Hivi Bongo muvi zinafunza jamii au zinabomoa?

Hivi Bongo muvi zinafunza jamii au zinabomoa?

Ninashindwa kuelewa connection iliyoko kati ya bongo movie na magazeti ya Shigongo. Wapenzi wake ni wa aina moja, wadada wa baa, beki 3 wengine ni wale waliopata bahati ya ajira katia maofisi na taasisi za serikali ambao majukumu yao yakiisha wanasoma mageziti.
 
kwa kweli sio nzuri zinaleta mambo mabaya sana kwa watoto....
Zinaharibu watoto
Bongo mavi weka mbali na watoto
Kama unawapenda
wote mliochangia kuusu uharibifu wa filamu hizi kwa watoto na jamii nawaunga mkono kabisa, tasnia hii imevamiwa na kuzimu ni uchafu mtupu wanaolishwa watu na hawa watumishi wa shetani.

Mimi nimepiga marufuku nyumbani juu ya filamu hizi na bongo fleva zinazojaza watu mapepo.

Angalia ndugu uliyeomba ushauri usijeshitukia umevuna mabua. Ukakuta tayari mkeo na watoto wameshalishwa Matango Mwitu.
 
Sio mpenzi kabisa kabsaaaa wa hizi muvi za bongo wala Naijeria.

Ila hapa hom mda wote nikienda nikirudi mke na watoto nakuta wameconcetrate [emoji15] hadi wanaunguza chakula.

Sababu sio mpenz wa hizo muvi me nikifika hom nachukua laptop naingia JF maana ndio burdani yangu ingawa kuna vilaza huku wengine wanaharibu maadili ila kwa kusoma huwezi kuharibika km kutazama muvi.

Hivi nnavyowaachia huo uhuru wa kutazama na kujiachia zinawajenga au kuwaharibu ili nipige block channel za kibongo muvi.
hazifai mzeya.. hata kama huangalii kwani husikii mbabu.. bongo moviez ni bongo lala.. kuna dogo mmoja(wakiume) alikua anapenda sana ile muvi ya SHOGA.. kila mara alikua anapenda kuitizama.. daaah mpaka leo wadau wanajilia kiboga.. ukiwa na pesa yako unajipigia mzigo so kuwa makini sana weka mbali na watotozzz..
 
Sijawai kuona muvi mbovu dunian kama za kibongo muvi haina mshike mshike hata kidogo ni mapenzi mwanzo mwisho vijitu kazi kuiga iga kingereza hawajui ata tense, subtitles ndo aibu.
Mavazi ovyoo sisi tuna dhamira nyingi sana kwenye mazingira yetu kama rushwa, unyanyasaji wa kijinsia, ugomvi, ndoa za mitara, tohara kwa wanawake, magonjwa, ajali, chuki, wivu wa maendeleo, uchawi, ujinga, umasikini, umoja, amani lakini wao huigiza mapenzi tu, seenziiiiiii
 
Industry yenyewe imejaa walaaniwa tu, wataifunza jamii mambo gani mazuri? Wanatajirika wasanii wa kike tu, kutokana na kale kabiashara kao ka ziada.
 
Piga ban hao na hizo bongo movie zao, zinaharibu watoto wanakuwa wajinga, mimi mpwa wangu nimempiga marufuku bongo movie na zaidi kabisa za Nigeria, akitaka aangalie za wahindi, wafilipino na wazungu
 
Back
Top Bottom