Hivi bado kuna kuibiwa hela ndani siku hizi?

Masulupwete

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2012
Posts
2,366
Reaction score
2,424
Wakuu kuna jirani hapa anadai wezi wamevunja kwake wameingia ndani na kuondoka na pesa.

Mimi sishangazwi na huo uvunjaji wala wizi wenyewe kinachonishangaza ni ishu ya wezi kuzikuta hela ndani unapolala. Hivi wakati huu wa mabenki, sakosi, vikoba na ma-mpesa kama yote bado kuna watu wanakaa na mabunda ya hela ndani?
 
Hili jina lako ndio tatizo lilipoanzia huwezi kuelewa. Kavae masulupwete yako uendelee na masulupwete yako mambo ya watu utaendelea kuyaona ni masulupwete tu

Jumatatu njema bwana masulupwete
[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Njoo Tandahimba, Mahuta na Newala, watu wanakaa na pesa ndani tena miizigo kweli, hawaamini kwenye taasisi,
 
... sio kwamba hiyo ndio ilikuwa salama yake? Ukiwa na hela hakikisha unawawekea kiasi fulani ndani ili wakija uwakabidhi ubaki salama. Kwa sisi makapuku hii haituhusu.
Hata ukiwakabidhi still awatoamini ndo pekee ulizonazo
 
Bank ukiweka mzigo wakati wa kuchukua hela ni yako ila viziwizi ni vingi na maswali ni mengi, wewe ni bwana mdogo huwezi kuelewa
 
Ni kawaida hujui miamala ina makato
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…