Baadhi ya sababu ni hizi zifuatazo wala sio hiyo yako uliotaja!
1; Tabia ya wakenya kupenda kuleta habari za kujisifia kuliko uhalisia wenyewe!
Hii ni Kenyan forum; ikiwa kuna kasoro au uwongo kwa chochote kisemwacho, basi pinga ukizingatia mada iliyopo. Nikija niseme Kenya inatoa maziwa mengi duniani nzima, nipinge kwa data ikiwa unaona ni uwongo. Lakini usije ukasema Tanzania inatoa mchele mingi duniani nzima. Huo ni kutoelewa mada na unadhihirisha elimu duni.
2; Tabia ya wakenya kupenda kuleta habari za kuiponda tz.
Ikiwa nia tu ni kuleta ubishi kati wa TZ vs KE, huo ni utoto pia. Lakini, kuna wakati mwingine mada huletwa hapa kwa ajili ya analysis. Kwa mfano, Kama Wakenya, tunaona nini kuhusu uongozi wa Magufuli? Kuna wale ambao wanaisupport na kuna wale ambao wanaipinga. Kama tu vile kwenye Jukwa la Siasa huwa na mada kuhusu uchaguzi wa Kenya na Katiba ya Kenya. Sio eti mnaiponda Kenya, bali ni kuanalyze aina ya katiba na siasa kwa macho ya mtanzania. Ni upuuzi mie kama mkenya kupeleka mada za kikenya kwenye Jukwaa la Kisiasa
3; Tabia ya wakenya kutoonekana kwenye majukwaa yanayoongelea habari za tz!
Mtu huenda kwenye majukwaa ambayo humfurahisha, ndio sababu hizi jukwa zilikuwa divided. Kilichonileta katika JF, ni Jukwaa la Lugha, na baadaye Jukwaa la Elimu. Nilidhani ya kuwa nitapata majadiliano ambayo yatafanana na zile nyuzi nilizozipata mtandaoni na amabazo zilinileta JF. Kilichoniudhi nilipata wengi tu michango zao ni za kitoto, kana kwamba wachangiaji wa hapo awali walishatoweka. Sub-forum ya kuchekesha ni ya mapenzi.
Kingine ni kuwa wengi hutemebelea majukwaa mengi ya TZ yakiwemo ya kisiasa lakini hatuwezi kucomment kwa kuwa tunajua vizuri sana hatuko informed ukilinganisha na wabongo wenyewe. Sina la kuwafunza kule; ni kujielimisha tu.
4; Ushindani iliopo baina ya nchi hizi mbili!
Wale wanaofanya mataifa haya mawili kushindana hawamo JF. Ni wanasiasa na watu wakubwa wenye kuamsha skyscrapper. Humu JF ni pahala pa kujielimisha na kutafuta njia ya kujindeleza maisha yetu. Haya mabishano ya JF ni ya wananchi wa kawaida ambao kila siku twajiuliza jinsi tutakavyolipa kodi ya nyumba na karo. Haina maana mie kujigamba kuhusu skyscrapper ambazo hata kazi ya mjengo sipati.
My take!
Kama suala hili linakukera sana, nenda jukwaa la pongezi, ushauri na malalamiko waombe mods waweke jukwaa la habari mchanganyiko za tz na kenya. Wakifanya hivyo nadhani hutatuona hapa maana hilo jukwaa naamini litakuwa vibrant kweli kweli!
Kama sio hivyo basi tutabanana hapa hapa maana hakuna namna sasa!
Ni sawa na wakenya wenzio wanapost hapa habari za mataifa mengine wakati lipo jukwaa la kimataifa.
Asante Kwa mchango wako. Nitakwenda kule nipeleke malamishi yangu kuwa TZ news zibaki kwenye Jukwaa la kisiasa au Biashara.