Hivi Cardinal Pengo ni Mtanzania?

 
Burabura:

Hivi unajuwa Pope ni kiongozi wa hanisa katoliki Duniani na kiongozi wa nchi...?

Usijaribu kuingiza hoja mbadala zenye nia ya ku-confuse na kuondoa attention kwenye maswali ya msingi niliyokuuliza. Jibu maswali!

Je tanzania kuna ubalozi na mwakilishi wa holy see au wa Vatican?

Jibu ni: Tanzania ina Mwakilishi wa Holy See, aka APOSTOLIC NUNCIATURE OF THE HOLY SEE
 

Hii ni hoja ya kijinga. Unaileta kwa sababu Pengo amesema Kanisa halitaacha kupinga ufisadi kwa vile ufisadi ni uovu. Na kuwa mkuu wa ufisadi ni ibilisi. Kwa nini haukusema Kadinari Rugambwa hakuwa Mtanzania. Kwa hiyo hutaki afanye kazi yake ya kukemea uovu. Huu ni upuuzi. Uleule wa CCM kusema Kambona hakuwa Mtanzania.
 
 
Last edited:
Ameomba kutoa hoja na sisi tunamtukana nadhani hapo tunakosea.

aelimishwe huyu kwani tukimtibua na swaumu yake atazidi kuwa zaidi ya alivyo sasa

wenye kujua kuelimisha mpeni darasa dogo ili next time asije akajamba mbele ya wakubwa
 
Kwa hiyo unaulizia uraia wa Pengo kwa sababu unapinga waraka? Haupingwi hapa kwa sababu unapinga waraka bali kwa sababu hoja yako haina mantik.

Mkatoliki yeyote anaweza kuteuliwa ( uPapa haugombewi) kuwa Papa, si lazima awe askofu au kadinali.

Hiyo red ni uongo mkubwa sana na inabidii tuukemee sana SHINDWA, SHINDWA. NA ULEGEE MPAKA SEHEMU ZAKO ZA SIRI.
Ina maana wakatoliki mlikusanyika pale Holy see kuchagua Pope? Usitake kuongopea watu hapa we Fundi Mchundo.

Pope anachaguliwa miongoni mwa makadinari tu na si vinginevyo. Na wawakilishi wao kwenye nchi mbalimbali lazima wawe maaskofu na sio mapadre.

kama itakuwa Mkatoliki yeyote anaweza kuwa Pope. basi tungepata Pope mwenye mke. Kwani ni maaskofu, mapadre tu katika ukatoliki hawaruhusiwi kuoa lakini waumini wanaruhusiwa kuoa.

Vile vile nilieleta bandiko ni mimi na sio Barubaru. Soma vizuri usikurupuke
 
.

Nasubiri Jibu barubaru kwani inaelekea wengi hatujui elimu za Uraia hapa. Tupe darsa
 
Ameomba kutoa hoja na sisi tunamtukana nadhani hapo tunakosea.

aelimishwe huyu kwani tukimtibua na swaumu yake atazidi kuwa zaidi ya alivyo sasa

wenye kujua kuelimisha mpeni darasa dogo ili next time asije akajamba mbele ya wakubwa
.

haya ndio maneno MSANII.

Hakika wengi wa watu hapa ni wale wasiozingatia ukweli na uhuru wa kutoa mawazo. wao wanakalia kutukana tu bila kuwa na mashiko.

lakini tumewazoea na tunajua janja yao. Kwa suala hili NI LAZIMA KIELEWEKE
 
kwa wakatoliki na wasio wakatoliki ni kweli kuwa polkarp kardinal pengo ana urai wa nchi mbili yaani vatican state na tanzania, kuna mikataba mingi ya kuhusu vatican state au holy see, leo nina haraka nitaweka bandiko hapa kumjibu mwenye hoja
.

Mwakimbi nazidi kuvuta subra kusubiri jibu. Kwani wahenga wamenena subra yavuta heri.

