Hivi Baadhi Ya Watanzania Wa JF (Kenyan Forums) Huwa Na Low Self-Esteem?

MwendaOmo

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2013
Posts
774
Reaction score
723
Kuna jambo ambalo hunishangaza sana katika jukwaa hili la Kenyan Forums. Kwanini watanzania wanaochangia katika Kenyan forums hupenda kuleta development projects za Tanzania kanita forum hii? Kwani ni affirmation wanatafuta au nini?

Tanzanian sub-forums zimejaa tele. Au ni kwasababu waTZ wenzao watawanyamazisha na hizo projects hewa?

Ni kwanini habari nzuri za kenya zikija kunao watakao kuja na mada tofauti ya "Hata sisi tunayo?" Huu si utoto jameni? Si semi ni wote, bali idadi kubwa
 
kwa sababu nyie wakenya mnapenda kujikweza huku uhalisia hamna tofauti yoyote na mataifa mengine ya kiafrika

Sasa unapofanya utoto wa "me too", ni nini unachotusaidia nacho? Kuna haja gani ya kuweka projects za TZ humu ilhali Jukwa la Siasa liko very active kule kwenu ingawa huwa sioni chochote wanachoongea apart from CHADEMA this CCM that? Kwanini msipeleke mada za Maendeleo kule?

Ikiwa mtu amesema jambo ambalo ni la uwongo, si basi umkosoe kwa lile ambalo amesema?

mulisaaa
 
You have point, hata mimi nimekuwa najiuliza sana na kuna wakati niliwahi kuuliza; 'kwanini habari za Tanzania (zisizoihusu kabisa Kenya ziletwe jukwaa la Kenya?'. Ila nadhani wanafanya hivi kwa sababu ya LIGI zenu zisizoisha za Tanzania VS Kenya... kwa sababu hata Wakenya kwenye Kenyan Forums hawaachi kuitaja Tanzania (hata kama haihusiki) kila wanapoposti habari za maendeleo yao. Hivyo usiangalie upande mmoja tu. This is madness at all...
 
Wakenya kweli mna mambo. Haya wasalimieni Kangemi.
 
yaani umesema ukweli kabisa mkuu...watanzania wengi huwa na tabia ya kuleta habari zisizohusu kenya humu ili muradi tu wazue debate na matusi kati yao na wakenya....mara nyingi wanaleta tz news kwa Kenyan news and politics....pia wana tabia ya kuleta habari mbaya toka Kenya humu...sijui wana ugonjwa ipi hawa...mtu ana rauka 6AM kutafta habari za Kenya toka Google kisha anaruka makusudi zile za good news akisaka zile mbaya mbaya...pengine ni unemployment na inferiority complex....lol!...

mkenya akileta habari za skyscrapers Nairobi, mtanzania analeta habari za Kibera....mkenya akileta za uchumi, mtz analeta za cooking data....yaani ni tabia mbaya sana...inaonyesha kuwa watz wengi wanashuku maendeleo yao na kuskilia Kenya wivu....I mean, is it difficult to say congratulations Kenyans for the development? Must you now bring tanzanian news in this forum so that you feel better?

ila pia siwezi walaumu sana sababu Wakenya wachache sana ndio huwa wanaenda kule ktk jukwaa la siasa ama thread zingine za kitz...wengi hawajishugulishi...sasa ni lazma walete Kenyan News ndio wapate replies za wakenya...

watz hawa ndio wanahusika zaidi
Geza,Kilam,Mwanzi, Mulisaa...ila kuna wengi tu wana tabia hizi za kitoto...
 
Kwahiyo hata hii nisikuletee?? Mbona Kenya kwenye hii list haipo kabisa. Hii nikuwa Tullow Oil ilikufa kabisa. kuweni wanaume face the challenge. Sio mnalialia kama demu.
 
Baadhi ya sababu ni hizi zifuatazo wala sio hiyo yako uliotaja!
1; Tabia ya wakenya kupenda kuleta habari za kujisifia kuliko uhalisia wenyewe!

2; Tabia ya wakenya kupenda kuleta habari za kuiponda tz.


