Hivi AU ina uwezo kuitisha mkutano wa nchi zake na na nchi za EU kwa agenda yake au sisi huwa tunaitwa tu kwa agenda za wakubwa?

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Kuna hii kitu unakuta nchi tajiri kama marekani, japan ufaransa, au china zinaitisha mkutano na viongozi wa afrika. Bila shaka ni kujadili agenda za maslahi kuhusu nchi hizo tajiri.

Hivi karibuni tumeona european union na wao wakiitisha mkutano na viongozi wa afrika. Sasa utaona viongozi wote hadi wagonjwa kama ali bongo wa gabon wakienda.

Tatizo ninaloliona mimi ni kwamba viongozi hawa wanaenda tu kuambiwa mpango wa bajeti ya nchi hizo tajiri kuhusu Afrika. Wanapanga kupata hiki kutoka africa kwa hivyo vikwazo vinaweza kua nini kwenye miundombinu na kathalika.

Mnaitwa kukopeshwa au kupews grant kujenga au kuelimisha watu wenu ili kufanikisha mipango yao. And then viongozi wetu wakirudi toka huko kula bata wanatuambia 'kuna vijisenti nimepata'

Viongozi wachache waliyowahi kutokea afrika wakidai kufanya yale kwa lengo la maendeleo ya nchi na watu wao wamekua wanakabiliwa na upinzani na kuitwa majina kama ni dikteta au mkiukaji wa haki za kibinadamu.

Yaani kitu wanafanya kumbe ni kuweka kipaumbele kwenye miradi ya kukomboa mchi zao kutoka utegemezi na kuwaletea wananchi wao maendeleo ya kweli.
 
Mimi binafsi sijui. Ningekuwa najua ningekujibu mkuu. Nisamehe sana.
 
Hebu fikiri kwanza ndio uchangie. Kwani afrika ni masikini au ni masikini wa fikra kama zako.
Ukishakuwa masikini wa fikra ht uwe na Malighafi ya kutosha utaendelea kuwa masikini. Hv uingereza wana Malighafi Gani mpk wawe matajiri vile
 
Maskini mwenye akili kubwa alikuwa Nyerere. Wazungu wakamwogopa walijua anakoenda ataunda vyombo vyake vya kazi na kuwa tajiri wa akili na mali. Hakupenda misaada akatafuta njia ya kujitosheleza mwenyewe. Kwa nini wao waweze sisi tusiweze?????
 
Ukishakuwa masikini wa fikra ht uwe na Malighafi ya kutosha utaendelea kuwa masikini. Hv uingereza wana Malighafi Gani mpk wawe matajiri vile
Kuna nchi nyingi duniani hawana chochote hata 1% ya tulichonacho lakini wako mbali sana tena sana. Hii kauli kila siku tunakila kitu sawa unakila kitu unafanyia nini hicho kila kitu? South Korea, Dubai( specific Dubai) Singapore sijui Hong kong na wako wengi tu hata ardhi ya kulima tu hawana lakini katizame budget zao. Je hicho kidogo unakitumiaje kujinufaisha? Denmark hawana makubwa hata Finland lakini sote tunajuwa wako wapi. Leo hii sisi tuna sehemu 100 za vituo asili vya utalii lakini sijui tunapata 1 to 2 million watalii wale Egypt wana yale ma pryamid na mwisho wa nile lakini 18 million huko wanaingia. Hakuna sera nzuri za kuvutia watu huku mtalii kuja tu nchi hii gharama kubwa sana, usafiri wa ndani gharama na hotel zetu poor service lakini gharama kubwa na baya kuliko yote gharama za mwekezaji hapa ni kubwa tax za mapato ni kubwa kupita maelezo nani aje hapa?
 
Walianza na fikra bora ikawawezesha kutumia malighafi yao vizuri kisha kwa fikra bora kwa upande wao wakatutia kwenye ukoloni na kutumia malighafi yetu kwa bei bure.
 
Kuna nchi nyingi duniani hawana chochote hata 1% ya tulichonacho lakini wako mbali sana tena sana. Hii kauli kila siku tunakila kitu sawa unakila kitu unafanyia nini hicho kila kitu? South Korea, Dubai( specific Dubai) Singapore sijui Hong kong na wako wengi tu hata ardhi ya kulima tu hawana lakini katizame budget zao. Je hicho kidogo unakitumiaje kujinufaisha? Denmark hawana makubwa hata Finland lakini sote tunajuwa wako wapi. Leo hii sisi tuna sehemu 100 za vituo asili vya utalii lakini sijui tunapata 1 to 2 million watalii wale Egypt wana yale ma pryamid na mwisho wa nile lakini 18 million huko wanaingia. Hakuna sera nzuri za kuvutia watu huku mtalii kuja tu nchi hii gharama kubwa sana, usafiri wa ndani gharama na hotel zetu poor service lakini gharama kubwa na baya kuliko yote gharama za mwekezaji hapa ni kubwa tax za mapato ni kubwa kupita maelezo nani aje hapa?
Hapa ngoja nikuamshe. Ni vizuri umetambua kua hawana kitu na bado wameendelea kuliko sisi.
Lakini ushawahi kujiuliza wanaweza kua na maisha mazuri bila sisi, kwa mfano afrika ikitoweka kwenye uso wa dunia. Ndo ujue ujinga na stupidity ya viongozi wa afrika ndo kinachosababisha ulaya waishi vizuri. Viongozi wa afrika wasipokua stupid, maisha kwa wazungu yangekua magumu kuliko hata maisha ya somalia

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Nadhani ungekuwa specific usiongelee kijumla. Miaka ya nyuma hakukuwa na biashara kubwa na nchi hizi. Sasa achana na Africa tutachanganya mambo. Hapa Tanzania nini kikubwa tunauza kwao labda kwingine duniani hakipatikani. Ongelea Tanzania tu ni tunauza kwao muhimu sana kwao. Nakuhakikishia kama kungekuwa na kitu kikubwa sana basi uneona camp yao ya kijeshi hapa.
 
Back
Top Bottom