Hivi Bongo Muvi wana Shida gani hawa watu?

Hivi Bongo Muvi wana Shida gani hawa watu?

Kacheza filamu na rammy galis aliyekuwa mpenzi wake ambayo haijatoka bado...inaitwa HUKUMU
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Mungu anisamehe jamani ila haka kamtu nakaona kama kanafiki sana..na mwenzake McPilipili.
Watu wafupi na wasio na nyama n matatizo matupu ref. Pole pole[emoji5]
 
Mtazamo wangu
1. Sijaona ubaya bongo movie kuungana katika msiba wa marehemu Masogange hata kama hajaigiza movie yoyote,huko tunaita kujumuika kijamii(socialize) kama hujui maana uliza usaidiwe.Ndio maana hata katika misiba yetu sis tulioko kitaani ukifiwa majirani huja msibani je wale ni ndugu zako wa damu? je wanajipendekeza au wanakuja kukufariji?
2. Tuache kujidai wajuaji katika mambo ambayo yametuzidi kimo.Tuwe na akiba ya maneno,kuongea sana sio kuzuri.
3. Kwa desturi ya mwanadamu pindi binadamu mwenzetu anapofariki tulio hai tuna mafunzo ya kujifunza na kukumbuka kwamba duniani tupo kwa msimu tu kwa hiyo pumzi uliyonayo isikufanye ujifarague kwamba wewe ni bora kuliko aliyekufa wakati ni wewe ni marehemu mtarajiwa,isitoshe kati yetu hakuna ajuaye kifo chake kitakujaje.

Asante
Kaigiza movie moja na ramy
 
Siku hizi hawatoi movie mpya wamebakiza kujichoresha kwenye misiba, na pia yule mc pilipili nahisi kama sio utoto ana mtindio wa ubongo kwa nilichoona anafanya kwa kujirekodi selfie na mtoto wa marehem
 
Back
Top Bottom