nakusubiri mkuu
 

Niliishakushauri kuwa uache uvivu. Google iko kwa ajili ya watu kama wewe. Ingawa mwanzo uteuzi wa Pope ulifanyika kutoka miongoni mwa makadinali lakini sasa hivi yeyote anaweza kuchaguliwa kuwa Papa. Ikiwa mtu asiye kadinali anateuliwa basi anapewa uaskofu kabla ya kukalia kiti cha upapa. Katika uteuzi uliopita palikuwa na tetesi kuwa wangeweza kuteua mtu asiye kadinali. Hii haikutokea lakini inawezekana. Kwa vile ni jopo la makadinali ndilo linalofanya uteuzi hakuna mahali ambapo wanalazimishwa kumteua mtu miongoni mwao. Imani yao ni kuwa uteuzi huo unaongozwa na mwenyezi Mungu kwa hiyo hawawezi kumlazimisha mwenyezi awachagulie mtu kutoka miongoni mwao tu! Ukumbuke kuwa kila nchi ina mfumo wake wa kuchagua kiongozi wake. Nchi nyingine anapigiwa kura na wananchi wote waliotimiza masharti ya kupiga kura. Nchi nyingine ni kiongozi wa chama kilichopata wabunge wengi zaidi ( Uingereza haikumpigia kura Brown kuwa waziri Mkuu), nchi nyingine ni wabunge wanaompigia kura rais. Hakuna standard. Kila nchi huru inajiamulia. Concept ambayo nadhani kwako ni vigumu kuelewa.

Mahali ambapo ungeweza kunisahihisha ni kuniambia kuwa wakatoliki wakike hawawezi kuchaguliwa kuwa Papa kwa vile kanisa katoliki halina mapdri wa kike. Kuhusu kuteuliwa mkatoliki mwenye mke hilo (theoretically kama ilivyo nchini mwetu mwanamke na raia asiye mweusi anaweza kuchaguliwa kuwa rais) linawezekana kama vile ambavyo mapadri wakianglikana walivyokubaliwa kujiunga na ukatoliki bila kutaliki wake zao.

Sehemu zangu za siri zinakuhusu nini? Unajuaje kuwa hazijalegea bado?

Kwangu hamna tofauti. Wewe na Barubaru ni walewale.

Amandla.........
 
Last edited:
.

Semilong je wewe unaweza kugombea kuwa waziri mkuu wa UK.

Elewa haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika uongozi wa juu.

Wewe unaongelea kuchagua na si kuchaguliwa. tafakari hilo.
nikiomba urai wa UK na kupewa basi naweza kugombea (hii itatokana na sheria za UK zinasemaje kuhusu watu waliokuja)
governer wa califonia si ni raia wa austria, na alivyopata uraia wa marekani akagombea u-governer
wewe ndio utafakari vitu unavyoandika, umetolewa mifano kibao hapo juu lakini utaki kuelewa

mfano uliotokea TZ kipindi cha nyuma - marehemu (mzee wa makondeko) alikuwa anaiwakilisha nchi ndani ya TZ wakati yeye ni mTZ
 

Kwa upande mmoja Zee la Kufuturisha, HM Hafif hajakosea kwa kudai kuwa ni Makadinali tu wanaweza kuteuliwa kuwa Papa.

Whatever Canon Law may suggest about who may qualify to be elected as Pope: for all practical purposes, chance ya asiye Kadinali kuwa Papa ni ndogo sana, na chance ya Mlei kuwa Papa ni virtually non-existent.
 

Ni kama vile ilivyo kwa Kadinali mwafrika kuwa Papa (pengine sio kwa kiwango hicho hicho). Tatizo ni hawa jamaa kutumia uwezekano huo kuwa moja ya vigezo vya kusema Pengo si Mtanzania! Tukumbuke kuwa pamekuwepo maPapa wachache mno wasio waitaliano. Hivi sasa inakubalika wakitoka nje ya Italia lakini naamini itachukua muda kupatikana asie mzungu. Si kwa vile ni wabaguzi lakini wingi wao katika nafasi za uongozi ndio unawapa nafasi zaidi. Itakuja siku atakuwepo Papa mweusi lakini bado. Kumhukumu Pengo ati kwa vile anapiga kura au theoretically anaweza kupigiwa kura kuwa Papa si kumtendea haki.

Amandla........
 

Sawa kabisa! takbiru alaa walibalu!
 

Hawa jamaa ni wavivu. Jamaa anadai kuwa haiwezekani m-lei kuwa Papa kwa sababu mtu aliyeoa hawezi kuwa Kadinali. Canon Law haikatazi mtu aliyeoa kuingia kwenye upadiri. Kinachokatazwa ni kuoa baada ya kuwa Padri. Hiyo hapo ni orodha ya mapapa waliokuwa wameoa kabla ya kuwa mapadri. Celibacy ni kwa mtu asiyeoa na aliyeingia kwenye upadri au utawa.

Amandla......
 

Bluray, I like your reasoning! What the guy has said is what I call "intellectual masturbation."
 
