko hivyo, kila mfalme anatafutiwa mpinzani.
Na ni worldwide hii culture.
Kunakuwa na makampuni tofauti ya promotion, na ukishasign na kampuni fulani inakuwa exclusive, so makampuni shindani yanakuja na mtu wao kutaka kuweka image shindanishi.
Recently, baada ya bifu la Birdman na Lil Wayne, kiasi fulani Nicki Minaji ushawishi umepungua, +ile kuachana na Meek, means support ya Maybach pia inaondoka, sameway kwa DJ Khaled, maana ni mshkaji sana na Rick Ross.
Hivyo kumwibua Cardi B imekuwa easy sana.
Kwa wanaokumbuka, before Cardi B ngoma yake ya Bodak Yellow haijawa released, Remy Ma alikuwa na Shether (kumdis Nicki), ilipata publicity kubwa sana ila haikumshusha Nicki, nadhani image issues zinaweza kuwa ni sababu.
So kuja Cardi B na Bodak Yellow, na ukiangalia Cardi B kajaribu kujitengeneza afanane na Nicki ilikuwa rahisi sana kumpambanisha na Nicki.
Ila kadri siku zinavyoenda, Nicki anarudi kwenye chati.
Kulikuwa na tuhuma kwamba kambi ya Cardi B inawahonga DJs wasipige nyimbo za Nicki, nakumbuka kuna interview Nicki alifanya kwa DJ Ebro, walitaja baadhi ya Γ§ases za namna hiyo.
I wish promo aliyopewa Cardi B angeipata Young Ma, tungeinjoi sana muziki.