Hivi Bisi Ni Salama?

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2010
Posts
4,290
Reaction score
2,468
Hizi Bisi Ni Maarufu Sana Manjiani Na Kwenye Kumbi Za Sinema. Nauliza Hivi Maana Kama Mahindi Ya Kawaida Leo Yamekuwa Hatari Katika Kutengeneza Unga Wa Dona Kutokana Na Kuvu, Hizi Bisi Hazina Kemikali?
 
Chumvi inayowekwa Kwenye Bisi(pop corn) si salama kwa Watu wenye pressure

Na Si salama Kwa Watu Wasio na Pressure inaweza Kusababisha Upressure Pia
 
sijawahi kuzipenda BISI,zinachafua meno!
 
Ziko Ambazo Hutengenezwa Bila Chumvi
 
Mahindi huwa yanahifadhiwa na madawa ya kuzuia wadudu, huwa najiuliza kama kweli mahindi yale huoshwa vizuri kabla ya kuingizwa kwenye mashine ya bisi.
 
Hizi Bisi Ni Maarufu Sana Manjiani Na Kwenye Kumbi Za Sinema. Nauliza Hivi Maana Kama Mahindi Ya Kawaida Leo Yamekuwa Hatari Katika Kutengeneza Unga Wa Dona Kutokana Na Kuvu, Hizi Bisi Hazina Kemikali?
Bisi ni dawa pia
 
Yawezekana ikawa dawa lakini zikawa na sumu kwa kuwa hazioshwi kabla ya kutengenezwa
Cha muhimu tujue temperature ya kupasua hilo hindi linakuwa nyuzi ngapi na hiyo dawa kama inaendelea kubaki kwenye hiyo bisi ni vizuri wataalamu wakatusaidia
 
Cha muhimu tujue temperature ya kupasua hilo hindi linakuwa nyuzi ngapi na hiyo dawa kama inaendelea kubaki kwenye hiyo bisi ni vizuri wataalamu wakatusaidia
Hivi kemikali inauliwa kwa joto? Sikujua aisee
 
Mahindi huwa yanahifadhiwa na madawa ya kuzuia wadudu, huwa najiuliza kama kweli mahindi yale huoshwa vizuri kabla ya kuingizwa kwenye mashine ya bisi.

Mkuu nafanya hiyo biashara, yale mahindi huwa yanauzwa supermarket yako sealed kwenye mifuko ya 20 kg huwezi kukuta wadudu au yamebunguliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…