Kama nilivyo kuahidi Bro HM Hafif nitachambua kidogo Kutoka katiba ya JM Tanzania kuhusu sifa za kiongozi wa juu yaani Rais na haki za kupiga kura. Tukiangalia Uchaguzi wa Rais Sheria ya 15 ya mwaka 1984, Ibara ya 19 inasema
'
38​
.-(1) Rais atachaguliwa na wananchi kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii na kwa mujibu wa sheria itakayoweka

masharti kuhusu uchaguzi wa Rais ambayo itatungwa na Bunge kwa kufuata masharti ya katiba hii''

Na Sifa za mtu kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania Sheria ya 4 ya mwaka 1992,Sheria ya 13 ya mwaka 1994,Sheria ya 34 ya mwaka 1994 na sheria ya 3 ibara ya 7 ya mwaka 2000 zinabainisha kuwa

39​
.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa
Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa
mujibu wa Sheria ya Uraia.
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe
wa Baraza la Wawakilishi,
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika
Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa

kodi yoyote ya Serikali.


Sasa utaona hizo ni sifa za Mtu kuweza kuchaguliwa kugombea uongozi wa juu ndani ya Tanzania.

Kwa haraka haraka tuiangalie tene katiba ya JM wa TZ inasemaje kuhusu haki ya kupiga kura sheria ya 15 ya mwaka 1984 ibara ya 6 na sheria ya 3 ya mwaka 2000 ibara ya 4

5​
.-(1) Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka
kumi na minane anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi
unaofaywa Tanzania na wananchi. Na haki hii itatumiwa kwa
kufuata masharti ya ibara ndogo ya (2) pamoja na masharti
mengineyo ya Katiba hii na ya Sheria inayotumika nchini
Tanzania kuhusu mambo ya uchaguzi.
(2) Bunge laweza kutunga sheria na kuweka masharti
yanayoweza kuzuia raia asitumie haki ya kupiga kura kutokana
na yoyote kati ya sababu zifuatazo, yaani raia huyo-
(a) kuwa na uraia wa nchi nyingine;
(b) kuwa na ugonjwa wa akili;
(c) kutiwa hatiani kwa makosa fulani ya jinai;
(d) kukosa au kushindwa kuthibitisha au kutoa
kitambulisho cha umri, uraia au uandikishwaji kama
mpiga kura,
mbali na sababu hizo hakuna sababu nyingine yoyote

inayoweza kumzuia raia asitumie haki ya kupiga kura.

Sasa utaona wazi mtu mwenye uraia wa nchi mbili haruhusiwi kabisa kupata ruhsa ya kupata haki ya Kupiga kura. Na kama ilivyo kama huna haki ya kupiga kura basi automatic huna haki hata ya kugombea uongozi katika Tanzania.

Hafif hao ni kwa ufupi tu kuhusu haki ya mtu kugombea uongozi wa juu kuhusu Tanzania. Naeza kuzidi bainisha zaidi lakini naona watu wengi wana jazba kubwa na kutotaka wengi wafaidike na darsa hili.

Lakini kama nilivyobainisha awali nitapembua vile vile sheria za kimataifa zinasemaje kuhusu ili nikijaaliwa Insh'Allah baadayn.

kama kuna suala Naruhusu Bismillah..



Nasriyah Saleh Al Nahdi
Doha. Qatar
 

Hivi unachojadili ni nini? Naona kama umeanzia kwenye hitimisho vile. Kwanza weka 'premises' zako wazi ili tuweze kuelewa unachojadili. Halafu, utachambua na kujadili Katiba za nchi gani?
 
Last edited:
Hivi unachojadili ni nini? Naona kama umeanzia kwenye hitimisho vile. Kwanza weka 'premises' zako wazi ili tuweze kuelewa unachojadili. Halafu, uchambua na kujadili Katiba za nchi gani?
.

Acha kudandia Treni kwa mbele Magobe.

Fuatilia mjadala toka mwanzoni ili uweze elewa nafafanua kitu gani.
 
Swaumu hufanya ubongo wakati mwingiene kushindwa kufanya kazi....upuuzi huu...!

Tunasoma katika maandiko kuwa ''Mungu'' Yesu alifunga (swaum) jee ina maana na huyu ''Mungu'' ubongo wake ulikuwa haufanyi kazi alipofunga (swaum?

Jibu bila hamasa tafadhali, kwa sababu hii ya kufunga (Swaum) sio kwa waIslam tu, nadhani hata waKiristo wana siku zao za kufunga ( kwarisima) na mabaniani nao wanazo, na mayahhudi wanazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…