Hivi Azam walishindwa kumuona Mgunda na kumpa timu au ndio vile hawaamini makocha wazawa?

je parle

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2018
Posts
2,022
Reaction score
3,919
Inanishangaza kumpa kumtafuta kocha mbali huko ambae hata CV yake haijulikani wakati hapa hapa ndani Kuna Makochaambao wapo na wanaweza kupanga koni vizuri.

Sote tunajua mpira wa kibongo nguvu kubwa inatumika nje ya uwanja ili timu kupata ushindi.

Na hao makocha wazawa wanajua nje ndani ligi ilivyo na njia zake.

Na pia kuna makocha wazawa wana mbinu nzuri tu na timu yao inaweza kupigania nafasi ya tatu bila shida mana ubingwa ni majaaliwa. Mgunda anawafaa kuwavusha hapo

Mbinu za huyo dabo hata Mgunda anazo zaidi ya hizo ni kwa kuwa tu Mgunda anatoka Simba labda anaweza kuwa na mahaba ya siri na Simba pamoja na Coastal Union.

Ila kwa nlivyoona Mgunga ni zaidi ya dabo wa Azam na huo ndio ukweli ndugu zangu.

Hizo Dola mnazompa Dabo ni bora mkampa Mgunda ili mzunguko wa fedha ukaishia ndani kuliko kumpa dabo na kupeleka kwao huko Magharibi.

Kingine Azam mnasajili mapro ambao hata hapa Tanzania wapo wa kutosha ni kiasi tu cha kuwaamini na kuwapa nafasi.
 
Kuvurunda wame vurunda wachezaji,kocha hapo afanye Nini,wachezaji kujituma hawataki.
 
Sawa sawa
 
Hata Julio pia angewafaa maana Azam wana wachezaji lakini 'hawana timu' wala kocha
 
hivi kwa akili yako mgunda ni kocha au mganga wa kienyeji?
 
Kwanini Simba hawakumpa Mkataba na badala yake humtumia kama backup tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…