3; Tabia ya wakenya kutoonekana kwenye majukwaa yanayoongelea habari za tz!

4; Ushindani iliopo baina ya nchi hizi mbili!


My take!

Kama suala hili linakukera sana, nenda jukwaa la pongezi, ushauri na malalamiko waombe mods waweke jukwaa la habari mchanganyiko za tz na kenya. Wakifanya hivyo nadhani hutatuona hapa maana hilo jukwaa naamini litakuwa vibrant kweli kweli!

Kama sio hivyo basi tutabanana hapa hapa maana hakuna namna sasa!
Ni sawa na wakenya wenzio wanapost hapa habari za mataifa mengine wakati lipo jukwaa la kimataifa.
 
chunga usije ukaugua maradhi ya moyo maana hatutoisha kujisifia
 
Baadhi ya sababu ni hizi zifuatazo wala sio hiyo yako uliotaja!

1; Tabia ya wakenya kupenda kuleta habari za kujisifia kuliko uhalisia wenyewe!

Hii ni Kenyan forum; ikiwa kuna kasoro au uwongo kwa chochote kisemwacho, basi pinga ukizingatia mada iliyopo. Nikija niseme Kenya inatoa maziwa mengi duniani nzima, nipinge kwa data ikiwa unaona ni uwongo. Lakini usije ukasema Tanzania inatoa mchele mingi duniani nzima. Huo ni kutoelewa mada na unadhihirisha elimu duni.

2; Tabia ya wakenya kupenda kuleta habari za kuiponda tz.

Ikiwa nia tu ni kuleta ubishi kati wa TZ vs KE, huo ni utoto pia. Lakini, kuna wakati mwingine mada huletwa hapa kwa ajili ya analysis. Kwa mfano, Kama Wakenya, tunaona nini kuhusu uongozi wa Magufuli? Kuna wale ambao wanaisupport na kuna wale ambao wanaipinga. Kama tu vile kwenye Jukwa la Siasa huwa na mada kuhusu uchaguzi wa Kenya na Katiba ya Kenya. Sio eti mnaiponda Kenya, bali ni kuanalyze aina ya katiba na siasa kwa macho ya mtanzania. Ni upuuzi mie kama mkenya kupeleka mada za kikenya kwenye Jukwaa la Kisiasa

3; Tabia ya wakenya kutoonekana kwenye majukwaa yanayoongelea habari za tz!

Mtu huenda kwenye majukwaa ambayo humfurahisha, ndio sababu hizi jukwa zilikuwa divided. Kilichonileta katika JF, ni Jukwaa la Lugha, na baadaye Jukwaa la Elimu. Nilidhani ya kuwa nitapata majadiliano ambayo yatafanana na zile nyuzi nilizozipata mtandaoni na amabazo zilinileta JF. Kilichoniudhi nilipata wengi tu michango zao ni za kitoto, kana kwamba wachangiaji wa hapo awali walishatoweka. Sub-forum ya kuchekesha ni ya mapenzi.

Kingine ni kuwa wengi hutemebelea majukwaa mengi ya TZ yakiwemo ya kisiasa lakini hatuwezi kucomment kwa kuwa tunajua vizuri sana hatuko informed ukilinganisha na wabongo wenyewe. Sina la kuwafunza kule; ni kujielimisha tu.

4; Ushindani iliopo baina ya nchi hizi mbili!

Wale wanaofanya mataifa haya mawili kushindana hawamo JF. Ni wanasiasa na watu wakubwa wenye kuamsha skyscrapper. Humu JF ni pahala pa kujielimisha na kutafuta njia ya kujindeleza maisha yetu. Haya mabishano ya JF ni ya wananchi wa kawaida ambao kila siku twajiuliza jinsi tutakavyolipa kodi ya nyumba na karo. Haina maana mie kujigamba kuhusu skyscrapper ambazo hata kazi ya mjengo sipati.


Asante Kwa mchango wako. Nitakwenda kule nipeleke malamishi yangu kuwa TZ news zibaki kwenye Jukwaa la kisiasa au Biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…