Acha tu mkuu ,, hii mambo unaenda unatoa laki5 na 60 , zen unapewa package ina dawa eti inatibu "magonjwa 100" ,pia ina kahawa inayoongeza 'akili darasani',unapewa pia dawa za mswaki kwenye hiyo hiyo package, ambayo thamani ya package ndio hiyo pesa uliyotoa…!
Sasa hiyo package ni wew uende kuuza au ukatumie mwenyewe kwa afya yako, zen unatafuta watu wa kuwajoin kwenye biashara , basi mambo yanakua yameiva unaanza kuingiza pesa na wewe kupitia chain ya watu uliowaunganisha
Jamaa wahuni sana , ukienda kwenye semina zao wanaongelea kununua magari na viwanja ndani ya miezi miwili
Mimi nimefatwa na washikaji zaidi ya wawili kuhusu hiyo makitu bt niliwaambia ujinga wa hivo sifanyagi