Hivi biashara ya mayai ya kware iliishia wapi jamani?

Dah ile heading ukiisoma ilikuwa inazuzua hatari,

"... Biashara yenye utajiri ambayo hakuna bank itataka uijue.. "
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji119]

Bahati mbaya sikuwa na hela kipindi hicho nahic nngeunguzaga account aisee
hahahaaa mimi ile heading ndio iliyonifnya niiogope biashara yenyewe sasa ..maana niliona mmhh ukiona mtu anakupa mchongo mzito kama huu kiboya boya tu jua kuna namna
 
Hahaha nimecheka sana aisee.

Sijui ilikuwa project ya mjanja gani ile.

Watu walifuga sana kware.

Bila kusahau biashara ya sungura pia, nayo ilishika kasi sana, sijui bado ipo?
HIYO NIASHARA YA SUNGURA WATU WAMEPIGA HELA MNOOO...KUNA JAMAA FLANI HVI WANAPATIKANA SINZA MAENEO YA UWANJA WA TIPI ..WALIKUWA WAMEPEWA TENDA YAKUTENGENEZA MA CAGE yA KISASA KABISAAA KWAAJILI YA SUNGURA..DAAHH JAMAA ALIKIWA ANAYAUZA ILE MBAYA
 
hahaaa hii kitu ikoje mkuu ..hebu idadavue vyema..daahh watu wezi aisee
 
Hahahaha nyie watu wakorofi hahahaha
sasa hivi analiingiza kingi taifa ...sasa mtu mwenye akili zakushikiwa mpka na babu wa loliondo eti kapewa nchi aiongoze ...hahaaa tanzania kuna miujiza aisee ..acha atuuze tu
 
Jiji la Dar likitaka kumaliza tatizo la Kunguru Makonda atangaze..."nyama ya kunguru inamaliza tatizo la nguvu za kiume"

Ndani ya mwezi mmoja tuuu, kunguru wote kwishaa
 
unganisha na biashara ya kuku wa kuchi, na kikombe cha babu wa loliondo, vyote hivyo vinaendana, ni dugu moja.
Ufugaji wa mbuzi wa maziwa, ufugaji wa sungura, kilimo cha Uyoga na kilimo cha matikiti maji
Vyote vilikuja kama upepo na kuondoka kama upepo
 
Ufugaji wa mbuzi wa maziwa, ufugaji wa sungura, kilimo cha Uyoga na kilimo cha matikiti maji
Vyote vilikuja kama upepo na kuondoka kama upepo
afadhali ya matikiti maji ..nizao ambalo demand yake kwa wateja waiona kwa macho mpka hii leo...hivyo vitu vingine ni imagination
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…