Hivi bado tupo nyuma kiasi hicho?

Hivi bado tupo nyuma kiasi hicho?

Mzee Saliboko

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2018
Posts
1,311
Reaction score
1,018
Bado na hoja kuhusu Hamza yule yule waliosema ni gaidi.

Hoja sio hiyo bali najiuliza hivi tupo nyuma kiasi hicho mtu mmoja kusumbua kikosi kizima cha polisi kilichopelekwa pale? Hatuna technology kiasi hicho?

Kwanini walihangaika kumlamba shaba badala ya kumchoma sindano ya usingizi au ya kumaliza nguvu palepale, kwanini hawakutumia wadunguaji waka mlamba shaba sehemu muhimu bila kufa? Kuna majengo marefu pale ya kukaa position nzuri tu.

Vipi kuhusu counter attack, net au vinginevyo. Bado najiuliza tu🤔🤔 kama mtu mmoja tu alisumbua hivyo vipi kama.......
 
Ukiondoa mawazo ya filamu kichwani mwako utaelewa kwanini alipgwa risasi.

Hii hutokea karibia dunia nzima, watu wengi waliofanya matukio kama ya Hamza waliuliwa hapohapo eneo la tukio, ni mara chache sana kusikia wamekamatwa wakiwa hai.

Fatilia matukio yenye ufanano na tukio la Hamza haswa Marekani, nahisi ndiko kuna matukio mengi ya kariba hiyo, utabaini washukiwa wengi huwa wanauawa eneo la tukio.
 
Ukiondoa mawazo ya filamu kichwani mwako utaelewa kwanini alipgwa risasi....
Ushahidi wa kimazingira unaonyesha hakuwa na nia ya kuua mtu mpaka pale polisi walipofika......sasa utapataje evidence ya nia yake huku umemuua?
 
Ushahidi wa kimazingira unaonyesha hakuwa na nia ya kuua mtu mpaka pale polisi walipofika......sasa utapataje evidence ya nia yake huku umemuua?
Hakuwa na nia wakati alikuwa keshaua Askari na akachukua siraha kabla hajasogea ubalozini?? Kama hakuwa na nia alichukua siraha kwajili ya nini??? Kujiremba??? Kupiga nayo picha???

Mzee usicheze na mtu mwenye siraha, hizo nadharia unazozisema hata kwa wenzetu walioendelea wanazitumia kwa kiwango kidogo sana na wananyenzo za kisasa kudeal na waharifu sembuse sisi??
 
Back
Top Bottom